Albedo,Mtanzania Mbona Ukada unakufanya unakuwa Kipofu hivi
CDM wameshawahi kuwatuhum u CCM kwamba walipitisha Magari yao bila kodi TRA wakawataka CDM wapeleke USHAHIDI. Lakini TRA baada ya kusikia Nape anasema Slaa halipi kodi TRA wakaanzisha Uchunguzi. Mkuu Mtanzania Wananchi wanaona na kupima Usanii wote huu na naamini una mwisho wake.
TRA ni wezi tu na ndio maana wameamua kupambana na CDM
Nijuavyo mimi CCM walilipa kodi ya magari hayo na kutoa ushahidi. Kama una ushahidi tofauti basi ni vizuri kuumwaga hapa JF.
Hata kama CCM hawakulipa basi nao wanafanya makosa hayo hayo.
Hili si suala la kisiasa na tukilijadili kisiasa tunakosea mno. Kama CCM wameishingia bango CHADEMA basi ndio muda muafaka kwa CHADEMA nao kuja na ushahidi kuonyesha CCM wana kwepa kodi.
Pia ni vizuri kama mtu unataka kuleta mabadiliko basi uwe whiter than white. Itakuwa ni makosa makubwa sana kwa CHADEMA kufikiri wanaweza kutumia njia zile zile chafu za CCM kwasababu CCM nao wanafanya. Watu hupenda kubaki kwenye status quo unless mabadiliko yataleta mambo mazuri zaidi.
Yaani haiingii akilini chama cha siasa kushindwa kulipa kodi lionekane jambo la kawaida. Nitaelewa kama wametumia accounting principles kukwepa kulipa kodi kwa kutumia sheria zilizopo kama yanavyofanya makampuni mengi makubwa. Lakini kushindwa kabisa kulipa hata kodi za ajira za wafanyakazi kwa kweli hapo ni dalili kwamba sisi sote ni wababaishaji tu na siasa zetu za kudanganyana. Hilo halijalishi ni CCM au CHADEMA.