Kwa hilo nakupinga huyo atasoma na mwanao ili washauriane vzr sio mtoto wangu kila kitu mnataka kulaumu na kupinga mzee sio kila kitu alikua anakosea
Yes,mtoto wako akipata mimba atajichokonoa ili aweze kuendelea na masomo kwa sababu hamna namna.
 
Mwanafunzi anayesoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Uzogole Manispaa ya Shinyanga (jina limehifadhiwa), amedaiwa kujitoa ujauzito kwa kijichokonoa na kijiti, ili aendelee na masomo.

Imeelezwa mwanafunzi huyo alipata ujauzito huo wakati akiwa nyumbani akisubiri matokeo ya kidato cha kwanza, na alipofaulu akaingia nao sekondari, ndipo Januari mwaka huu akaona autoe ili asifukuzwe shule.

Askari Polisi Kata wa Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga ilipo shule hiyo, Emmanuel Maganjila, ilibainisha hayo juzi kwenye kikao cha kujadiliana kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye kata hiyo, kilichoandaliwa na Shirika la YWCA.

Alisema mwanafunzi huyo alifanikiwa kujitoa ujauzito huo, na kwamba kilitoka kiumbe kikiwa kimekufa, lakini mwanafunzi huyo aliwahishwa hospitali kwa ajili ya matibabu, na sasa anaendelea na masomo.

"Natoa wito kwa wazazi mkoani Shinyanga vunjeni ukimya, zungumzeni na watoto wenu na kuwapatia elimu ya makuzi na madhara ya kufanya ngono katika umri mdogo," alisema Maganjila.

Naye Katibu wa Shirika la YWCA, Marysiana Makundi, ambao wanatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye Kata ya Ibadakuli, alisema matatizo hayo ya mimba za utotoni ili kuisha, inapaswa wahusika wawe wanafungwa jela badala ya kuachiwa huru.

Alisema mbali na utoaji wa elimu ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia, wazazi wamekuwa kikwazo, kutokana na kuwa na tabia ya kumaliza kesi kimya kimya na watuhumiwa ambao huwapatia ujauzito wanafunzi, kwa kupeana fedha ama mifugo na kusababisha kesi kufutwa mahakamani kutokana na kukosekana ushahidi.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Ibadakuli, Mwijage Patrick, aliwataka wazazi mkoani Shinyanga, waachane na mila kandamizi, ambazo zimekuwa zikimnyima haki mtoto wa kike, kwa kuonekana hastahili masomo bali ni wa kuolewa tu, na ndio chanzo cha mimba na ndoa za utotoni kuendelea kwa kasi mkoani humo.

Chanzo: IPP MEDIA
Naomba tu kuuliza, hivi YWCA ni Shirika, Taasisi ama Jumuiya?
 
Wanasema kijiti cha mhogo ni sumu balaa ukiwa na mimba...watu wa kanda ya ziwa wanatumia mno..kuna ndg yangu alijigundua ana mimba 50 yrs tukamzika !....! Sijui kina nini...!
Yaan alipata mimba na 50yrs akaitoa na kijiti cha mhogo?

Pia kuna mama mmoja kijijini kwetu 2018 ile nimeenda likizo alikuwa na 46 yrs ana watoto 10, alipata mimba akajichokonoa na huo mti wa mhogo akaoza huko ndani tukazika!

Inaonesha ilikuwa michezo yake sasa siku hiyo ikawa bahati mbaya
 
We ushasoma tafiti juu ya kuwazuia watoto wasirudi shule pale wanapopata mimba?Unaelewa kuwa watoto hawa huwa wanakufa kwa sababu ya kutoa mimba ili warudi shule?
Unachosema waruhusiwe kuendelea na shule kwa sababu watakufa wakati wanatoa mimba!? Kwa fikra hizi za kubembeleza, basi na wanaofeli wapitishwe tu maana huwa wanajiua kwa sababu ya matokeo mabaya.
 
Mwanafunzi anayesoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Uzogole Manispaa ya Shinyanga (jina limehifadhiwa), amedaiwa kujitoa ujauzito kwa kijichokonoa na kijiti, ili aendelee na masomo.

Imeelezwa mwanafunzi huyo alipata ujauzito huo wakati akiwa nyumbani akisubiri matokeo ya kidato cha kwanza, na alipofaulu akaingia nao sekondari, ndipo Januari mwaka huu akaona autoe ili asifukuzwe shule.

Askari Polisi Kata wa Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga ilipo shule hiyo, Emmanuel Maganjila, ilibainisha hayo juzi kwenye kikao cha kujadiliana kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye kata hiyo, kilichoandaliwa na Shirika la YWCA.

Alisema mwanafunzi huyo alifanikiwa kujitoa ujauzito huo, na kwamba kilitoka kiumbe kikiwa kimekufa, lakini mwanafunzi huyo aliwahishwa hospitali kwa ajili ya matibabu, na sasa anaendelea na masomo.

"Natoa wito kwa wazazi mkoani Shinyanga vunjeni ukimya, zungumzeni na watoto wenu na kuwapatia elimu ya makuzi na madhara ya kufanya ngono katika umri mdogo," alisema Maganjila.

Naye Katibu wa Shirika la YWCA, Marysiana Makundi, ambao wanatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye Kata ya Ibadakuli, alisema matatizo hayo ya mimba za utotoni ili kuisha, inapaswa wahusika wawe wanafungwa jela badala ya kuachiwa huru.

Alisema mbali na utoaji wa elimu ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia, wazazi wamekuwa kikwazo, kutokana na kuwa na tabia ya kumaliza kesi kimya kimya na watuhumiwa ambao huwapatia ujauzito wanafunzi, kwa kupeana fedha ama mifugo na kusababisha kesi kufutwa mahakamani kutokana na kukosekana ushahidi.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Ibadakuli, Mwijage Patrick, aliwataka wazazi mkoani Shinyanga, waachane na mila kandamizi, ambazo zimekuwa zikimnyima haki mtoto wa kike, kwa kuonekana hastahili masomo bali ni wa kuolewa tu, na ndio chanzo cha mimba na ndoa za utotoni kuendelea kwa kasi mkoani humo.

Chanzo: IPP MEDIA
Wasukuma bwana.
Daaah. Kuna kipindi walipewa nchi wanatuongoza kabisa yaani
 
Kwa hiyo sasa hapo kawini? Si kesi ya mauaji hiyo na kutoa mimba au sheria inasemaje?
 
Yaan alipata mimba na 50yrs akaitoa na kijiti cha mhogo?

Pia kuna mama mmoja kijijini kwetu 2018 ile nimeenda likizo alikuwa na 46 yrs ana watoto 10, alipata mimba akajichokonoa na huo mti wa mhogo akaoza huko ndani tukazika!

Inaonesha ilikuwa michezo yake sasa siku hiyo ikawa bahati mbaya
Same na huyo wa kwetu...!alifariki.kwaajili.hizo.alibleed balaa na mimba ilikua 7mths..
 
Back
Top Bottom