JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma October 18, 2023 imemhukumu kifungo cha Miaka 60 Jela, Faraji Milanzi Yasini, (20), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Ruanda - Mkowela Wilayani Tunduru baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa Darasa la Saba.
Akisoma hukumu hiyo kesi namba 62 ya mwaka 2023 Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mhe. Kando alisema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.
Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 10, 2022 huko Kijiji cha Ruanda - Mkowela na kufikishwa mahakamani October 10, 2023 ambapo alipatikana na hatia la makosa hayo.
Mtuhumiwa huyo alitiwa hatiani kwa makosa mawili ya Kubaka chini ya K/F 130 (1)(2) (e) na 131(1) Sheria ya kanuni ya adhabu Sira ya 16 R.E 2022 na kosa la Kumpa mimba mwanafunzi chini ya K/F 60A (1)(3) cha sheria ya Elimu Sura ya 363 iliyofanyiwa marekebisho madogo no. 2 mwaka 2016 na baada ya kutiwa hatia mtuhumiwa alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kila kosa.