Sensa: Kianalogia siku 1, kidigitali siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Kesho mwisho! Je, ambao bado hawajafikiwa watahesabiwa?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,628
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa ki analogia na ilichukua siku 1 tuu, sasa tunahesabiana kidigitali inachukua siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho. Je, kaya zote zilizobakia zitafikiwa? Je, ambazo hawajafikiwa mpaka kesho watafikiwa? Je, watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
Screen Shot 2022-08-28 at 6.43.34 AM.png
Screen Shot 2022-08-28 at 6.43.49 AM.png


Leo ni siku ya sita ya zoezi la sensa, ambao hatujahesabiwa, tutahesabiwa Kweli?

Ama kweli, mkamia maji hayanywi! Waswahili walisema, jambo ukilipania sana haliwi! Inawezekana hii sensa mimi niliipania sana. Kwa wiki tatu mfulululizo kabla ya sensa safu yangu hii ya kwa maslahi ya taifa ilijikita kwenye kuhamasisha zoezi la sensa, sasa siku ya sensa yenyewe imefika mimi siku hesabiwa! Leo ni siku ya 6 ya zoezi la sensa bado sijahesabiwa! Kuuliza kama tutahesabiwa kweli ni genuine concern!

Kuna ka mtindo kamezuka, ukihoji jambo lolote ambalo wewe kwa mtazamo wako unaona haliendi vizuri au haliendeshwi vema, utanyoonyeshewa kidole kuhusu uzalendo wako. Hii sensa hatukuanza nayo leo, tena tumeihamasisha kikamilifu.

Sensa nilianza nayo hapa Sensa: Je, kuna ubaya kuwauliza watanzania their hopes & expectations of their government? Niko tayari kuhesabiwa, wewe je? kisha nikaja hapa Agost 23, tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa ili kuiwezesha Serikali kujipanga kimipango mkakati ya SMART, kutuletea maendeleo. halafu hapa Natoa wito Agosti 23 tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa na hapa Sensa: Leo ni leo, Kazi ni Moja tu!, Kuhesabiwa! na hapa Shuhudia Sensa Live Kupitia TBC, Nimeshuhudia Live Rais Samia Akihesabiwa. Let's Share Experiences za Sensa na Zoezi la Kuhesabiwa Toka Maeneo Tofauti

Nimeshiriki sensa 4, ya mwaka 1978, ya mwaka 1988, ya mwaka 2002 na ya mwaka 2012, sense ya mwaka huu, 2022 ndio sensa yangu ya kwanza kutohesabiwa siku ya kwanza ya sensa yenyewe. Mpaka leo naandika hapa, leo ni siku ya 6 tangu zoezi la sensa lianze na bado kaya yangu, au mtaa wangu, haujafikiwa!

Siku ya sensa niliianza vizuri kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Rais wa JMT, amenitumia ujumbe mfupi wa maandishi, SMS kuhusu Sensa na nikapandisha bandiko humu Just Imagine Umepokea SMS hii "Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha ...."- Ungemjibu nini?
"Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha kushiriki Sensa tarehe 23 Agosti,2022. Nakusihi utoe taarifa sahihi".

Mimi niliupata ujumbe huu, vipi wewe mwenzagu, pia uliupata?. Umejisikiaje kupokea SMS ya Rais wa JMT kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu? Nani mwenye kumbukumbu yoyote ya Rais wa JMT kuwahi kutuma SMS yoyote kuhusu jambo lolote at person level? Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha..."

Si lengo la makala hii kuingilia kazi ya makarani wa sensa, lakini kwa vile sensa zote zilizopita, ulikuwa unahesabiwa siku ya kwanza, hivyo ile siku ya kwanza ya sensa unakuwa umeipania sana. Kila ukisikia mlango kugongwa, siku siku zote ni kumtuma dada kufugua geti, lakini siku hiyo ni baba mwenyewe unakwenda kufungua geti ili uwapokee mwenyewe makarani wa sensa hivyo kusikia tuu geti linagongwa baba mbio kwenda kufugua geti kukaribisha makarani wa sensa!

Kufika getini na kufungua geti… la haula, kumbe ni mama wa mboga! Nusu ubamize mlango na kutaka kumfurusha mama wa watu kuwa leo hatununui mboga. Mama wa mboga, anamuulizia dada kama leo tunachukua, kumbe dada kamsikia na kuja getini, tunachukua. Pesa utapitia baadae, dada wa mboga nae kasema leo nimepita mapema zaidi ili nimalize mapema na mimi niende kwangu kusubiri kuhesabiwa. Hivyo naomba pesa kabisa maana leo nikipita nimepita sirudi tena njia hii! Uzuri wa waleta bidhaa wa nyumbani siku huna wataacha na kesho yake watapitia. Hivyo dada akamwambia tunachukua utapitia kesho, na siku hiyo ndio baba unashuhudia mboga zikinunuliwa, kisa ni kuwasubiri makarani wa sensa.

Kwa vile sensa zote za nyuma, umezoea kuhesabiwa siku ya kwanza ya sensa, sijui kama ilikuwa ni bahati tuu, lakini kaya nyingine zilikuwa zinahesabiwa kwa siku 7, sijui. Lakini sensa hii leo siku ya 6, nina haki ya kujiuliza kama leo au kesho nitafikiwa kweli?

Hivyo nikaanza kuwaza mbali Tanzania tulipopata uhuru ile miaka ya 60, kuna nchi tulipata nazo uhuru pamoja, zikiwemo nchi zinaitwa Tiger. Ukiziangalia zilikuwa na nani ukilinganisha na sisi tuna nini, nchi hizo zilikuwa hazina kitu, na sisi tulikuwa tuna kila kitu. Lakini leo ukiziangalia zilipo na sisi tulipo, lazima utakubaliana na mimi, sisi tuna matatizo mahali.

Sasa nikilinganisha zile sensa nyingine na hii sensa ya leo, kiukweli kabisa wa dhati ya moyo wangu, kuna tatizo mahali. Hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko mjumbe wake wa nyumba 10, hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko serikali yake ya mtaa, nyumba yangu ni hatua chache kutoka ofisi ya serikali ya mtaa wangu, haiwezekani leo ni siku ya 6 makarani wa sensa hawajanifikia. Wakati inawachukua nusu siku tuu kwa watu wa serikali ya mtaa wangu kuwafikia wakazi wote wa mtaa wangu, kwa nini hawa makarani wa sensa hawakuwa ni wajumbe wetu wa nyumba 10 na maofisa wetu wa serikali za mtaa?

Kama Tanzania sasa tuna vitambulisho vya taifa, vyenye biometric data, na tuna serikali mtandao, nini faida ya vitambulisho vya taifa vyenye biometric data na serikali mtandao kama tunahesabina kijima hivi?

Nimemsikia Kamishna wa Sensa kitaifa Mama Anna Makinda akisema, tungekuwa ni nchi za wenzetu tungejihesabu na kutuma data. Mbona kuna sisi watanzania wengi tuu tuna simu janja, tuna vitambulisho vya taifa, nchi yetu ina serikali mtandao, si wenye uwezo wa kujihesabu na kutuma data tungetuma na karani angepita tuu kuhakiki kwa dakika chache. Zile sensa za kuhesabiwa ki analojia tumehesabiwa kwa siku moja, leo tunahesabiana kidigitali, tunasubiri siku 6 tuhesabiwe, hapa sio kuna tatizo?

Mbona kwenye E Passport tumeweza, E Visa tunaweza, E registrations tumeweza, TRA tunafanya E-Filing, tunashindwa vipi kwenye kitu kidogo kama kujihesabu tuu?

Pamoja na matatizo yote, kwenye mazuri pia tupongeze. Naipongeza televisheni ya taifa kutulea matangazo mubashara ya sensa tukashuhudia ile siku ya kwanza ya sensa ya viongozi wakihesabiwa, na mpaka leo wananchi tukihesabiwa. Hongera sana Dr. Rioba na timu yako kwa kazi nzuri.

Kuna uwezekano Dr. Albina Chuwa ame over stay pale NBS, maana sijui huu ni mwaka wa ngapi pale. Wenzetu wazungu wana msemo hata uwe mzuri vipi miaka 10 ni mwisho, na ndio maana hata vipindi vya uongozi mwisho ni miaka 10. Wakuu wa taasisi za umma mwisho ni miaka 10, vipi hapo NBS?

La mwisho, mfumo wa kidigitali unarahisisha sana kazi, tukijenga mifumo imara hatuhitaji hii duplicity ya vizazi na vifo (RITA), vitambulisho vya taifa (NIDA), idara ya takwimu (NBS), immigration, vunja haya makitu yote. Centralize all the data katika mfumo mmoja, hata ukusanyaji wa kodi hakuna tena kushikana mashati. Kila kitu ni streamlined pamoja.

Nasubiria Kuhesabiwa!

Wasalaam,

Paskali

Update
Hatimaye leo nimehesabiwa!.
Pia nimemsikia Kamishna wa Sensa, Anna Makinda, ametoa tangazo kuwa yeyote ambaye hajahesabiwa, aende ofisi ya serikali ya mtaa wake, akaripoti kuwa hajahesabiwa na kuacha contact number yake, hivyo makarani wa sensa watampigia na kumfuata kumhesabu, hivyo sasa ni Watanzania wote wenye simu ndio watahesabiwa. Ikitokea wewe ni Mtanzania na hujahesabiwa, na hauna simu, then sijui utahesabiwaje?!.

Ila pio dodoso la sensa, lime miss swali moja muhimu sana, na kwangu mimi hilo swali ndilo lenye umuhimu wa pili baada ya swali la kitambulisho cha taifa, hili ni dodoso kuhusu Tin Number na umiliki wa leseni ya biashara.

Nilibahatika kuhudhuria ile semina ya Prof. Hernando De Sotto kuhusu formalization of properties, kila Mtanzania anayefanya biashara yoyote, anapaswa kuwa na Tin Number, na leseni ya biashara ili kujua the tax base!. Kulikiwa ma maswali mengi kuhusu biashara, umachinga, ufugaji, uchimbaji madini but none is as important as tin number na leseni ya biashara!.
Tukisema Tanzania bado tunatatizo la upangaji vipaumbele vyetu, tutakuwa tunajionea Tanzania bado tuna tatizo la upangaji vipaumbele vyetu, baada ya Elimu, Afya na kilimo, ilipaswa ije nishati!. Ni aibu na hatari kupikia kuni na mkaa!

Thanks kwa kuhesabiwa!.
P
 
Leo namsubiri karani. Alikuja saa moja usiku ajasema kesho anaazia hapa.
Lakini huku mtaani kwetu kuna nyumba mamia kwa mamia hazijahesabiwa.

Makarani wanatumia muda mrefu kuhesabu na hata kutembea unakuta wanatembea kama wamemakiza kuhesabu.
Watu wanamwamko Sana wa kuhesabiwa sema haitawezekana kumaliza kwa siku hii iliyobakia. Lazima waongeze siku kama nne.
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Paskali
Kiukweli kupitia hii sensa ilipaswa kuwatoa viongozi wote wa NBS na wanasiasa wanaohusika na hii taasisi. Inatia aibu.
 
Twende pole pole jamani. Hivi mnajua hawa makarani wanalipwa kimafungu mara hawa wamelipwa hivi mara hawa wamelipwa vile na yamkini wapo kata moja na wametofautiana AE na wanajaza dodoso la aina moja. Tusiwalaumu makarani kuna kitu hakipo sawa kwenye mfumo.
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe,
Honestly, kwa nchi kama Tanzania huwezi kufanya sensa kwa siku moja unless kama unakusudia kufanya survey na sio sensa!!

Assume una Makarani 200K wanaotakiwa kuwafikia watu 50M... hapo ina maana kila karani anatakiwa kuwafikia watu 50M/200K = 250

Again, assume unatumia dakika 10 kwa kila mtu... yaani una-include muda wa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Hiyo maana yake kila karani atatumia Dakika 2500 kuwafikia hao watu 250.

Dakika 2500 ni sawa na saa 41... NONE STOP ambazo ni almost 4 days for 10 hours per day!!

That being said, kama siku za nyuma sensa zilikuwa zinachukua siku moja, basi tulikuwa tunapigwa manake hata hizo dakika 10 nilizotaja, ni impractical.
 
Kuwafikia wote inaweza kuwa changamoto. Nina maoni mchache juu ya hili zoezi. Hili zoezi la kuhesabu watu limefanana sana na zoezi la anwani za makazi, niulize tu swali dogo, je zoezi la anwani za makazi tangu lilipoanza miezi 3 iliyopita limekamilika? Jibu ni hapana. Kwanini halijakamilika?

Sensa ya makazi pia inachukua taarifa za anwani ya makazi ambalo halijakamilika bado, kwahiyo kuna taarifa za sensa ambazo zitakuwa na mapungufu mengi mengi
Jana nimeona taarifa ya makaranihuko Nyamagama hawajalipwa na siku zinakaribia kwisha Hili nalo ni tatizo tunaweza kupata taarifa za ovyo.

Swali dogo tu la challenges, ni lini Serikali imepeleka maendeleo sehemu fulani kutokana na takwimu za watu? Nikiangalia mfano madarasa ya uviko, vituo vya afya, stendi nk ni vitu ambavyo vinapelekwa uniform na sio kwa kuangalia idadi ya watu .

La mwisho kungekuwa na option ya kupiga picha kila nyumba iliyopitiwa ikawa saved kwenye taarifa za sensa.
Naamini next sensa watafanyia kazi mapungufu yaliyobainika, naamini hakuna linaloshindikana tujitokeze kuhesabiwa the rest tuwaachie Serikali
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Paskali
Rafiki yangu, kabla ya kuandika anza kufanya utafiti. Sensa zilizopita hakuna sensa ilichukua siku chache kama hii. Unayoita ya 2012 ilichukua siku 14
 
Sidhani kama kweli dhamira yao SENSA, maswali ni mengi sana na yasiyo na mlengo wa Sensa ya watu, na ndio maana wanatumia muda mrefu sana kwenye kaya moja,
Baadhi ya maswali yanafikirisha na kukera,
-mimba zilizoharibika!!!! Ngapi!!
-Umewahi kuolewa!!! Mara ngapi!!
Hapo tukajikuta tumeanzisha mjadala mwingine wa yeye kuulizwa badala ya yeye kuuliza.
Wapewe mwezi mzima ndio watawafikia kaya zote kwa hilo zoezi wanalofanya.
 
Leo namsubiri karani. Alikuja saa moja usiku ajasema kesho anaazia hapa.
Lakini huku mtaani kwetu kuna nyumba mamia kwa mamia hazijahesabiwa.

Makarani wanatumia muda mrefu kuhesabu na hata kutembea unakuta wanatembea kama wamemakiza kuhesabu.
Watu wanamwamko Sana wa kuhesabiwa sema haitawezekana kumaliza kwa siku hii iliyobakia. Lazima waongeze siku kama nne.
Mamia kwa mamia kimahesabu ndio 100×100!??.(3digits×3digits maximum ni 999×999=998001)
Je Kuna mtaa bongo una nyumba 10000-998001?
Too much exaggerations
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom