wanaotakiwa kulipa kodi hii inayoongelewa (PAYEE) ni wafanyakazi wala si chama au taasisi! Hapo ndo tunapopotoshana....Anayelipa kodi ni mwajiliwa na si mwajili.Sasa mbona wanaituhumu chadema wakati wao(CHADEMA) ni waajili tu?
Wakuu,
Tuache politics hata kwenye mambo ya maana kwenye ustawi wa nchi yetu. Suala la kulipa kodi ni wajibu wa kila mtu na kila mwajiri kuhakikisha anafikisha kodi ya wafanyakazi wake TRA. Kitendo cha chama cha siasa chochote kile kutokulipa kodi ni cha kusikitisha sana.
Inapotokea kwamba hata watu wanaotaka kuwa viongozi wa nchi yetu hawalipi kodi kwa visingizio vyovyote vile ni jambo la kusikitisha mno. Mimi namwelewa Dr. Slaa na mapambano yake dhidi ya ufisadi. Hata siku moja nisingetegemea Dr. Slaa apokee mshahara wake bila kulipa kodi. Ningetegemea awe na mjanja vyakutosha na kusema hapana, hapa kuna tatizo.
Kwa sheria zet za kodi wenye kosa hapa ni CHADEMA maana kama mwajiri lazima uhakikishe kila mfanyakazi analipa kodi. Lakini pia mwajiriwa una hata moral responsibility ya kuzijulisha mamlaka husika pale unapoona jambo fulani haliko sawa.
Arguments nyingi tunazotoa hapa ni shallow mno kwa maana ya kwamba kujifanya hujui sheria si utetezi kwenye mambo ya sheria. Ninaamini CHADEMA, CCM na vyama vingine vina watu wenye elimu zao na ambao wanajua kwamba ni wajibu kwa kila raia mwenye kipato kulipa kodi.
TRA imeshindwa kazi na is not fit for purpose. Inakuwaje kwa miaka yote hii wameshindwa kujua kwamba vyama vya siasa vina mapato ya kutosha kwa wafanyakazi wao kulipa kodi? Inakuwaje miaka yote hii wameshindwa kukusanya hata senti tano kutoka CHADEMA?
Je kuna vyama vingapi vingine ambavyo havilipi kodi? Kuna watu wangapi wengine ambao hawalipi kodi? Haya mambo yanafanyika wakati Machinga na wauza vitumbua mitaani wanalipishwa kodi kupitia leseni. Iweje hawa watu ambao wana mapato kidogo sana wanalipa kodi wakati wenye mamilioni hawalipi kitu? Huyo CEO wa TRA anaendelea kupewa muda wa kuongoza shirika kwa mafanikio gani wakati Watanzania wengi tu wenye mapato hawalipi kodi?
TRA ni failure na kuna haja ya kuifanyia mabadiliko makubwa ili kodi ikusanywe hasa kutoka kwa matajiri mbalimbali ambo wanakwepa kulipa kodi.
Kule kwetu Kyela sisi tulipoanza biashara, moja ya majukumu niliyowapa vijana ilikuwa ni kuonana na TRA na kujadiliana nao juu ya nini tunatakiwa kufanya kwenye suala la kodi. Sisi tuna majengo pale tunakodisha vyumba vya biashara, mikataba yote tunaipeleka sisi wenyewe kwa hiari yetu TRA na kuhakikisha 10% withholding tax ya pango inapelekwa.
Hata tulipoanza biashara zingine tumeenda kuwaona na wametupa ushauri mzuri tu na kutushukuru kwa kutambua umuhimu wa kulipa kodi. Kwa nilivyowaona mimi tungeweza kuendesha biashara zetu bila kulipa kodi kama tungelitaka. Lakini kama ni mfanybiashara ni muhimu kuwa na uhusiano mzuri na mamlaka ya kodi.
Hata ukiwa na matatizo ni kuwaambia ili waone kama wanaweza kukusaidia. Kama umejenga uaminifu kwao nina uhakika hata kama una shida kuna nafasi kubwa ya kukuelewa na kukuruhusu kuchelewa kupeleka kodi au kulipa taratibu.
Ningependa kuona vyama vya siasa vyote vinatoka clean kwenye hili. Wahakikishe wafanyakazi wao wote pamoja na vifaa vyote vinavyonunuliwa kwamba vinalipiwa kodi. Vinginevyo wananchi tusahau kupata nafuu yoyote kutoka kwa hawa viongozi wetu. Binafsi ningependa TRA iunde tume ambayo ipite kwenye kila chama na kuhakisha wanakagua mahesabu yao yote na kuangalia wapi wanakwepa kodi.
Adhabu ya 100m kwa kushindwa kulipa kodi kwa miaka 11 ni ndogo sana. Kuna haja ya kuwafilisi na kuwapeleka jela wale wanaoshindwa kulipa kodi kama wanavyofanya Wajerumani na hii ndio itafanya watu wawe waoga.