Shirika gani lilikufa na bado linakuuma?

Shirika gani lilikufa na bado linakuuma?

>>UFI - Ubungo Farm Implements
>>TFC - Mbolea Tanga
>>TFC - Cenema zenye mafundisho za akina Yombayomba
>>TPPI -Tanzania Pyrethrum Processing Industry
>>SPM - Makaratasi Mgololo
>>ATC - Original []Winne.com - Report on Tanzania, Getting ready for take off
>>TRC - Enzi hizo Leyland CD, Albion Cargo and Passengers, Reli na Meli
>>KSC - Sukari Kilombero
>>VOIL -Mafuta yatokanayo na mbegu za pamba****
>>BHESCO
>>AISCO
>>National Panasonic
>>TAFICO
>>NAFCO
Mlioko Mwanza - Tunaambiwa kuna kiwanda kilikufa kabla hakijazinduliwa kipo upande wa kulia ukitokea Nyegezi kuelekea mjini kabla hujachepuka kwenda Butimba TTC
 
Shirika la Reli bana na laana ya kuzamisha MV Bukoba yaani nayo imezama mazimaaa wala hatukuhangaika kama janga la MH370 ya Malaysia.
 
:embarassed2:Yaani vifo vya haya Mashirika vinauma sana,yameuawa na Watanzania wenzetu!.
 
mimi kiwanda cha kutengeneza viatu bata.... na reli
 
Wana bodi najua wengi wenu mnakumbuka baadhi ya mashirika yalifilisiwa na mengine kubinafisishwa kwa bei ya chee!mfano NBC namengineyo mengi!ila mimi nakumbuka mashirka kama NASACO,TANGANYIKA PAKERS,TACOSHIL;MANG'ULA,FAIBERBOARD,GENERAL TYRE,na mengineyo!mimi lina niuma GENERAL TYRE je wewe?

Tanesco mkuu!
 
Hakuna shirika ambalo hadi kesho nalililia kama General Tyre! Najiuliza, inakuwaje shirika life wakati uingzaji wa magari nchini ni mkubwa zaidi (reflecting big market) kuliko kipindi chochote kile katika historia ya nchi hii....!!
Kilichoiua general tyre ni kampuni ya matairi ya kenya baada ya General tyre kuingia ubia na continental kenya ikabidi waje wakenya kuomba kazi general tyre baadae wakaifilisi kijanja YANA ikawa imara kwakuwa ilikuwa imeingia ubia na Firestone nawakati huo Firestone inakashifa ulaya yakupasuka mipira yake nakusababisha vifo! Continental ikawa ndo kinara hapo ndo wakaiujumu general tyre na leo kenya inawika.
 
Dah! Unfair competition beat techniques... hii inatumika sana kwenye unfair business world!
 
mashine tools pale njia panda ya machame!
uwiiii
 
Wapi Tanzania Elimu Supplies Nakumbuka nikisoma Pale Bunazi Primary School-Mkoani Kagera Tulikuwa tunapewa Madaftari,Pencel Zimeandikwa Elimu Supplies,Bic dah leo mtoto unagharamia kuanzia chekechea!
 
Back
Top Bottom