Shirika gani lilikufa na bado linakuuma?

Shirika gani lilikufa na bado linakuuma?

KakaKiiza

Platinum Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,947
Reaction score
9,460
Wana bodi najua wengi wenu mnakumbuka baadhi ya mashirika yalifilisiwa na mengine kubinafisishwa kwa bei ya chee!mfano NBC namengineyo mengi!ila mimi nakumbuka mashirka kama NASACO,TANGANYIKA PAKERS,TACOSHIL;MANG'ULA,FAIBERBOARD,GENERAL TYRE,na mengineyo!mimi lina niuma GENERAL TYRE je wewe?
 
Hivi na yale ya mikoani yanaruhusiwa? Mimi KAUDO na DOWICO waliifilisi hawa wazee wetu halafu saivi wanajifanya waheshimiwa sana mi naumia wewe acha tu
 
Mimi kcu inaniuma sana wazee walipigishwa shule leo hii wanakula wameshindwa kurudisha fadhila kwa kurivive hili shirika ili wakulima wasomeshe na watoto wengine. So sad
 
Nikiliona tu neno General Tyre na nikikumbuka enzi hizo nikiwa mitaa ya Njiro tukienda kupiga soka kwenye viwanja vya general tyre nahisi hadi machozi kunitoka

Ni juzi tu lakini leo ukipita hapo utafikiri jumba la makumbusho lililosahauliwa kutunzwa

Hii inaitwa kula mnyama na ngozi yake, hubakizi hata ushahidi
 
Kilimanjaro Machine Tools nadhani ndilo shirika muhimu sana kwetu kama kweli tulitaka kusonga mbele kwenye viwanda....bahati mbaya wajanja waliiba kila kitu na bado wanaendelea kumalizia hata vilivyobaki.
 
Mimi naona walifanya makosa sana maana tulikuwa na viwanda vingi sana na ilibidi tukae tuandae mpango kazi wakubinafsisha kuliko tulivyofanya sasa hivi na hii ndo ilisababisha kifo cha Mwalimu Nyerere...............Hataari sana mfano Tanganyika Peckers walimpa Admijee akang'oa mashine zote motor na akafanya kiwanda ghara sasa maana ya kubinafsisha ilikuwa kuwapa watu wenye uwezo kuboresha zaidi siyo kubadirisha matumizi maana baada ya serikali kujitoa rasimi katika maswala ya kuendesha uchumi kwa kuendesha shughuli za uzalishaji!Kama mimi nakuwa rais ninawawajibisha wote waliohusika na kuhujumu taifa hili hasa katika mchakato wakubinafsisha mashirika!!
 
Back
Top Bottom