Shirika gani lilikufa na bado linakuuma?

Shirika gani lilikufa na bado linakuuma?

aisee KakaKiiza mie nilisononeka sana pale viongozi wetu walipokubali kukiua kiwanda cha kusafisha mafuta (TIPPER).. maumivu yote tunayoyapata sasa na mfumuko huu wa bei umechangiwa kwa kiwango kikubwa na kuuliwa kwa kiwanda kile.. Nakumbuka wakati ule yanaletwa mafuta machafu.. yanasafishwa hapa hapa kwa gharama ndogo na ndani kupata sampuli kama tano hivi.. Ninaamini kabisa kama TIPPER ingelikuwako bado kusingelikuwa na gharama kubwa ya mafuta kama leo.. Ulikuwa ni uhaini wa kiwango cha juu.. Ndio maana Mwalimu alisema kama mtu akikupa mawazo ya kijinga na wewe unajua kwamba mawazo aliyokupa ni ya kijinga na ukayakubali basi atakudharau sana.. Leo tunadharauliwa mno.. foreigners wanajua chochote watakacho Tanzania watakipata.. Loliondo ni mfano mwingine wa wazi kabisa..
Lakini hao hao waliokuwa nyuma ya mpango huo wakapewa uwaziri mimi sijui hii nchi hakuna wenye maono au mtu akiisha ingia pale magogoni basi mipango yote inavurugika??maana hata kwenye kampeni na utendaji tofauti!!

tena yanakufa tukiyaona hivi hivi!
Mfano shirika kama ATC kulikuwa na na aja ya kuunza njia au kuingia ubia na Alliance air??

KakaKiiza ninaikumbuka Bank ya Nyumba Tanzania.. ninaikumbuka Matsushita.. Phillips.. Kiuta.. Metal box.. kiwanda cha kutengeneza mabox cha kibo..
Mimi nilienda national service nikawa na jamaa mmoja alikuwa meneja pale sokoine drive alikuwa akiniadithia mipango ya THB nikajua nitakuwa na nyumba karibuni!!Aliitwa BRUCE NYAMWANGI.R.I.PBRUCE!Nilivyo ingia uraiani nakuta hata benki hakuna watu wana haha kutafuta kazi eti shirika limeuzwa!

CCM inaniuma sana hadi leo!
Hii ikifa nachinja Ng'ombe 2 japo sijawahi kuchinja!

sasa hivi wamekuja na hii kitu inaitwa Export processing zone(epz). cha ajabu ni kuwa wamegeuza kuwa magodown wakikodishia wachina na wahindi na sasa inegeuka ni Import na sio export.
Wewe unaanzisha kitu ndani ya CCM UNAONDOKA UNADHANI KUNA MTU WAKUSIMAMIA HUKO NYUMA??
 
Hakuna shirika ambalo hadi kesho nalililia kama General Tyre! Najiuliza, inakuwaje shirika life wakati uingzaji wa magari nchini ni mkubwa zaidi (reflecting big market) kuliko kipindi chochote kile katika historia ya nchi hii....!!

Hata mi nashangaa,ni kama TTCL,tz tunaongoza kumiliki vilongaX2 within east africa,how on earth kampuni ya simu inakwama??
 
Hata mi nashangaa,ni kama TTCL,tz tunaongoza kumiliki vilongaX2 within east africa,how on earth kampuni ya simu inakwama??
Hili la TTCL ni mtihani mkubwa ambao solution yake ni kufanya marekebisho na kuiacha iwe inaamua mambo yake yenyewe!! Hofu yangu hapa ni kwamba, Competitors wa TTCL(Kampuni za simu za mikononi) ni aggressive business entities....wapo faster kufanya maamuzi! So, kwa TTCL, ambayo si ajabu baadhi ya mambo ya msingi kabisa kibiashara unaweza kuta hadi wapate baraka za serikali au bunge; they'll always lag behind!
 
Hakuna linalo niuma kama nbc kuwawa tanzania kabla ya muda wake na na kufufukia south africa !
 
Zana Za Kilimo (ZZK) - mbeya,
Hi-Soap - Mbeya
Mbeya Ceramics

Wana bodi najua wengi wenu mnakumbuka baadhi ya mashirika yalifilisiwa na mengine kubinafisishwa kwa bei ya chee!mfano NBC namengineyo mengi!ila mimi nakumbuka mashirka kama NASACO,TANGANYIKA PAKERS,TACOSHIL;MANG'ULA,FAIBERBOARD,GENERAL TYRE,na mengineyo!mimi lina niuma GENERAL TYRE je wewe?
 
tena iliuzwa kitu cha milioni 19 tena kwa mkopo eti,
benki na maeneo yake yote???????
Hakuna linalo niuma kama nbc kuwawa tanzania kabla ya muda wake na na kufufukia south africa !
 
haujambo anti yangu?

sasa hivi wamekuja na hii kitu inaitwa Export processing zone(epz). cha ajabu ni kuwa wamegeuza kuwa magodown wakikodishia wachina na wahindi na sasa inegeuka ni Import na sio export.
 
Msisahau TAWICO, lile lililokuwa linatuuzia nyama za porini zilizokaushwa. KAMATA, RAILWAY BUS, Makampuni ya usafirishaji ya mikoa kama kama KAUDO, KAGERA-RETCO, KAUMA, na yale ya vyama ushirika kama KNCU ya kilimanjaro, ARCU y Arusha, CRCU dodoma. Dah...!! Roho inaniuma nikikumbuka nafasi hizi za kazi zilizotoweshwa wa Watanzania wenzetu wenye roho za ubinafsi. Naomba tu eeeeeehhhh Mola wetu uwachukue watu hawa wanaosababisha tunateseka leo hii kwa kukosa kazi. Aaaameeen.
 
kazi ya ben hiyo,
na ndo kitu alikuwa hapendi mwalimu kusikia benki yake inauzwa.

Kwa bei hiyo bora hata tungeacha life polepole mikononi mwetu, kuliko uchizi uliofanyika!
 
Wana bodi najua wengi wenu mnakumbuka baadhi ya mashirika yalifilisiwa na mengine kubinafisishwa kwa bei ya chee!mfano NBC namengineyo mengi!ila mimi nakumbuka mashirka kama NASACO,TANGANYIKA PAKERS,TACOSHIL;MANG'ULA,FAIBERBOARD,GENERAL TYRE,na mengineyo!mimi lina niuma GENERAL TYRE je wewe?
hayo mimi ndo yananiuma sana kwakweli!
 
kazi ya ben hiyo,
na ndo kitu alikuwa hapendi mwalimu kusikia benki yake inauzwa.

Ndio iliopelekea kifo cha haraka cha mwalim nini? maana ni balaa, Ben nadhani alisomea uchuuzi maana aliuza kweli enzi zake.lol!
 
kwa kuwa sie wote ni watu wazima lazima tujue baada ya hapo na kifo cha mwalimu vina ukaribu gani,
but all in all R.I.P. Mwalimu Nyerere, ninakukumbuka sana.

Ndio iliopelekea kifo cha haraka cha mwalim nini? maana ni balaa, Ben nadhani alisomea uchuuzi maana aliuza kweli enzi zake.lol!
 
TWICO.. Tanzania Wood Industries Corporation ilikuwa na viwanda vya mbao kilwa,mbeya,mafinga,kilimanjaro na lushoto kama sikosei. wakati huo mbao ilikuwa inatema hela si mchezoo..
 
mimi nalia machozi hapa acha wewe unayepata hasira,
angalia hii nchi kitu ilichotufanyia,
tena bila woga na huruma tunazidi kuwapa uongozi tu.

we ndo unazidi kuniongezea hasila na hayo makampuni nakumbuka nilipokuwa darasa la 5 Mbeya tulitembelea huko
 
Wana bodi najua wengi wenu mnakumbuka baadhi ya mashirika yalifilisiwa na mengine kubinafisishwa kwa bei ya chee!mfano NBC namengineyo mengi!ila mimi nakumbuka mashirka kama NASACO,TANGANYIKA PAKERS,TACOSHIL;MANG'ULA,FAIBERBOARD,GENERAL TYRE,na mengineyo!mimi lina niuma GENERAL TYRE je wewe?

pia kama unamfahamu aliyehusika/changia kuua shirika lolote atajwe tu hapa hapa kwani nini!
 
Back
Top Bottom