josam
JF-Expert Member
- Nov 22, 2011
- 2,252
- 1,046
Ni wazi kwamba mwandishi wa hekaya hii ni mtu asiyejua chochote katika nchi hii, wala katiba ya chama, wala mfumo na uundo wa CHADEMA. Hivi kama ni kweli akisemacho huyu mwandishi wa hekaya hizi, tujiulize wafuatao kama ni wakwe wa Mtei
1. Meshak Opulukwa Mbunge wa Meatu
2. David Silinde Mbunge wa Mbozi
3. Vincent Nyerere Mbunge wa Musoma Mjini
4. Suzan Kiwanga Mbunge vITI Maalum Morogoro
Hii ni mifano tu, ya kupanuka kwa Chama hiki kinachoingia ikulu October, Kwa takwimu za Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014, Mkoa ulioongoza kwa Ushindi wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa ni Kagera, hasa Jimbo la mama Escrow, Mikoa ya Shinyanga, Simiyu Mbeya na Rukwa imefanya vizuri kuliko Kilimanjaro na Arusha, kuendelea kuandika hekaya za kumtuhumu Mzee Mtei na Kaka Freeman Mbowe ni uvivu wa kufikiri, kuendelea kuwaza yaleyale ambayo yamekuwa yakisemwa na walioshindwa kuongoza nchi hii.
Ikumbukwe Zitto Kabwe wakati anakuwa Mbunge Kigoma Kaskazini, CHADEMA ilikuwa na Madiwani 8, leo anaondoka akiwa na Diwani MMOJA TU.
Nimeanza nitakuja kuendelea.
Unajua ndg yangu wengine kupata walau kofia, kiroba basi shida hadi kulazimika kutoa mawazo ambayo hata anaye fikiri kwa masaburi hawezi kufanya hivyo! Hivi kama mambo yanafanyika wazi wazi namna hii, leo mtu anatoa wapi ujasili wa kunena wapendayo wafalume kuyasikia!?
Kuna nyimbo nyingi kwamba CHADEMA ni cha kasikazini! Binafsi nimefarijika na takwimu zako hapo juu kama ni sahihi. Nadhani ndiyo maana CHADEMA hawapotezi muda kukanusha habari potofu kamahizi lakini inapo bidi wawe wanatuwekea evidences kama hizi ili kuweka record/ kumbu kumbu vizuri.
Isitoshe kuna mdau mwingine kaandika kuwa kila jambo lazima lina mwanzilishi wake. Hiyo CCM yenyewe ilitokana na nguvu ya pamoja ya watanganyika wote kupitia TANU na wazanzibari wa ASP miaka hiyo. Kama ilivyo kwa CHADEMA navyo vina wanzilishi wake. Leo hii ukabila ndani ya ukoo wa TANU na ASP na mjukuu wao CCM hauongelewi kwa sababu kubwa mbili.
1. Watanganyika wote waliungana kumuondoa mkoloni. 2. Ukoo huo ulifanikisha kuondoa mkoloni huyo na kuwa kiongozi ambapo uongozi na mali zote za Tanu ali rithi mwamanao CCM.
Nina imani hata CHADEMA AMA UKAWA ikishinda na kukalia kiti kile cha uzima uzushi wa UKABILA, UDINI na mizengwe iliyopo leo, havitakuwa kipaumbele vya wapinzani wao CCM. Kwa nn nasema hivi? Watanganyika ni wepesi kusahau mambo na hupenda kujipendekeza kwa mwenye nyumba. Najua kutakuwepo upinzani mkali sana kwani ALIYE ZOEA KULA BILA KIPIMO atapiga kelele kuliko maelezo kwa sababu anaona anadhulumiwa, anawaza hashibi bila kujua mabadiliko katika fikra ni swala la muda na kujiandaa kisaikolojia!
Siku njema!