Shirika gani lilikufa na bado linakuuma?

Shirika gani lilikufa na bado linakuuma?

Mi inaniuma sana NMC na RTC! Kiukweli hii nchi inahitaji mkono wa Mungu vinginevyo tunaangamia na kuangamiza vizazi vyetu, leo hii watoto wamekuwa wakisomeshwa mashirika kama historia ya nchi wakati wenzetu wanafundisha kama contemporary issues za kimaendeleo!
 
Umenichekesha na hii habri maana dah!Nikikuona nitakukumbusha hapa nipo na Colleague wako wazamani kacheka hadi basi!
KakaKiiza, huyo jamaa ni collegue wa wapi?, shule?, chuo?, Jeda?, au kwenye media?.
Ila mashirika haya tumeyaua wenyewe na kuendelea kuwapa waliotuulia sasa nchi ndio hii angalau hatuui bali tunaiuza kwa mkopo kwa Mchina!. 2015 tunawapa tena ili wakamilishe kazi nzuri wanaotufanyia hawa watu!.
Pasco
Pasco
 
Mimi naona walifanya makosa sana maana tulikuwa na viwanda vingi sana na ilibidi tukae tuandae mpango kazi wakubinafsisha kuliko tulivyofanya sasa hivi na hii ndo ilisababisha kifo cha Mwalimu Nyerere...............Hataari sana mfano Tanganyika Peckers walimpa Admijee akang'oa mashine zote motor na akafanya kiwanda ghara sasa maana ya kubinafsisha ilikuwa kuwapa watu wenye uwezo kuboresha zaidi siyo kubadirisha matumizi maana baada ya serikali kujitoa rasimi katika maswala ya kuendesha uchumi kwa kuendesha shughuli za uzalishaji!Kama mimi nakuwa rais ninawawajibisha wote waliohusika na kuhujumu taifa hili hasa katika



mchakato wakubinafsisha mashirika!!



mimi yote yananiuma,tulikuwa na mashirika approx 400..
truth be told sisi wenyewe tunastahili lawama,undugu,uvivu na usela mavi ulizidi baadhi yakafa..
ila kwa leo nakataa kuamini hata TTCL ,a monster who owns and controls over 80% ya telecoms infrastructure
linashindwa hata kutoa huduma ya simu ikiacha hawa makurubembe wa kikaburu,waarabu,wahindi na kina kabaang watushike maskio..yaani hata haya hatuna looh...jamani..hapa kwa TTCL,TRC,Tazara,Nic bima mi napata huzuni hadi nalia...
Yaani natamani wale kina Karl Peters na wadachi waje watutie mboko tupate adabu...
 
Rtc,

national milling,

mikate ya siha,

bora shoe company limited,

mwatex, mutex

tanganyika pakers

ilula soap company.

Hi-soap mbeya
 
Deci.
Nililiwa laki 1.5 yangu ya ujana nikitegemea kuvuma pesa kibao.
Kumbe daaah sijui mpaka leo hizo pesa ziko wapi??
 
Mkuu hata haya yaliyopo binafsi ninaona kama yamekufa tu, kilichobaki ni kuzikwa.
Ila hakuna taasisi iliyokufa na kuniuma kama Kiwanda cha Mbolea cha Tanga na Shirika la Reli enzi hizo tunaliita "Relwe".
 
Mashirika haya yalikua yakifanya kazi saa 24,hivyo kuwa na shift 3 ajira kibao,mabasi ya wafanyakazi,wakulima kuuza vyakula ktk canteen za wafanyakazi yaani mzunguko wa pesa unakuwepo
 
KakaKiiza, huyo jamaa ni collegue wa wapi?, shule?, chuo?, Jeda?, au kwenye media?.Ila mashirika haya tumeyaua wenyewe na kuendelea kuwapa waliotuulia sasa nchi ndio hii angalau hatuui bali tunaiuza kwa mkopo kwa Mchina!. 2015 tunawapa tena ili wakamilishe kazi nzuri wanaotufanyia hawa watu!.PascoPasco
Media mkuu!Ninahuhakika Nyerere akifufuka leo atakufa hata kabla ajalala usiku mmoja!R.I.P JK.Nyerere
 
Ooooohh, nakumbuka: GENERAL TYRE, NATEX, GAPEX, SCOPO, NASACO, STC, GEPCO, DARTEX, AISCO, HOSCO, TACOSHILI, KAMATA, TADECO, Tanga Fertilizer, UFI, nk. Katika haya yanayoniuma sana ni: GENERAL TYRE, GAPEX, NASACO, STC, TACOSHILI, KAMATA, Tanga Fertilizer, na UFI. Kwani haya yalikuwa yanagusa maiosha ya kila mtanzania mwenye kipato cha chini. RIP mashirika hayo.

Mwalimu Nyerere.jpg

,
 
kiwanda cha katratasi mgororo(iringa) PAMOJA NA KWAMBA % KUBWA YA KUFA KWA MASHIRIKA HAYO ILITOKANA NA SISI WENYEWE , LKN LAWAMA NIIPELEKE KWA SERIKALI ZAIDI, NA ILIPOKUJA KUHARIBU NI PALE ILIPOANZA ZOEZI LA KUBINAFSISHA. MAANA KTK HILI VIONGOZI WALIKUWA NA AJENDA YAO NYUMA YA PAZIA.
 
General Tyre, sitakaa nisahau maisha yangu yote, nilishuhudia ikifa ghafla! nikipitaga pale Machozi yananilenga!
 
kampuni ya mabasi ya KAMATA na mabasi ya KAURI pia kampuni ya biashara ya RTC kuna viwanda vya nguo MWATEX,SUNGURA TEX,URAFIKI,kiwanda cha zana za kilimo pale urafiki jina nimesahau UFI NA RELWE
 
Hakuna shirika ambalo hadi kesho nalililia kama General Tyre! Najiuliza, inakuwaje shirika life wakati uingzaji wa magari nchini ni mkubwa zaidi (reflecting big market) kuliko kipindi chochote kile katika historia ya nchi hii....!!
 
Back
Top Bottom