Ni wazi kwamba mwandishi wa hekaya hii ni mtu asiyejua chochote katika nchi hii, wala katiba ya chama, wala mfumo na uundo wa CHADEMA. Hivi kama ni kweli akisemacho huyu mwandishi wa hekaya hizi, tujiulize wafuatao kama ni wakwe wa Mtei
1. Meshak Opulukwa Mbunge wa Meatu
2. David Silinde Mbunge wa Mbozi
3. Vincent Nyerere Mbunge wa Musoma Mjini
4. Suzan Kiwanga Mbunge vITI Maalum Morogoro
Hii ni mifano tu, ya kupanuka kwa Chama hiki kinachoingia ikulu October, Kwa takwimu za Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014, Mkoa ulioongoza kwa Ushindi wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa ni Kagera, hasa Jimbo la mama Escrow, Mikoa ya Shinyanga, Simiyu Mbeya na Rukwa imefanya vizuri kuliko Kilimanjaro na Arusha, kuendelea kuandika hekaya za kumtuhumu Mzee Mtei na Kaka Freeman Mbowe ni uvivu wa kufikiri, kuendelea kuwaza yaleyale ambayo yamekuwa yakisemwa na walioshindwa kuongoza nchi hii.
Ikumbukwe Zitto Kabwe wakati anakuwa Mbunge Kigoma Kaskazini, CHADEMA ilikuwa na Madiwani 8, leo anaondoka akiwa na Diwani MMOJA TU.
Nimeanza nitakuja kuendelea.