Shibuda out


Hahahaaa..Mkuu umesahau Sofia Simba alitukanana na kutaka kupigana na Mama Kahama kwenye kinyang'anyiro cha Uenyekiti UWT?
na unataka kusema uamuzi uliomhalalisha Masauni agombee Uenyekiti UVCCM haukuwa na misingi ya zengwe?
Au unadhani Nape alienguliwa kihalali?
Fanya analysis vizuri wewe
 

Kama Baraza Kuu la Chadema Mkoa litakubaliana na maamuzi haya nitawaona hawanazo, hii sio demokrasia kwa viwango vyovyote na maamuzi kama haya hayapaswi kuendelea kuvumiliwa, kamati kuu ya Chadema iliyojaa wateuliwa wa Mwenyekiti ina nguvu kupita kiasi na inatumika kama chombo cha kuwashughulikia wote wanaopingana na status guo ndani ya chama.

Ilianza kwa Chacha Wangwe, ikaja kwa walioshinda Uchaguzi wa Vijana, ikaendelea kwenye uchaguzi wa kuchagua Wabunge wa Viti Maalumu, Sasa Shibuda na kama hatua stahili hazitachukuliwa list itaendelea to infinity, tunaulea ugonjwa mbaya sana na ambao ni hatari kwa taifa kama Chadema itaingia madarakani kama ilivyo sasa!!

Can you imagine ingekuwa vipi kama former Spika Sitta na Mwakyembe wangekuwa Chadema hii na kutofautiana na chama kama walivyofanya kwenye issue ya Richmond ndani ya CCM?wangeshughulikiwa zamani...!! Nasharia kuwa Chadema inaendeshwa kidikteta kuliko ata chama kikongwe cha CCM, tutauonaje mbadala katika mazingira haya?

Ni Heri CCM walishinda kwenye uchaguzi wa 2010 kwa sababu nasharia ingekuwa ni disaster kwa nchi.
 

Ndivyo hivyo,
Kwanza ilianza kula kwa CHACHA baada ya kutaka kuuwania uenyekiti, wakasitisha kwa mda zoezi la uchaguzi walipolileta baada ya CHACHA kuwa kishatoweka wakafanya uchaguzi wakiamini hatatokea mpinzani mara gafra bin vuu Zitto, tangu hapo inakula kwa Zitto. Jaribu kuidanganya akili tu kwamba walianza kabla. Ofcoz ukisema walianza kabla kwenye kipindi cha kampeni hiyo ya kuchukua fomu na kujitoa nitakuelewa.

Mukama na Mkama ni majina mawili tofauti na hata kama kwani una unataka kujenga hoja gani?
 

Kwahiyo na ninyi mnafanya kama ccm sio?
 
hiyo ni kwako wewe sio kwa kila mtu.
 

Ah! Huyo jamaa waovyo sana, wala hajuwi anachofanya ilimradi yeye aseme tu.
 
Vandugu zangu, yatokeayo hapana budi yawe ili kuibua kasoro ndogo ndogo zilizofichika ziweze kufanyiwa kazi. Chadema kinahitaji kukua si kwa kuongeza wanachama tu ila kimuundo systematically ili mfumo wake uweze kuleta ufanisi katika jitihada za kujijenga kuchukua dola. Viongozi ni binadamu ambao wangali na silika na madhaifu, yatokeayo ni kama mirrow itakayowasaidia walipo matongotongo wayaonayo waweze kujisafisha.

Zitto ana kasoro zake, lakini kamati ya maadili ilishawahi kumwita na kumsikia au kumwonya kutokana na yale wanayoona anafanya yasiyofaa kwa chama? Kwa vile hakuna utaratibu kama huo ndio maana Zitto anaendelea na hamsini zake na wale wanaochoshwa na tabia hiyo wanaamua kumtolea uvivu vikaoni na hii inawafumbua macho viongozi.

Misuguano kama hiyo ni yakawaida ila ustaarabu utangulizwe ili kunusuru amani na utulivu ndani ya chama. Mwenye kujali maamuzi ya vikao ni mtume na anania njema ya kujenga chama, na mwenye kupendelea maamuzi ya papo kwa papo bila vikao ni kasoro inayohitaji kufanyiwa kazi, na itakuja siku wataelewa na kutoleana uvivu kwa kujenga umoja wenye nguvu ndani ya Chama.

Kasoro tuzionazo tuziweke wazi ili kuwasaidia maana kushabikia kila kitu kama mtu huna akili timamu vile ni utumwa wa kifikra.

Ningeshauri Chadema wawe na tume ya maadili ya Chama, kama wanayo ni vema na kama bado hawana basi waiunde mara moja. Na tume hiyo iwe huru kupokea maoni ya wapenzi kutokana na wengi kuonekana kufurahishwa na kasi yao. Hilo nalisema kwa vile kuna wengi wanatoa maoni mazuri kuhusu Chadema lakini ni nani anayeratibu maoni hayo? Haiwezekani maoni ya watu yamfikie kiongozi binafsi na kufanyia kazi, ila kuwe na utaratibu mzuri wa kuratibu maoni ya wetu hapo chama kitapata mawazo mengi mazuri ya kujijenga.
 
Katiba ya chadema inasemaje? http://www.chadema.or.tz/nyaraka/katiba_2006.pdf

6.3.5 Kuziba Nafasi Wazi za Uongozi
(a) Kamati ya Utendaji ya kila ngazi au Baraza Kuu itaziba kwa muda nafasi yoyote ya
kiongozi aliyechaguliwa na mkutano mkuu wa ngazi husika.
(b) Nafasi wazi za uongozi walioteuliwa zitazibwa na vikao husika kwa kufanya uteuzi
mpya katika muda usiozidi miezi mitatu tangu nafasi kuwa wazi.
(c) Muda wa uongozi wa muda kwa mujibu wa kifungu 6.3.5 (b) hautazidi mwaka
mmoja.
(d) Bila kujali sharti la kifungu 6.3.5 (c) hakutafanyika uchaguzi rasmi wa kuziba
nafasi kama kumebakia miezi sita tu au chini ya hapo kabla ya uchaguzi mkuu wa
kawaida wa Chama unaofuata kufanyika.
 

Kama hivyo ndivyo,then Baraza Kuu la Chadema Shinyanga limekosea nini hapa kumteua Kaimu Mwenyekiti?

 

huja tenda haki kwa kujaribu kumshawishi mwandishi afiche mengine!!!!
hivi ingekuwa ni habari inayomuhusu JK na EL ungetoa huo ushawishi?!!!!
forum hii haina chama kwa hiyo maoni yatolewe kwa uwazi bila kuegemea upande wowote!
shibuda ni tatizo tangu siku ile alipojitoa kwenye kinyang'anyiro cha urais!!! mara nyingi mimi hushawishika kuamini kuwa JS katumwa kukisambaratisha chicho chama!!
 

mwandishi kaweka wazi ili tujue kilichojili kule kikaoni siyo mpaka asubiri siku lema azipige na zitto ndio aanze kuelezea chanzo cha ugomvi wao, kuanzia leo tayari namjua Lema kama si mtu mwema kwa mbunge wangu zitto.asante kwa kutujuza.
 

kwa wasiomjua Zitto watasema anafanya kazi nzito.alipoanzaa alikuwa kijana mzsuri sana.lakini ulimbukeni umemponza sana,amepoteza sifa zote na hiyo ni kawaida.wanadamu huwa hatuhesabu wema wa mtu bali mabaya mangapi amefanya.kijana huyu amejaa hila kuanzia kichwani mpaka kwenye unyayo.alinikera sana alipouza mkoa wa kigoma kwa NCCr huku akiwadanganya wenzake wa chadema,usiku anafanya yake.
 
Huyu Shibuda atarudi CCM huyu. Nyi subirini tu mtaona.
 

Hiko cheo si hela yako tu, hata ukichangia BUKU unakuwa Premier Member!
 
Mi nimefurahi, na nimeipenda kama mnaweza kukaa, kuelezana ukweli, kukosoana ni vizuri kuliko mmekaa kwenye kikao mnakazi ya kusema ndiyo ndiyo alafu mkitoka nje muanza kusema fulani sijui fulani.
ni safi kupeana challenge then mnatafuta conclusion na ndio unakuwa msimamo wa chama nje na ndani ya chama.
 
huyu zitto kama kafanya hivyo ni laana tupu hafai kabisa tusilee litakuwa donda ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…