Shinyanga: Wafanyabiashara 6 wakamatwa kwa kuuza Sukari kinyume na Bei elekezi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, linawashikilia wafanyabiashara sita wa sukari kwa tuhuma za kuuza sukari kinyume na bei elekezi ya serikali.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme, katika kikao alichofanya na wafanyabiashara wa sukari mkoani humo kilichokuwa na lengo la kujua changamoto zinazowakumba wafanyabiashara hao na kuwasababisha kushindwa kuuza bei elekezi ya serikali.

Mndeme amesema mkoani humo kuna tatizo la bei ya sukari kutokuwa rafiki wa walaji, hivyo ameona akutane na wafanyabiashara hao ili kuzungumza nao kujua tatizo nini hadi kushindwa kuuza sukari kwa bei elekezi ya serikali.

Amesema serikali imetoa maelekezo na kila Kanda imetolewa bei elekezi ambapo Kanda ya Ziwa ukiwamo Mkoa wa Shinyanga, kwamba bei ya jumla ni Sh. 2,600 hadi 2,800, rejareja Sh. 2,800 hadi 3,000 na kwamba mlaji wa sukari kwa mkoa huo wa Shinyanga anauziwa sukari kilo moja Sh. 3,200 hadi 5,000.

“Kunanini kwa wafanyabiashara mnashindwa kuuza sukari kwa bei elekezi ya serikali, mnaficha sukari na kwanini mpaka tunafikia hatua ya kukamatana, na mpaka sasa tumewakamata wafanyabiashara sita kutoka Kahama, watatu wakubwa, watatu wadogo kwa kwenda kinyume na maelekezo ya serikali ya kuuza sukari kwa bei elekezi,” amesema Mndeme.

NIPASHE
 
Serikali si ingekuwa na maduka yake iuze kwa bei elelekezi?
 
Back
Top Bottom