Kikwete: Lowassa ameacha alama zitakazokumbukwa daima

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye shughuli ya kuaga mwili wa hayati Edward Lowassa kwenye viwanja vya Karimjee,

“TUMSHUKURU Mwenyezi Mungu kwa muda aliotupatia wa kuishi na kuhudumiwa na ndugu Edward Ngoyai Lowassa, wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu, na ameacha alama zitakazokumbukwa daima. Shukrani kubwa tunayoweza kuitoa kwake kwasasa ni kumuombea kwa Mola aiweke roho yake mahala pema peponi” -Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

📹 AzamTV
 
Nimerudia rudia hotuba za JK katika msiba wa Lowasa, hakuna mahali kasema alienda kumsalimia Lowasa akiwa anaumwa.

Ni Lowasa ndye alimpa JK urais, Lowasa anaumwa JK hajatia mguu hospitali.

Je, marafiki zako unawaamini kiasi gani, na umejifunza nini kwa usaliti aliofanyiwa Lowasa na JK?
 
Mzimu wa Lowassa utamtesa sana Jakaya,kwani bila kupepesa maneno,mateso,madhira aliyoyapata Lowassa yana mkono wa Jakaya.hata akatae namna yoyote ile,dunia na watanzania karibu wote wanafahamu hilo.

Hata kifo cha Mkapa na Magufuli anahusishwa pia,hii si nzuri kwa afya ya akili yake,

Rejea Blaise Compore alichomtenda Thomas Sankara
 
Eti Lowassa ndiye aliyempa Urais Kikwete! Utakuwa mzaliwa wa miaka ya 2000. Jakaya tayari alishakuwa kwenye mstari wa Urais toka miaka ya mwanzo ya tisini na hapakuwa na mtu aliyekuwa anamzidi umaarufu na kukubalika kama Jakaya ndani na nje ya CCM. Mtu pekee aliyeweza kumdhibiti Kikwete kuchukua urais mwaka 1995 alikuwa Hayati baba wa Taifa. Lowassa na Rostam waliona fursa na sio kumpa Urais.

Na sio lazima aseme alienda kumtazama. Nje ya siasa hao watu waliendelea kuwa Marafiki na wanajua a faulo walizochezeana.
 
Eti Lowassa ndiye aliyempa Urais Kikwete! Utakuwa mzaliwa wa miaka ya 2000. Jakaya tayari alishakuwa kwenye mstari wa Urais toka miaka ya mwanzo ya tisini na hapakuwa na mtu aliyekuwa anamzidi umaarufu na kukubalika kama Jakaya ndani na nje ya CCM. Mtu pekee aliyeweza kumdhibiti Kikwete kuchukua urais mwaka 1995 alikuwa Hayati baba wa Taifa. Lowassa na Rostam waliona fursa na sio kumpa Urais.
We hujui, kama nyerere asinge kata jina la lowassa mwaka 1995, Lowassa angekua Rais wa awamu ya 3.
 
Nimerudia rudia hotuba za JK katika msiba wa Lowasa, hakuna mahali kasema alienda kumsalimia Lowasa akiwa anaumwa.

Ni Lowasa mdoye alimpa JK urais, Lowasa anaumwa JK hajatia mguu hospitali.

Je marafiki zako unawaamini kiasi gani, na umejifunza nini kwa usaliti aliofanyiwa Lowasa?
haina maana na haikua na haja kueleza mengi.
Mzee ameumaliza mwendo, imani ameilinda 🐒

R I P Laigwanan comrade ENL
 
We hujui, kama nyerere asinge kata jina la lowassa mwaka 1995, Lowassa angekua Rais wa awamu ya 3.
Hakuna aliyemjua Lowassa na hakuwa na umaarufu. Tishio la Kikwete llikuwa Malecela na Cleopa Msuya. Lowassa alipata umaarufu mkubwa kipindi Cha Mkapa na mwaka 2005 alijua asingeweza kushindana na Kikwete ndio maana akakubali kuungana na Kambi ya Jakaya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom