Adhabu ya kufungwa Jela miaka 30 kijana aliempa mwanafunzi mimba ni hasara kuliko tukio lenyewe

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Najua inaumiza sana Mzazi kupokea Taarifa za Binti yake kupata ujauzito ile hali angali mwanafunzi,
Lakini siku zote panapo maamzi ya hasira lazima kuna galama zake pia.

Sheria zipo kwa ajili ya kulinda na kutetea haki lakini pia sio kosa kutumia busara na hekima kabla hatujafikia hatua ya sheria.

Yapo mazingira ambayo Wazazi tunapaswa kuyazingatia hasa tunapopokea taarifa za watoto wetu kupata ujauzito kabla hatujafuata sheria.

Kwanza Mzazi kama mzazi inafaa kujiuliza mimba ilipatikana kwa mazingira yapi? Binti kabakwa, yaani kaingiliwa bila ridhaa au aliridhia mwenyewe na walikubaliana?

Naongea hivi kwa sababu zifuatazo, Kuna baadhi ya watoto wetu wakike Wameshindikana na mara nyingi tabia zao tunazijua hata sisi wenyewe wazazi na hata mda mwingine tunawaonya lakini hawabadiliki, Mtoto wa hivyo akipewa mimba tumuache aolewe na sio kupelekana jela, cha msingi ni kumskiliza kijana kama yuko tayari kuwajibika kama baba acha waishi mda mwingine Dunia nayo hufunza, Lakini pia sio kila lijalo kwa ubaya huishia pabaya kuna mambo mengine yanaweza kuja kwa taswira ya Ubaya na aibu mwishoni ikawa neema.

Kuna familia binti anapata ujauzito wanapanic wanamfungulia kijana mashtaka anaenda jela miaka 30, kisha Binti anarudishwa shule bado anapuyanga anapata Ziro. Akirudi nyumbani napo anakuta hamna msaada hatmae Binti anaondoka nyumban kwenda kujitaftia maisha na kuacha mtoto nyumban ambae hana Baba.

Anahangaika huko kutafta kazi anaishia kuwa BARMAID, anapalangana huko anadumbukia kwenye Udangaji na mwisho anajikuta anakwaa HIV POSITIVE, anakufa.

Huku nyuma mtoto anakosa malezi ya Baba ambae anatumikia kifungo cha miaka 30 jela, anakosa huduma za msingi, Mwisho wa siku anaishia kuwa Mvuta bange na Panya road anachomwa moto, Historia finish.

Baba mtu chukulia picha alitekereza tukio akiwa na miaka 33 akifungwa mingine 30 anakuja kutoka Jela na miaka 63, tayari keshapoteza matumaini hana nguvu ya kuzalisha chochote, akirudi anakuja kuwa tegemezi na masikini akiangalia wenzake aliowaacha uraian walishamtangulia anapata depression tunampoteza. Total Finish.

Matokeo ya hayo yote ni HASIRA NA SHERIA. Siku zote waliotunga sheria hawakuwazia Matokeo baada ya sheria, Anaepaswa kufikiria ni wewe kabla hujaifikia sheria.

Lakini kumbe pengine ingetumka busara ukatambua kuwa mwanao kachagua maisha ya Ndoa badala ya shule ungebariki tu, Wakaishi mwenyezimungu huwa anamipango kwa kila mtu pengine wangepambana wakaishi kwa amani na kulea mtoto wao kwa upendo na hata kesho akawa mtu mhimu katika jamii, lakini hasira za mda mfupi na sheria zimeharibu maisha ya watu watatu wote kwa pamoja, HASIRA HASARA.

Naomba nisieleweke vibaya sitetei mimba za utotoni lakini katika maamzi ya hasira siku zote matokeo yake hubomoa.

Tujifunze kutumia busara kwanza kabla hatujatumia sheria.
 
ili iwe fundisho kwa wengine. Ukifanya hata wewe tutakukamata na nimiak 30 jela. Acha wanafunzi wasome
 
Nadhani wacha sheria isimame tu kama ilivyo. Unaanzaje kudeal na mtoto under age (mwanafunzi)? Mwanaume awe mkubwa kiumri 18+ au chini ya hapo let's say 15-17 bado lazima mtoto wa kike especially mwanafunzi alindwe.

Kuweka loop hole ya maelewano nadhani hali itakuwa mbaya zaidi.

Kuna kisa ntakuleta hapa jamaa alikuwa napenda sana dogo dogo hasa wanafunzi siku yakamkuta. Kibinti kilikuwa kimeshakata kamba kitambo kikashonewa uniform na daftari za kuzuga. Jamaa kaenda jela.
 
Lazima mazingira ya mimba yaangaliwe maana kuna watoto wa shule wanakunya hadi pombe na bange mnaweza kutana nae mtaani anakula bange na usjue hata kama anasoma ko lazima mazingira yaangaliwe, pia mimi silaumu sheria ila narudia familia ya binti ambayo inashiriki pia kuteketeza future ya mtoto wao kwa kuamini wamekomoa mtu
 
Bado haki ya mtoto kusoma iko palepale. Zingine kelele
 
Kuna kabint hapa mtaani kana mtoto miaka 5 kanakaa uswahilini chumba cha Giza, kanahangaika na vibarua hakana A wala B, mvua ikinyesha ni yake, Jua lake mtoto akiumwa majirani ndio tunamchangia matibabu na mda mwingine hata chakula yule mtoto anapewa na majirani, Mtoto miaka 5 hata chekechea bado hajaanza, Mama mtu Bodaboda wanajilia tu,

Niliwahi kusikia baba mtoto alifungwa jela miaka 30 kisa mimba, sasa hapo alieharibikiwa ni nani?? Si bora angeachwa pengine wangesaidiana kulea yule mtoto hata sasa angepata haki ya kusoma na huduma zingine ambazo mama yake hawezi??

Unakuta katoto mvua zinanyesha kanaswampa tu kwenye baridi bila nguo na mama mtu yuko huko na mabodaboda anatafta ugali, yule mtoto atakuja kuwa mtu wa aina gani? Je familia ya Binti wanafurahia yale maisha ya mjukuu wao?? Si bora wangeacha pengine mtoto angepata haki ya kulelewa na bba yake
 
mimi naomba serikali iongeze miaka 20 kwenye hiyo 30.
Ila atakayebainika anaanza kumrubuni mwenzake awekwe ndani miaka 50 kama ni demu kaanza kumtongoza mwanaume akae miaka 50 jela baada ya kujifungua na kama ni mwanaume akae miaka 50 jela.
Huwezi ukawa umetumwa kusoma hata kujitawaza huwezi unaenda kutongoza watoto wakike. Wafungwe tu waongeze hiyo miaka
 
Hakuna anaekataa adhabu tatzo ni matokeo baada ya adhabu, kipi kinafuatia kwa maisha ya hawa watatu kwa maana ya baba mama na mtoto, wanaishije baada ya hukumu

Nakama adhabu zitaongezewa basi kuwepo na namna ya kuwasaidia mam na mtoto ambao wanabaki uraiani, au hata mtoto tu aliezaliwa iwepo namna ya kuhakikisha anapata huduma za kijamii na elimu
 
Adhabu hiyo ni nzuri sana, mimi napendekeza wafungwe wote, binti aliyepewa mimba na kijana aliyempa mimba. Kumfunga kijana wa kiume pekee ni unyanyasaji na kutotenda haki!
 
Maisha yako unbidi kuyapa thamani na kuyalinda kwa kutumia AKILI

Ngono ni jambo la kawaida Sana Ila watu mnalikuza na kuamini usipofanya NGO no utakufa.

Kama kijana kufanya ngono na mwanamke ambaye huna bond nae ya kubwa nikuyaweka maisha yako katika hatari.

Miaka 30, ni adhabu ndogo pia ni adhabu kubwa

Hapa duniani Ukiipa ngono nguvu fahamu tu utashindwa kuwa yule ambaye uliumbwa ili uwe.

Ngono hata mwanamke asipopata mimba bado Ina play sehemu kubwa ya yeye kuwa MTU Wa hovyo.

Mwisho Serikali iendelee kuwapa Elimu vijana wa kike na kiume.
 
Nadhani wacha sheria isimame tu kama ilivyo. Unaanzaje kudeal na mtoto under age (mwanafunzi)? Mwanaume awe mkubwa kiumri 18+ au chini ya hapo let's say 15-17 bado lazima mtoto wa kike especially mwanafunzi alindwe.
Kuweka loop hole ya maelewano nadhani hali itakuwa mbaya zaidi.
Kuna kisa ntakuleta hapa jamaa alikuwa napenda sana dogo dogo hasa wanafunzi siku yakamkuta. Kibinti kilikuwa kimeshakata kamba kitambo kikashonewa uniform na daftari za kuzuga. Jamaa kaenda jela.
Nawapa pole binti zako kwa kuwa na baba mwenye akili ndogo kama ww anaye tegemea sheria kumlindia binti yako ,kwanza aliye kwambia kuwa sheria ndo intamlinda binti yako ni nani?
Mbona pamoja na sheria hiyo lakini bado maelfu kwa maelfu ya mabinti wa shule wanapewa mimba kila mwaka hapa nchini?
Yeye kama binti ndo mwenye jukumu la kujilinda na mwenye jukumu la kumfundisha binti namna ya kujilinda lipo kwako ww mzazi wake uliye mzaa.
Sasa nyinyi wazazi wa siku hizi mmeendekeza malezi ya hovyo na uzungu mwingi kwa watoto wenu alafu mnategemea eti walindwe na sheria?
 
Back
Top Bottom