Serikali itangaze bei ya sukari elekezi kwa wananchi tofauti na hapo mitaa inaumia kwa manufaa ya Wafanyabiashara

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,201
12,717
Nimeona habari moja inayosema kuwa Kuna wafanyabiashara 84 wamekamatwa kwa kuuza sukari 4000, 4800 wakati Bei ya jumla wamenunua 2500.

Waziri Bashe kupitia jukwaa hili la jamiiforum NALIA NGWENA nakupasha habari kuwa hao wafanya biashara 84 ni wachache mno wananchi wanaumia kwa na Hawa wafanyabiashara na Bei ya elfu 5000 imezoeleka.

Njoo Dodoma maduka mengi sukari ni elfu 5000 na ni kawaida kabisa kwa kua wananchi hawana habari kuwa Kama wafanyabiashara wanauziwa sukari kwa Bei elekezi.

Maoni Yangu: serikali kupitia vyombo vya habari waimbe kuhusu Bei elekezi ya serikali na mfanyabiashara akibainika kuwa anauza sukari juu ya kiwango pangwa basi wananchi/wahusika waambiwe wakaripoti wapi.
 
Back
Top Bottom