Shoka la TRA latua CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shoka la TRA latua CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 9, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Monday, 08 August 2011
  NA HAMIS SHIMYE
  , Gazeti la Uhuru

  [​IMG]


  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeitoza faini ya sh. milioni 100 CHADEMA, baada ya kubainika inakwepa kodi tangu ilipoanzishwa mwaka 1992. TRA pia imeanza kukata kodi mshahara wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa na watumishi wengine wa CHADEMA.

  Habari za kuaminika kutoka ndani TRA zilisema ulipaji faini unaanza mara moja, baada ya uchunguzi kukamilika na kuonyesha chama hicho hakilipi kodi.

  "Tumemaliza uchunguzi na kubaini CHADEMA hailipi kodi ya mishahara ya kila mwezi ya watumishi wake tangu ilipoanzishwa,'' kilisema chanzo chetu cha habari.

  Imeelezwa kuwa, CHADEMA imekiuka sheria na kanuni za ulipaji kodi, zinazotaka mtu, kampuni au taasisi yoyote kulipa kodi TRA.

  "Ijapokuwa tangu ilipoanzishwa ilikuwa hailipi kodi, katika uchunguzi tulipata taarifa za kuanzia mwaka 2000 hadi sasa zinazoonyesha hailipi kodi,'' kilisema chanzo hicho.

  Kutokana na hilo, chama hicho kinapaswa kulipa faini ya sh. milioni 100 na kimeamriwa kulipa kodi ya mishahara ya watumishi wake kuanzia mwezi uliopita.

  Chanzo hicho kilisema CHADEMA imeiandika barua TRA ikidai wanacholipana ni posho na si mishahara.

  Hata hivyo, sheria ya kodi inaeleza kiwango chochote cha posho kinachozidi kima cha chini cha mshahara kinapaswa kukatwa kodi.


  Watendaji ambao TRA imeanza kuwakata kodi ni Dk. Slaa, ambaye analipwa mshahara wa zaidi ya milioni 7.4, fedha ambazo ni nyingi kuliko mshahara wa mbunge.


  Mshahara huo unatokana na mapendekezo ya Azimio la Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana Januari 29 na 30, mwaka huu, mjini Dar es Salaam, ambapo mshahara huo umegawanya katika sehemu sita.

  Sehemu hizo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi, ambapo mshahara wa mwezi ni sh. 2,300,000.


  Fedha za mafuta ni sh. sh. 1,387,000 kwa wastani wa lita 750 kwa mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. milioni moja.


  Posho kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa mshahara kama huo.  Last Updated ( Monday, 08 August 2011 19:34 )


  CHADEMA yakiri kukwepa kodi


  Tuesday, 09 August 2011 20:09


  NA SULEIMAN JONGO  KATIBU Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibroad Slaa, amekiri kuwa chama chake kimetozwa faini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hatua hiyo imetokana na chama hicho kudaiwa kukwepa kulipa kodi za mishahara na posho za watumishi wake kwa miaka kadhaa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, jana, Dk. Slaa alisema TRA imeitoza CHADEMA faini ya sh. milioni 94. "Ni kweli tumepigwa faini na TRA kulipa sh. milioni 94, kwa kutolipa mishahara ya watumishi wetu.

  Tutalifikisha hilo katika vikao vya juu na tutalipa tu," alisema Dk. Slaa.


  Alisema kuwa tayari wamepokea barua kutoka TRA inayowataka kulipa sh. milioni 94, kama adhabu ya kutolipa kodi za watumishi wake. Hata hivyo, katika hali ya kushangaza Dk. Slaa alisema kuwa CHADEMA haijalipa kodi tangu kuanzishwa mwaka 1992, haijalipa kodi za watumishi wake kwa kutofahamu.  Pia, alisema kuwa walikuwa hawafahamu mabadiliko ya Sheria za Kodi, ambayo huko nyuma mishahara ya watumishi inayotokana na fedha za ruzuku ya serikali.

  Wakati huo huo, CHADEMA kimeshauri kutazamwa upya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) baada ya kukosa mwelekeo katika kutimiza majuku yake.
  Dk. Slaa alisema mkanganyiko katika mambo mbalimbali yanayotokea kwenye sekta ya nishati na maji yanatokana na ulegevu wa EWURA na kutotimiza majuku yake ipasavyo.
  Alisema lengo la kuanzishwa EWURA ni kusimamia na kuratibu huduma mbalimbali zinzohusiana na maji na nishati ya mafuta na gesi, jambo ambalo linafanya kuwepo na haja ya kuitazama upya EWURA.  Kwa mara ya kwanza habari za CHADEMA kukwepa kodi ziliibuliwa na gazeti hili, ambapo baada ya TRA kufanya uchunguzi wake ilibaini ni kweli na sasa itavuna mamilioni ya shilingi kama adhabu, ambazo zitasaidia kutoa huduma kwa jamii.
   
 2. P

  PWERU Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lazima tudhibiti wakwepa kodi ili kukuza uchumi wetu.
   
 3. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  eeeh, siasa bwana??!!

  hivi kwenye vyama vingine hali ikoje? katika vyama takriban 18 vilivyosajiliwa ni chadema tu ndio walikuwa "wakorofi" kwenye masualal ya kodi? hata hivyo wawe makini kama haya madai ni ya kweli na ya haki kwani harakati zao zina gharama sana na hii ni mojawapo
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hawa TRA ile consultancy fee ya Idd Simba (Milion 285) kutoka Simon group wamechukua kodi? Vipi CCM,CUF, TLP wamewadai ngapi????????
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,220
  Likes Received: 1,626
  Trophy Points: 280
  Wameshasakiziwa!

  Wakati wa uchaguzi mbona CCM waliingiza magari bila kulipia kodi (nakumbuka kama vile somehow sheria iliwalinda, baada ya kuingiza tu wakaweka sheria ya kuwabana wengine. Hopefully watabadilisha tena hapa kati ili wafanye vitu vyao then wabadilishe tena). Big up CCM! Kusanyeni kodi mtatue matatizo yetu wananchi!

  TIP FOR TRA: Kuna wahindi wengi tu mjini wanawapa mshahara mameneja wao kwenye bahasha ili wasikatwe kodi, mkiweza kuwamulika tutashukuru sana
   
 6. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,310
  Likes Received: 4,754
  Trophy Points: 280
  hizo ni habari za gazeti la uhuru.ndo maana hajataja chanzo.
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,639
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe...

  Kesho utasikia dr slaa kashinda kesi na kesi imeisha halafu baada ya miez 2 kuna chama kinakwepa kodi...
   
 8. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,491
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Swali:Chadema walikuwa wanalipa kodi?.....Huu ni ufisadi wa hali ya juu,kuweni mfano bora jamani dah!!!
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,328
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 160
  Kulipa kodi ni lazima kwa kila mtu au taasisi yoyote. Kama CHADEMA walikuwa hawalipi ni makosa na wanastahili kulipa hiyo faini haraka na wasirudie tena.

  Jambo ninalojiuliza hapa ni kuhusu vyama vingine! Kwanini CHADEMA peke yake? Hao TRA walikuwa wapi kwa miaka 19? Kama walikuwa wanalipwa na vyama vingine, mbona hawakukikumbuka CHADEMA? Anayetakiwa kukusanya hiyo kodi anawajibika vipi kwa kutokutekeleza majukumu yake?

  Kwa kifupi maswali ni mengi kuliko majibu!
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Jamaa yangu aliye makao makuu ya CCM Lumumba ananitayarishia document ya kuonyesha kuwa CCM nayo hailipi kodi katika mambo yao mengi sana -- mishahara ya baadhi ya watendaji wake, kodi za majengo, viwanja mbali mbali chama hicho inavyovimiliki etc. Hii itamwagwa kwenye gazeti moja la kila wiki hivi karibuni.

  Wananchi msihofu kabisa kuhusu hili, ni ukweli kabisa na itaonyesha kuwa kama vile TAKUKURU, Polisi, etc, TRA nayo inatumiwa na CCM.
   
 11. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 931
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hapa nani alaumiwe? TRA au CHADEMA? Kwani TRA imekuepo kuanzia lini na majukumu yake siku zote ilisahau au ilikuwa wapi tangu 1992 - 2011? Waache unafiki!
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hee, una maana wasomaji wa Uhuru nao wanatambua kuwa gazeti lao ni la udaku? Kwa nini anaficha chanzo?
   
 13. m

  mopaomokonzi JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mfano mbaya sana kutokulipa kodi huku unasema serkali haifanyi kitu, ingekuwa nchi za wenzetu wangeburuzwa mahakamani
   
 14. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,491
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Kwa chama cha siasa au mwanasiasa kutolipa kodi ni jambo la aibu sana!!...kuhusu hayo maswali mengine,mimi naona ni sawa na kumkatalia mtu mwingine asijikinge na jua kwa kutumia kivuli chako....it won't solve your problem!
   
 15. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,797
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Serikali inatafuta pesa kwa udi na uvumba ili bajeti tuliyosomewa isipwaye...
   
 16. N

  Nipe tano Senior Member

  #16
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ile HOJA ya NEPI kuwa Chadema wanakwepa kodi sasa linaitafuna Chadema BAADA ya tra kuwapiga fine CHADEMA ya tshs 100mill.
   
 17. p

  politiki JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,330
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hakutaja chanzo kwa sababu chanzo cha hii habari ni kutoka gazeti la uhuru, gazeti ambalo thamani yake ni
  chini ya toilet na linaendeshwa kwa ruzuku asilimia 90% kwani hakuna mtu mwenye busara anayesoma gazeti la uhuru.
   
 18. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 5,920
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  They have to comply. Mbowe ni mfanyabiashara wa siku nyingi, lazima atakuwa ana ufahamu mkubwa wa mambo ya kodi. Kudai kuwa kiasi anacholipwa Slaa ni posho hivyo hakistahili kulipiwa kodi ni upotoshaji mkubwa.

  Kipindi hiki tunaposonga mbele si vema kuanza kufanya vitu vinavyoutia mashaka umma unaotuunga mkono. Hata hivyo zoezi hili lisiishie kwa CDM tu. Taarifa nilizonazo ni kuwa Mbatia anavuta pesa ndefu kuliko hiyo ya Slaa. TRA mulikeni maeneo yote.
   
 19. n

  niweze JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kikwete kagundua njia nyingine ya kuwafuatafuata chadema, kikwete na wahuni wenu. The problem ya Kikwete na Ndulu na mkullo uwezo wenu ni mdogo sana wa kufikiria - unajua kabisa CHADEMA wata-demand records zote za TRA ziwe public from previous years, mtaweza kuonyesha mafisadi wote wanalipa kodi?

  Hizo kodi za CCM inalipa records zipo wapi? Records za Taifa kwanini kikwete inazifungia? Si muonyeshe public nani analipa na nani alipi mbona mnachagua only chadema? Tutaona nani atatoka mshindi katika hili saga mnaanzisha wakati mkijua politics of hate na ubaguzi hazijawahi kufanikiwa popote pale duniani.
   
 20. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,465
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  Teh teh teh
   
Loading...