Mkuu Mkandara,
Kwanza, nimeongelea ruzuku kama njia mojawapo ya mapato ya vyama vya siasa. Wana mapato yao mengine. Pia wana wafanyakazi ambao wameajiriwa na wanatakiwa kulipa kodi. Hiyo kodi ya wafanyakazi ndio haijawahi kupelekwa TRA. Sasa kama wewe unafaidika na ruzuku ambayo inatokana na kodi ya Watanzania, ningetegemea uwe wa kwanza kuelewa umuhimu wa kulipa kodi.
Pili, suala la mtu aliyeajiriwa, kodi yake hulipwa na mwajiri wake. Kwenye suala la Dr. Slaa ni kosa la CHADEMA kwamba hawajalipa kodi yake. Ingelikuwa amejiajiri hapo ndipo yeye mwenyewe angetakiwa kuhakikisha kodi yake inalipwa TRA. Lakini ukisema chama cha siasa hakilipi kodi, huwezi kuwaondoa viongozi wake wakuu katika lawama.
Tatu, Suala la viongozi kuwakilisha mali zao tume ya maadili, halina uhusiano na kodi au TRA. Hilo ni kwa lengo la kujua kama wamezipata hizo mali kihalali au la.
Nne, sijaona mahali popote wakisema Dr. Slaa alipokuwa mbunge hakuwahi kulipa kodi. Kodi ya mbunge inakusanywa na ofisi ya bunge au wizara ya fedha (sina uhakika nani analipa mishahara ya wabunge) na ndio wao wanaiwakilisha serikalini. Ambao hawajawahi kulipa kodi ni wafanyakazi wa CHADEMA. Dr. Slaa alikuwa hajalipa hiki kipindi cha hapa mwishoni ambacho mshahara wake sasa unalipwa na CHADEMA.