Rais Samia ahutubia taifa leo Agosti 22, 2022. Ametoa wito na kuwasihi Watanzania wote kujitokeza kuhesabiwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasihi Watanzania kujitokeza kuhesabiwa na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti 2022 ikiwa ni sensa ya Sita kufanyika katika Tanzania huru huku akieleza kuwa matokeo ya awali yatatolewa mwezi Oktoba mwaka huu.

Katika ujumbe wake kwa watanzania alioutoa kupitia vvyombo vya habari usiku wa leo Jumatatu tarehe 22 Agosti 2022 (Saa chache kabla ya zoezi la Sensa) Rais Samia amewakumbusha Watanzania umuhimu wa kutoa taarifa sahihi kwani taarifa hizo ni muhimu kwa mipango ya maendeleo ya taifa na amewatoa hofu watanzania akieleza kuwa kila taarifa inayokusanywa itatunzwa kwa mujibu wa sheria kwani ni kosa kisheria kwa karani wa Sensa kutoa taarifa yoyote aliyoikusanya.

Rais Samia ameeleza kuwa kutokana na ukubwa wa nchi yetu, makarani hawatoweza kuwafikia watu wote kwa siku moja hivyo amewasihi wale wote ambao hawatofikiwa siku ya kwanza ya Sensa (23 Agosti 2022) kutunza kumbukumbu za wale wote watakaolala katika kaya usiku wa kuamkia siku ya sensa ili kuwezesha taarifa hizo kutolewa kwa usahihi pale ambapo makarani watafika.

Kwa mara ya kwanza Sensa ya mwaka huu itajumuisha ukusanyaji wa takwimu za majengo yote nchi nzima hivyo kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi juu ya ubora wa makazi ya wananchi. Kukamilika kwa zoez hili kutaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuunganisha sensa ya watu na makazi.

Rais Samia pia amewasisitiza wananchi kutowaficha watu wenye ulemavu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mila potofu kwani kufanya hivyo kutaikwamisha Serikali kupanga kwa usahihi namna ya kuwahudumia watu hao.

Kwa kawaida sensa hufanyika kila baada ya miaka 10, ambapo kwa miaka ya nyuma imewahi kufanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002, 2012 na kumbukumbu zaidi zinaonesha kuwa kabla ya uhuru, kwa upande wa Tanganyika Sensa ilifanyika mara 5 (Mwaka 1913, 1921, 1931, 1948 na 1957 huku Zanzibar wakifanya sensa mara moja tu mwaka 1958 ingawa sensa za kabla ya uhuru zilikosa vigezo vingi vya kisayansi.

 
Samia kawapa Wahadzabe kitoweo cha Nyumbu ishirini ili kesho wasiende kuwinda wahesabiwe

Raisi mkarimu sana tofauti kabisa na Jinamizi .

Kumbuka Wahadzabe ni Kabila linalotoweka katika Ardhi kama juhudi za Serikali hazitafanyika.
 
Sawa
Tutarajie Baadhi Ya Machache Ambayo Ni Haya:-
(a) Sensa
(b) Tozo
(c) Uelekeo Wa Serikali
 
Back
Top Bottom