Shughuli ya kuaga mwili wa Hayati Edward Lowassa Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam

Hakuna mnafiki, kama umemsikiliza Warioba vizuri amesema Lowasa aliwekewa vikwazo na mowamo wa kuwa rais hata na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mungu hakutaka Lowasa awe rais, hivyo hawa akina Nyerere na Kikwete walitumika tu.

Ni ujinga kumlaumu Yuda kwa kumsaliti Yesu wakati ilikuwa ni mpango wa Mungu.
Khaaaa Mungu anasingiziwa na mengi jmn
Mungu ?!! Mna uhakika?
 
Noma sana
🤣🙌

Mkuu upo eneo la tukio? Hivi mwakyembe anaon kana hapo?
Maana Kila nikifuatilia matukio simuoni🤷
Hapana mkuu, niko mbali sana. USA.

Wanasiasa wasivyo na aibu, usishangae ukimuona Mwakyembe naye kashika mic anaomboleza kifo cha kiongozi mahiri Tanzania.

Msiba wa Mzee Lowassa umenikumbusha mbali sana.

Shule ya msingi, alikuwa ni kati ya wazazi waliokuwa wanakuja sana shuleni kufuatilia elimu ya watoto.

Kabla ya siasa hapo.

Alikutana sana na rafiki yake mwalimu Ndosi. Sasa Ndosi katangulia na Lowassa kafuata.

Alivyoingia kwenye siasa na kuhimiza mambo ya elimu nilijua huyu baba anamaanisha kutoka moyoni, haya si maneno ya siasa tu.

Kwa sababu nilimuona alivyokuwa anafuatilia elimu kabla hata hajaingia kwenye siasa.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba mpya na Waziri mkuu mstaafu mzee Warioba amesema kwenye Uchaguzi Mkuu wa 1995 Lowassa aligombea Urais Lakini Jina lake halikufika Kamati kuu lilikatwa

Warioba amesema " Lowassa alikuja nyumbani kwangu Oysterbay na kunieleza jinsi alivyoumia roho kwa Jina lake kukatwa bila hata kuhojiwa na kusikiliza"

Warioba amesema alimshauri Lowassa asikae na maumivu moyoni bali aende kwa Mwalimu Nyerere akamueleze dukuduku lake

Lowassa akamwambia Mzee Warioba kuwa hana njia ya kuweza kumfikia Nyerere ndipo Mzee Warioba akampigia simu msaidizi wa Nyerere na kumwambia anaomba amkutanishe Lowassa na Mwalimu Nyerere kwani Edward ana jambo la kuzungumza na Mwalimu

Ndipo Lowassa akapewa nafasi ya kwenda kumuona Mwalimu Nyerere na Wakazungumza na kuyamaliza kabisa

Source: TBC msibani
 
JK kaenda tu kukamilisha ratiba. Kwa kuwa alipangwa kuongea basi ikambidi kuongea.

Hakuweza kumzungumzia Marehemu kwa ukaribu, lakini pongezi apewe Dkt Warioba kwa kutokuwa mnafki.

Alale salama Edward.
 
Ukizungumzia waasisi wa UFISADI ndani ya Taifa la Tanzania, huwezi kuacha kumtaja marehemu.

Apumzike panapostahili.

Kauli ya Warioba kuwa lowasa alikuwa na uchungu sana baada ya kuambiwa Nyerere ndiye alizuia urais wake 1995 imenifikirisha mengi kuhusu ugonjwa na kifo cha Nyerere.
 
EL ali prove kwamba yeye ni zaidi ya CCM kwa kushinda uchaguzi Mkuu 2015.

Dola ikagoma kumtangaza..lakini sisi watanzania tunajua kwamba Rais wa Tanzania 2015 alikuwa Edward Lowassa baada ya kushinda uchaguzi Mkuu.
Sasa hivi hata ukiweka Mbuzi au Bata agombee na Mgombea wa CCM, Mgombea wa CCM atashindwa tu.
Kinachoiweka CCM Madarakani ni mfumo unaowalea, ni mfumo huohuo unafanya utakacho hata ukitaka kuuza bandari au nchi au mbuga watampa wamtakaye. Watanzania siyo wenye nchi bali ni walipa kodi tu, kama watahisi kuchoshwa milango ipo wazi kusepea watakako, lakini kama ni nchi watu wameshaigawana na kujimilikisha.
 
Siyo kwa uwezo ama matakwa yake, bali ni kwa kudra za aliye juu. Maana Warioba ni mlevi wa kutupwa wa pombe kali.
Mimi Huwa nawa ambiaga watu ukimkuta mwanaume hajawai kutumia kilevi chochote basi mwanaume huyo hajawai kuishi....

Msibani Kwa ENL mzee warioba kaongea Kweli tupu Yani Punch after punch mzee ni mtu mkweli na mjenga hoja mzuri sanaa

Mzee warioba ni hazina Kwa taifa
 
Mbona sasa mnatuchanganya tuliambiwa JK na ENL 1995 walikuwa na lengo moja la kuunda team ya kushinda Urais, sasa imekuwaje Lowassa awe na kinyongo Jina lake kutofika CC wakati swahiba wake alifika hadi tatu bora za 1995.
 
Hapana mkuu, niko mbali sana. USA.

Wanasiasa wasivyo na aibu, usishangae ukimuona Mwakyembe naye kashika mic anaomboleza kifo cha kiongozi mahiri Tanzania.

Msiba wa Mzee Lowassa umenikumbusha mbali sana.

Shule ya msingi, alikuwa ni kati ya wazazi waliokuwa wanakuja sana shuleni kufuatilia elimu ya watoto.

Kabla ya siasa hapo.

Alikutana sana na rafiki yake mwalimu Ndosi. Sasa Ndosi katangulia na Lowassa kafuata.

Alivyoingia kwenye siasa na kuhimiza mambo ya elimu nilijua huyu baba anamaanisha kutoka moyoni, haya si maneno ya siasa tu.

Kwa sababu nilimuona alivyokuwa anafuatilia elimu kabla hata hajaingia kwenye siasa.
Okay , comment yako nikahisi umerudi bongo nini😅
Nimekusoma👍

Uko sahihi wanasiasa ni wanafiki jmn mpk sio poa 🙌🙌
 
Mbona sasa mnatuchanganya tuliambiwa JK na ENL 1995 walikuwa na lengo moja la kuunda team ya kushinda Urais, sasa imekuwaje Lowassa awe na kinyongo Jina lake kutofika CC wakati swahiba wake alifika hadi tatu bora za 1995.
Mi nimesikiliza warioba kaongea kule karimjee, nimemuelewa...Wala hajapepesa macho ...

Lkn pia nimesikiliza clip ya zamani sn lowasa akiwa mzima baada ya like sakata la Richmond
Lusekelo kaongea ,aisee Dunia hii🙌🙌
Tena kasema naongea akiwa hajafa maana watz wanafiki wataongea akifa...
 
Back
Top Bottom