CHADEMA kuwashitaki wanaombagaza Heche

CHADEMA kuwashitaki wanaombagaza Heche

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,843
Reaction score
3,072
JOHN-HECHE.jpg

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza nia ya kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaojitambulisha kuwa viongozi wa chama hicho bila uhalali, kikidai wamekuwa wakikibagaza chama hicho na kumkashifu Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche.

Hali hiyo ilianza kujitokeza kufuatia kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichofanyika mkoani Kigoma, zikidai Heche alitumia vibaya michango ya kampeni ya 'Tone Tone' kwa kujinufaisha binafsi badala ya chama.

Soma pia: Pascal Anthony: Heche ameleta Mpasuko ndani ya chama, tunajiandaa kufanya maandamano

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, aliwahi kukanusha tuhuma hizo hadharani, akisema fedha za kampeni hiyo ziko salama.

Licha ya ufafanuzi huo, baadhi ya watu waliodai kuwa viongozi wa Chadema waliendelea kutoa matamko wakimtaka Heche ajiondoe madarakani ili kupisha uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 2, 2026, katika makao makuu ya Chadema yaliyopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi wa chama hicho, Wakili Dickson Matata, amesema watu hao si viongozi halali wa Chadema na wamekuwa wakilitumia jina la chama kwa masilahi yao ya kisiasa.

Amesema vitendo vya kufanya mikutano ya waandishi wa habari na kutoa taarifa zinazokichafua chama pamoja na viongozi wake vinapaswa kukomeshwa kwa kuwachukulia wahusika hatua za kisheria.

Amedai matukio ya watu kujitambulisha kwa uongo kama viongozi wa Chadema yamekuwa yakijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Kanda ya Pwani na Nyasa, ambapo baadaye viongozi halali wa chama hulazimika kujitokeza na kukanusha madai hayo.

Kupitia mkutano huo, Matata pia amemshauri Heche kufungua kesi ya madai dhidi ya watu hao ili wadaiwe fidia kwa kile alichodai ni kumchafulia jina kwa tuhuma ambazo hazijathibitishwa na zisizo na msingi.

Chanzo: Mwananchi
 
Waache watu watoe maoni yao. Kwanini waingilie uhuru wa watu kutoa maoni? Hiyo sio demokrasia wanayopigania.
 
View attachment 3642294

Chama cha udikteta uchwara na umaskini. Kumbe mkuki kwa nguruwe kwao unaumiza? Kila siku ni kumtukana, kumdhalilisha, kumzushia Rais wetu. Huko hawatashinda lolote hao nyumbu
 
Msiishie kutishia tu. Nendeni mahakamani!
 
Waache watu watoe maoni yao. Kwanini waingilie uhuru wa watu kutoa maoni? Hiyo sio demokrasia wanayopigania.
Huko ccm mnafanya hivi walivyofanya hao csm uchwara au umehemkwa tu? Kwanini wasifuate utaratibu wa kupeleka hoja zao kwenye vikao halali na kuacha kuvunja katiba waliyoiandika wenyewe? Tunakusubiri mahakamani na jiandae kuuza mali za ukoo maana utadaiwa fidia kubwa ili mfilisike!
Cdm kazeni buti maana wameshaanza kutoa ushuzi huku!
 
Heche anasema samuya aache uenyekiti apishe uchunguzi, yeye Heche akiambiwa apishe uchunguzi mnapinga.
 
Huko ccm mnafanya hivi walivyofanya hao csm uchwara au umehemkwa tu? Kwanini wasifuate utaratibu wa kupeleka hoja zao kwenye vikao halali na kuacha kuvunja katiba waliyoiandika wenyewe? Tunakusubiri mahakamani na jiandae kuuza mali za ukoo maana utadaiwa fidia kubwa ili mfilisike!
Cdm kazeni buti maana wameshaanza kutoa ushuzi huku!
May be in your next life.
 
Back
Top Bottom