Mkuu Kaka Kiiza, mimi nimemkumbuka mtu aitwae John Colos Kapinga! (RIP), huyu Mzee alikuwa GM wa Sukita!, sidhani kama kuna mtu alikuwa anakata mshiko mkubwa kama Sukita!. Enzi hizo 1995 mimi ndio naingia TV newsroom kwa mara kwanza, by then bahasha za waamdishi zilikuwa hakuna na ikitokea ni 1,000 tuu mwisho 5,000. Ukienda SUKITA, hata kusalimia tuu, unaondoka na bahasha ya laki!.
Kuna siku ilikuwa Jumamosi fulani, kulitokea bad news ya Sukita, sijui wafanyakazi waligoma, hivyo wakaja newsroom kulalamika, wakarekodiwa ili watokee kwenye news ya usiku. Jumamosi hiyo, news akafunga news mapema tuu by saa saba mchana, desk nikaachiwa mimi!. By saa 9, habari zikamfikia Mzee John Kolos Kapinga, kuwa vijana wamemchafua kwenye media!. Ilipigwa simu toka Sukita ikimuulizia editor!, si nimeachiwa desk, nikaitwa, kuisikia tuu ni sauti ya Kapinga, nilipojitambulisha tuu, nikaamriwa kuchukua taxi na kamera haraka sana, kwenda Sukita, kurekodi the other side!.
Kufika tuu, Boss katueleza amepata habari kuna vijana wanapita news kumchafua!, secretary akaelekeza kuweka fungu nene kabisa kwenye bahasha!, Mzee akasema tushughulikie hiyo issue vizuri!, nikamshauri asijibu malalamiko, bali aseme anything positive ili kufunika, just incase hao jamaa wameenda newsroms mbalimbali!, akasema kote ameisha rekebisha, tulibaki sisi!.
Tukarudi zetu newsroom!, kufika ilibidi ile story ya malalamiko ife, story ya Sukita ni mafanikio tuu!. (Kiukweli, we were bad boys, that was then). Kumbe editor anaangalia news, kuona ile news ya Sukita aliyoiacha yeye haipo, imekuwa replaced na news nyingine!, alinipigia simu, nikamweleza ukweli!, akaja juu kuwa on Monday, lazima nifukuzwe kazi!.
Ile Jumatatu asubuhi, kwenye post mortem editor akawaka ile mbaya, akemwandikia ofisa utumishi, ili nipewe barua ya dismissal!, ofisa utumishi akamwambi editor, haya yakifika kwa DG editor nae atakuwa in hot soup!, kwa nini afunge news saa 7!, editor anatakiwa awepo wakati news inakuwa load kwenye TX kwa nini hakuwepo?!.
Mchana huo kumbe na editor nae aliitwa Sukita, kurudi, kesi iliisha!.
Hiyo ndio ilikuwa SUKITA, mkombozi wa waandishi wa habari!.
Ile bahasha haikuwa rushwa!, ilikuwa ni bahasha ya uwezeshaji, kuzuia news za upotoshaji, zinazochafua good reputation ya shirika la umma, SUKITA, zisienee!, kumbauka
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa ...
Pasco.