Should CHADEMA Fire Zitto?

Should CHADEMA Fire Zitto?

Should Zitto get FIRED from CHADEMA?

  • YES

    Votes: 137 65.9%
  • NO

    Votes: 57 27.4%
  • May be

    Votes: 10 4.8%
  • I don't know

    Votes: 4 1.9%

  • Total voters
    208
Status
Not open for further replies.
Kama kweli ushahidi ukipatikana basi itabidi aondoke zake maana cdm wanapinga rushwa , ufisadi n.k ila nitasikitika sana kwa mwanasiasa kama zitto kukumbwa na kashfa kama hiyo duuu.
 
Ulipoanza, hukuchanganya mambo ya Urais, umeuliza kuwa should the party fire him? If you want to speak of Urais nadhani ungeiweka post yako ikae vizuri zaidi. Issue hapa ni yeye kuwa fired endapo itathibitika kuwa amechukua Rushwa. Ikiwa amechukua, ameshasema atawajibika, irregardless of the stand of the party!!! Unless kama sijakuelewa thread yako, i stand to be corrected...Kama hajachukua Chama hakiwezi kumuwajibisha!Unamuwajibisha mtu kwa kitu ambacho una uhakika nacho na si vinginevyo.

Hayo ya Urais unayaleta ni mengine!

Nakuunga mkono, Walicho kifanya Muhongo na Maswi nikuwachanganya wabunge wakashindwa kujadili ufisadi wa makampuni yanayo zalisha umeme km vle Songs, Agrco, Iptl nk na kujadili tuhuma za ztt! Yaani bunge la upinzani limekosa mwelekeo wamenasika ktk mtego wa ccm! Badala ya kujipanga nijinsigani ya kufanya kuhusu spika na naibu wake wanavyo dhibiti upinzani, tuliwategemea sana cdm lkn kwa style hii Basi tena, vyama vyaupinzani Tanzania ni tatizo sana! Naanza kuamini maneno ya Mwl Kambarage "MPINZANI WA KWELI ATATOKA CCM
 
PRESS CONFERENCE: MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Video kwa hisani ya zittokabwe wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Jambo linalonitatiza ni watu Zitto anaowatupia lawama dhidi ya shutma hizo.Ukimsoma vyema utagunduwa anawalalamikia wenzake ambapo walitakiwa wawe together.Statement yake haijasaidia chochote.However nakubaliana na maoni yako.
Mkuu jmushi1, Zitto ni Polarizing figure. Bila kujali ametendewa au amatenda dhambi ninasema kwa uhakika he is a polarizing figure.

Kama unafuatilia habari zake tangu 2010 amekuwa mtu wa utata sana hasa pale chama kinapoonekana kuimarika.
Sina maana anakihujumu, lakini utakumbuka operesheni Sangara ilipopamba moto ni yeye aliyesababisha ikafifia.

Sasa suala la uenyekiti wa kamati ya bunge na urais vinatoka wapi?
Suala la wabunge wenzake kumpiga vita linatoka wapi?
Huko kwenye kamati nadiriki kusema hakuwa makini.
Haiwezekani awe mwenyekiti siku zote halafu baada ya kuvunjwa ndipo atoke na kusema kuna madudu.

Zitto bado anaamini kuwa Kafulila alionewa na wala hajakanusha kauli za udini au ukabila kwasababu Kafulila aliyetoa maneno machafu na mazito bado ni mshiriki mkubwa wa ZZK, yeye alijotoa mhanga kwa aijili ya ZZK.
Tamasha la Kigoma ni mwendelezo wa falsafa ya ujana hata kama kufanya hivyo kutaleta madhara ndani ya chama

Mh ZZK anaamini kuwa yeye peke ni chadema na hivyo hahitaji timu ya chama.
Ukifuatailia utaona jinsi gani mwezi huu alivyoua M4C kwa hoja na mambo yanayoonyesha political immaturity nzuri tu.

Chadema wana window of opportunity ya kuwaondoa CCM as of today. CCM hawakubali kirahisi na wanauzoefu wa kisiasa mkubwa wa kugeuza hali ya kisiasa.

Jambo lolote linaloweza kuleta mtafaruku ndani ya Chadema basi ni mtaji kwa CCM.
Hakuna ubaya kwa Zitto kutanganza nia, lakini alizingatia nyakati na busara za kufanya hivyo?

Hoja yangu ni kuwa hadi utakapopatikana ushahidi wa kutosha, CDM hawana haki ya kumchukulia hatua.
Zitto naye asifikirie political career kama solo candidate, lazima afanye kazi na wenzake na ajue ni maarufu kwasababu ni sehemu ya chama maarufu. ZZK anatakiwa awe kiungo cha CDM na si kigawe au kigawo.

I stand to be corrected, historia inaonyesha ZZK ni muumini wa siasa za ujana,anadhani ni beacon CDM, mara nyingi amekuwa anakigawa chama, ana misimamo yenye utata sana hata yale yenye masilahi ya taifa.

Chadema nao wanapaswa kubeba lawama, tumewatahadharisha mara nyingi sana juu ya mfumo wao wa kufichana na kuficha matatizo. Haya tunayoyaona ni mwendelezo wa akina Juliana Shonzo, Kafulila,Tuntemeke n.k.
CDM wamechukua mfumo wa kufuga watu na si taasisi kama lilivyo CCM.

Kwa mahali ilipo CDM wanatakiwa wawe na uangalifu sana, ni make au break.
Wakiongozwa na kanuni, sheria na taratibu watavuka mawaimbi haya, wakifuata upepo na emotional decision they're done! Very fine and thin line to walk on.
 
PRESS CONFERENCE: MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Video kwa hisani ya zittokabwe wa youtube
Zitto amekosea kusema wenzake ndo wameingia mtegoni,mi nadhani either yeye ndo kaingia mtegoni,ama kawaingiza wenzake mtegoni.Nadhani siasa za Zitto ni very divisive.Route aliyoichukuwa anajuwa kuwa hata kama anataka a more powerfull position,cost yake itakuwa kubwa.Na yeye anafahamu,kweli kawatega chadema.Ndo maana anawaambia kuchafuliwa kwake ni ni kuchafuliwa kwa chadema,so ni wazi malalamiko hayo ni dhidi ya wenzake.I can't believe this stuff.Zitto uliingia mtegoni kwa kujweka karibu na mafisadi na kusapoti baadhi ya issues zao.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz
Napita tu huyu jamaa si alidai yeye sio mwanachadema hebu nikumbushe unajua thread zimekuwa nyingi sana humu JF

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Issue ya rushwa ni ya kipuuzi kama uzinzi. Unaweza ona katoto kazuri kenye uzoefu katik mchezo ingawa ni kadogo kiumri, kimekula sana maisha waziwazi na wakubwa kuliko wewe, ila siku zinavyokwenda kinaanza kutega, kinakutafuta kama mshauri, halafu kinaamua weka wazi mambo kuwa kinakuzimia na kinavyokujua kinaamini kuwa kuwa nawe maisha yake yatabadilika sana.Ghafla akili inaanza kulainika na kuifikiri hiyo option, and then occassionally kinatokea kwa style ya kuhamasiza zaidi akili yako.Then unalegea, unajisikia kuhesabu 1, 2 , unastop, siku inapita.Then akili inakosa uvumilivu, halafu natokea mtu kukafukuzia mbele yako, unapata wivu bila kujijua, na hali ya kutaka wahi inaongezeka .Then mazingira yanakuja tena unaanza hesabu 1,2 unashangaa umepita 3.Unafanya zoezi rasmi.Katikati ya Tukio unashtushwa na kujilaumu kwa ulichofanya baada ya kuona mamlaka ikikutia hatia hatiani, marafiki wanakushangaa, watoto, na mchumba /mke wako anakushangaa anakuchukia, anakuona kuwa hata mwanao unaweza mnanii, na mwanao naye kama yupo naye anaanga kuogopa, ghalfa inakuwa habari ya nchi hata kama ulikuwa hujulikani hata ktk nyumba kumi za jirani.

Rushwa ina mbaya zaidi ilikunyemelea wakati una hitaji hela na watoa rushwa walikuwa na predatory strategies.Huna ujanja unakuwa prey within seconds, halfu unashindwa elewa kwanini watu wa karibu nao wanakuchukia wanakuacha pekee yako uilezee hiyo hali.Ni haki yao kwa vile hawakuwa nawe wakati ulikuwa unajenga mazingira ya kudakwa, wakati ukitoa utetezi kuwa hao wawindaji hawakuwezi kwani umeshakomaa na kuwajua vya kutosha.Pengine pia ukaongeze nyama kuwa hii ndio njia ya wewe kunasa mambo yao.

CIA huwa wakituma operative wao huwa wanatuma na mtu mwingine wa kumtazama, ili asijejikuta amekuwa addicted/au hata kuangukia katika mapenzi na tamaduni au hata uatartibu wa anayewindwa.Hata wagonjwa wa waganga hujikuta wakiolewa na waganga.

Kama mh atakuwa ameanguka kweli basi CDM watakuwa na kipindi kigumu sana:
-Kumtupa si vyema kwani pia alikuwa na mchango.
-Kumtunza bado ni shida kwani kam ni addict basi ,once occassionally atakuwa akienda onja unga kambi ya jirani.
-CDM kumtuza kuta compromise misingi yao, kwani watakuwa na double standard na baadaye CCM wakaamua tumia kama fimbo.Kwani hata suala la posho, CCM wamejitahidi kulalama kuwa CDM wanapokea.

-Kama ni kweli na Takukuru wakalivalia njuga, kupigana kumtoa ni kuingilia utawala wa sheria, na hata akitoka itabidi awe mjumbe wa halamshauri kwani public image itakuwa ni burdden.

ZItto ndiye anayejua ukweli hadi sasa,kabla hizo tuhuma hazijachukua sura mpya.Anapaswa kuwa na busara ,ajitahidi kuminimize impact na ajaribu kutokihusisha chama na mapungufu yake kwa kiasi awezacho.Awe kama marion Jones,yule dada mkimbiaji aliyekuja thibitika kutumia dawa, alikubali makosa yake, akawajibika kwa kulipa fine na kurudisha medali zote, na kupata kifungo ch amiezi kadhaa.sasa anaishi kwa furaha ana amani,sasa yupo kuru kushiriki ibada, kukaa na watu kwani keshatoa hatia.

Kama Zitto atakuwa amehusika basi atakuwa na test ingine katik nafsi yake ,kuukubali ukweli hata kama utakuwa umemaliza kabisa nguvu ya kutangaza nia.Atakuwa na test ya kulinda chama, na wengine ambao hawakuhusishwa.Atakuwa na Test ya kutoona matatizo yake yamesababishwa na wana CDM wengine.Kwani bado takukuru wanaweza anzisha upelelezi wa kuzuia suala kama sasa tunavyoambiwa kuwa suala lipo mahakamani, litakalomfanya apoteze nafasi ya CDM hata kama baadaye itagundulika otherwise.

Pia kama hana hatia pia inabidi awe na mpangilio mathubuti wa kujitoa na kuiaminisha jamiii kuhusu hilo na kuwafanya wenzie warudi katik hali ya kawaida na upendo kama zamani wakati cdm ikiwa just another party
 
Mkuu Ritz
Napita tu huyu jamaa si alidai yeye sio mwanachadema hebu nikumbushe unajua thread zimekuwa nyingi sana humu JF

Chama
Gongo la mboto DSM
Mkuu ninazo na thread za ccm humu,fuatilia,nilishakata nao tamaa,huwezi kuwawatetea kama hunufaiki na ufisadi,very simple...
 
Nicholas,nashangazwa sana na Zitto.Mafanikio yake kweli mbali ya kuwa yeye ni charismatic,yametokana na chama chake.Hata hivyo kuna dalili za ubinafsi,kwasababu mafanikio yake huwa anajicredit,however anataka chama chake nacho kiwe mashakani kwaajili ya tuhuma zake za rushwa.
Ni kwasababu tu sasa tumeshazoea,lakini nilishangazwa sana mara ile ya kwanza waliposhirikiana na JK kuunda kamati ya madini,kuanzia wakati ule,si ajabu kukuta watu tuliowaamini wakiwaback up suspicious people.Na kuwa na suspicious decisions.Its true that you can't fool everyone...Can't fool all the people all the times.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ninazo na thread za ccm humu,fuatilia,nilishakata nao tamaa,huwezi kuwawatetea kama hunufaiki na ufisadi,very simple...

Wewe kama umekata tamaa kivyakovyako si bado tupo tunaendelea na vita, ahahaaa mkuu sitegemei ajira ya CCM na wala sijanufaika na huo ufisadi ila nilinufaika na sera za CCM na serikali ya kielimu hata Chadema mafisadi wapo wengi tu!

hivi kama unataka kujuwa tofauti kati ya chadema na ccm,subiri ccm waondolewe madarakani ndo utajuwa nani fisadi na nani si fisadi...

Hayo maneno unayozungumza wewe,ni ya kishabiki,watu wamefisadi nchi halafu unakuja na hoja dhaifu kiasi hiki?Niambie hao mafisadi wa chadema na ufisadi wao,halafu naomba usiniulize ufisadi wa magamba maana hapatatosha hapa.
 
Nicholas,nashangazwa sana na Zitto.Mafanikio yake kweli mbali ya kuwa yeye ni charismatic,yametokana na chama chake.Hata hivyo kuna dalili za ubinafsi,kwasababu mafanikio yake huwa anajicredit,however anataka chama chake nacho kiwe mashakani kwaajili ya tuhuma zake za rushwa.
Ni kwasababu tu sasa tumeshazoea,lakini nilishangazwa sana mara ile ya kwanza waliposhirikiana na JK kuunda kamati ya madini,kuanzia wakati ule,si ajabu kukuta watu tuliowaamini wakiwaback up suspicious people.Na kuwa na suspicious decisions.Its true that you can't fool everyone...Can't fool all the people all the times.

Shida yeye mwenyewe na wafuasi wake hawajui pia kuna misuse of charisma.Hawajui hata cell za mwili huwa zikichangawa na kupata kichaa huanza kutafuna mwili hadi mtu kufa kwa kukonda.Na wengi wetu tunaopiga kelele humu ndani na kuonekana tupo kinyume ni kuwa tunapenda ana achukue positive move mapema.
 
Nicholas,nashangazwa sana na Zitto.Mafanikio yake kweli mbali ya kuwa yeye ni charismatic,yametokana na chama chake.Hata hivyo kuna dalili za ubinafsi,kwasababu mafanikio yake huwa anajicredit,however anataka chama chake nacho kiwe mashakani kwaajili ya tuhuma zake za rushwa.
Ni kwasababu tu sasa tumeshazoea,lakini nilishangazwa sana mara ile ya kwanza waliposhirikiana na JK kuunda kamati ya madini,kuanzia wakati ule,si ajabu kukuta watu tuliowaamini wakiwaback up suspicious people.Na kuwa na suspicious decisions.Its true that you can't fool everyone...Can't fool all the people all the times.
Jmushi1, mkuu umebonyeza kidonda maana hapa ndipo utata ulipoanzia. JK kumweka Zitto ktk kamati ya madini alifanya makusudi kabisa lakini Zitto alifikiri kwamba anaaminika sana baada ya kufumua zengwe la Buzwagi.. Zitto angetumia akili kidogo tu angeelewa kwamba katumiwa hasa baada ya mkataba wa Buzwagi kupita akiahidiwa sheria itabadilika mwaka 2010.

Kuna ukweli mkubwa kwamba Zitto bado immature kisiasa japokuwa mwanzo alipata ushauri mkubwa sana toka kwa Salim A. Salim na sijui kama alimjenga kisiasa au ndio alimweka sawa baada ya kuiona PUPA yake kuruka bila mabawa. Na kama sikosei ni baada ya kuchaguliwa tume ya madini na kuwasha mgogoro mkubwa ndani ya chama hasa Mnyika akimpinga wazi wazi nilianza kuziona dalili za utengano na Zitto kwa kiburi ama kuajiamini akajisogeza karibu zaidi na sera za CCM..

Muda mwingi nadhani hakuwa na imani na baadhi ya watu Chadema na hasa ilipotokea la kugombea uenyekiti ndipo alipoanza kuuona ukweli kwamba CDM haikumchukulia kama alivyotegemea. na kilicho haribu zaidi mahusiano yake na viongozi wengine ni kuondolewa kwa Kafulila, hii nadhani ilimpa shock kwake maana aliamini kabisa kijana anaweza kuvumiliwa kutokana na kwamba chama kinamhitaji kama Mtaji wa kuchukua Kigoma..Nadhani hii pia ndio ilosukuma hadi kutaka kugombea Uenyekiti tena kwa habari tulizopata hapa JF ni kwamba Zitto aliletewa form akiwa Airport na mwanachadema sijui nani?.ili kugombea wenyekiti, haikuishia pale likaja swala la Dowans nalo akatofautiana na wenzake kabla ya matokeo ya Urais mwaka 2010..Hizi ndizo sehemu kubwa ambazo Zitto anatakiwa kutazamwa kwa makini zaidi na pengine kumwonyesha njia.

Lakini haya ya tuhuma za rushwa jamani tuyaache hayana mpango kabisa maana hakuna ukweli wowote isipokuwa nyie ndio hamjui kinachochezwa nyuma ya pazia.. Tanesco ni sehemu ya kuchuma na kuna watu wamewekeza vibaya sana..yaliyopita Tanesco hatutaweza kuyaona kamaMhando hataitwa kutoa ushahidi wa tuhuma za yeye kufukuzwa maana kuna Mhando kupinga uwekezaji wa mashirika ya umeme wa dharura na Mhando aliyempa mkewe tender..Mkataba ule ule wa Richmond na Dowans umekuwa passed to Symbion kwa mwenye kuelewa maana atajua kuna habari nzito zaidi. Richmond ilikuwa ya Marekani na Symbion ya Marekani.. who real owns Symbion ni kitendawili.

Zitto hawezi kula rushwa isipokuwa kosa lake ni kuto share infomation alizonazo na viongozi wenzake, yeye anataka kulipua bomu jingine na kujipatia umaarufu ambao timing yake ilikuwa mbaya safari hii. Tatizo la Zitto ni ambition yake, anapenda sana kuonekana kafanya jambo kubwa kwa wananchi. Yaani yeye Zitto kawezesha kadhaa wa kadhaa ktk utawala wa JK..Well, ni lazima tukubali kwamba Zitto ana mapungufu yake na pengine kujiamini sana kupita kiasi kama asili ya Wabembe na Wazaire. Ina uzuri wake na ubaya wake hasa unapokutana na watu wa makabila mengine. Mbowe anapenda kuwa urais siku moja, lakini Zitto kaupenda zaidi...

Zitto anautaka Urais na sii pekee Chadema, isipokuwa tofauti ni kwamba Zitto anataka kuweka nia yake wazi mapema na hivyo kujikuta anaropoka hadi bungeni mahala pasipo husika kabisa lakini anajuaa watanzania wengi wanamsikia na kumwona ktk luninga..Hakuna asiyependa sifa lakini mkuu wangu Zitto anapitiliza sana. Pengine anataka kufanya kama JK alivyofanya CCM mwaka 2003. Hii ina hatari zake kisiasa na repercussion zake ndio mzigo unaomrudisha nyuma kwa kila hatua anayo piga kwenda mbele utadhani chura aliyetumbukia shimoni..Mra zote kwa wajuzi wa siasa husema politically incorrect is a joke of immaturity!..

Hivyo mchukulieni kama alivyo japokuwa anaweza kabisa kutuvuruga akili kama tutakuwa tunafuatilia kila hatua yake na aanafanya nini..Zitto sio mla rushwa na pengine kajiingiza ktk shimo ambalo haoni nje ni swala la sisi kumwekea ngazi atoke shimoni maana mwenzetu huyu. Dream yake aendelee kuwa nayo hakatazwi lakini akubali tu maneno yake mwenye kwamba ni wananchi wanachagua mgombea wao sio swala la Kupenda kuwa rais. Wananchi wakimpendekeza hewallah!.

Now, let's get a life - wazungu wanasema. Haya ni mambo ya mpito maadam rais atapendekezwa na kuchaguliwa na wananchi hofu ya nini?, hivyo Zitto sio mtoto mdogo kusoma wakati. Hana sababu ya kula rushwa kabisa ikiwa yeye mwenyewe anajiandaa kugombea Urais iwe mwaka 2015, 2020 au 2025 lakini sii kwa tiketi ya Ujana maana hata kina Nyerere, Banda, Kenyatta, Obotte, Kaunda na viongozi wengine wote walikuwa vijana na wametawala kwa miaka zaidi ya 20, lakini walishindwa kutuondoa ktk umaskini.

Lakini nchi za wenzetu ambazo viongozi wao walikuwa mature hasa za Ulaya wameweza kuondokana na umaskini toka enzi za kutawaliwa..Na nina hakika hawa vijana wa leo wakiingia madarakani watazeekea madarakani na wagumu sana kukubali kuachia baada ya miaka 10.. Hii ni historia tosha ya nchi zetu za kiafrika ambazo tumekuwa na marais vijana na wameiingi ktk Udikteta haraka zaidi kwa sababu huwa bado hawajakomaa kisiasa na tamaa ya uongozi kuiacha ujanani ni kishawishi kikubwa cha kukataa kushindwa ikiwa hukumaliza maazimio yako..
- Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania..
 
hivi kama unataka kujuwa tofauti kati ya chadema na ccm,subiri ccm waondolewe madarakani ndo utajuwa nani fisadi na nani si fisadi...

Hayo maneno unayozungumza wewe,ni ya kishabiki,watu wamefisadi nchi halafu unakuja na hoja dhaifu kiasi hiki?Niambie hao mafisadi wa chadema na ufisadi wao,halafu naomba usiniulize ufisadi wa magamba maana hapatatosha hapa.

Mafisadi wa Chadema mbona wako wengi unaye Mwenyekiti Mbowe &CO, unaye Dr. Slaa wapo wengi tu tatizo lenu mna ugonjwa wa kupenda chongo mnaita kengeza

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mafisadi wa Chadema mbona wako wengi unaye Mwenyekiti Mbowe &CO, unaye Dr. Slaa wapo wengi tu tatizo lenu mna ugonjwa wa kupenda chongo mnaita kengeza

Chama
Gongo la mboto DSM
Wameibia nini nchi?Ona jinsi kauli yako ilivyokuwa shallow analytically,yani unasema ama unaongea almuradi umeongea.Ulilielewa swali nililokuuliza?
 
Wameibia nini nchi?Ona jinsi kauli yako ilivyokuwa shallow analytically,yani unasema ama unaongea almuradi umeongea.Ulilielewa swali nililokuuliza?

Unajua watu kama nyie ambao mpo kwa kutafuta maslahi ya kimaisha kupitia vyama vya siasa mna matatizo sana, wewe ndioy umekuwa mfinyu waki fikra na sijui kama unaelewa nini unachokisema yapo mambo mengi machafu yanafanyika na ndiyo yanayoleta mzozo mkubwa ndani ya Chadema hivi wewe kwa akili yako Fuso iliyotumika ilinunuliwa kwa Mil. 350; mwenyeketi alijipa tenda kupitia mlango kwa kushirikiana na wapambe bila kuitangaza tenda zaidi ya mil. 300, katibu mkuu kujipangia mshahara wa mil. 7 kwa mwezi; katibu mkuu kulazimisha kujengewa nyumba katibu mkuu kumpa tenda hawara yake yapo mambo tu ni ufisadi kama ule tunaoupigiia CCM; wengi wenu mnatumika kumpiga vita Zitto sababu yote ni kuwa wapo wanachadema wakweli wanauona ufisadi huo, hata mchakato wa matumizi ya ruzuku ni siri ya watu wawili. wewe kama umeamua kuhamia Chadema eti kwa kukimbia ufisadi wa CCM naona kama unajipotezea muda ukweli hao viongozi wako tayari wameshaonesha ni mafisadi, fisadi ni fisadi tu hakuna fisadi mdogo wala fisadi mkubwa; watu kama nyie ambao ni shallow minded ndio mnarudisha nyuma harakati za kweli za ukombozi hapa unatumika au unajipendekeza kwa viongozi wa Chadema; ni hivi unapoteza muda wako kumjadili Zitto eti Chadema wamfukuze, Zitto hakuchaguliwa na wanakigoma kwa mapenzi ya Chadema; wao wamemchagua Zitto kama Zitto leo akihamia TLP hata mumsimamishe Dr. Slaa Kigoma Zitto ni kijana wao na ndio chaguo lao. Ni nyie wanachedema msiojielewa mnachokiongea si mpo mstari wa mbele kupiga kelele za Mhando wa Tanesco je alichokifanya Mhando kina tofauti na matendo ya Mbowe na Dr. Slaa Chadema?

ningetaka maslahi ya kimaisha, ningejiunga na gambaz mafisadi...tumia akili mkuu.
 
ningetaka maslahi ya kimaisha, ningejiunga na gambaz mafisadi...tumia akili mkuu.

Ahaaa haaaaaaaaa acha kuzuga mkuu mpo wengi tu ndani ya JF mnafahamika!! Ufisadi upo Chadema labda ningekushauri anzisha chama chako mbona hujajibu ufisadi wa kina mh. Mbowe na Dr. Slaa? Somo limeeleweka

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom