Shibuda out


Nyani halioni kundule!!!!!!
 

Mkuu nimekupata. Nianze na ukilaza wangu. Nadhani kutofautiana mawazo si ukilaza na kama ni hivyo basi kila mtu atakuwa kilaza kwa kuwa kila binadamu huwa anatofautiana na wenzake katika mahala fulani. Kuhusu wasaka tonge ni kwamba mimi siamini hiyo mikusanyiko inayoitwa vyama kwa kuwa ndani ya hivyo vyama ni mkusanyiko wa watu wanaotetea maslahi yao binafsi. Huko CCM kuna ufiisadi unaopigiwa kelele na huko chadema si unaona kuna fukuto watu hawaelewani mara wengine wanaambiwa ni mamluki na kuna kelele za ukabila pia. Kwenye vyama kuna watu wachache sana ambao wanatetea maslahi ya nchi, wengi ni watetezi wa matumbo yao!

Lema nilikuwa nikimshabikia kwa hoja alizokuwa akizitoa tangia kwenye mchakato wa uchaguzi na hadi alipomkamata koo mtoto wa mkulima pale bungeni ati amesema uongo bungeni. Baada ya hapo nikashangaa akisema milango ya bunge ifungwe ili watu wapigane ngumi. Kupigana ngumi hakujengi na hakusaidii chochote nilitegemea apigane kwa hoja. Ukipigana ngumi hupati chochote zaidi ya kudharauliwa kwa maana hiyo mimi siwezi kunufaika na kauli za ngumi mbele. Nitampigia makofi mtu mwenye hoja inayogusa maslahi ya nchi na wananchi wake lakini ngumi hapana. Sitasita kumpigia makofi Tundu Lisu, Augustino Mrema, Ole Sendeka ama mtu yeyote ili mradi tu awe na hoja na si ngumi. Nashukuru huna neno na zambarau (Manake)
 
nadiriki kuamini kwamba watetezi wengi wa cdm mbowe ni wafuata mkumbo tu, ambao hawapo tayari kupokea mawazo tofauti na wanayoyataka wayasikie!!!!
 

Magafu, umetoa hoja mhimu na nzito, lakini iko ndani ya mabano..., Hata mimi nimesikitika kwa hatua hiyo. CDM kwa hatua hiyo itapata maumivu kiasi fulani. Ninavyoangalia trend ya siasa za CDM, naona kuna incosistent judgements... Mf. Zito amekuwa akisababisha matatizo kwa kutofautiana na msimamo wa CDM openly, lakini mara zote anavumiliwa na ama kupewa ushauri nasaha. Je kwa nini kipimo hicho kisitumiwe kwa huyo Mh Shibuda, ambaye ni mbunge kwa ticket ya CDM? Kwa nini wabunge wenye nguvu ya kuzungumza na uhuru wa kufanya vurugu bila kukemewa ni watu kama lema tu? Hapo kuna mshkeli..

Ndugu Magafu, mimi ni mwana CCM tangu kuanzishwa kwake. Lakini CCM iko hoi na huenda kikavurugika zaidi na zaidi. Alternative inayovutia watu wengi sasa hivi ni CDM. Na mimi nilikuwa njiani kuelekea kufanya uamuzi wa kupata kadi ya uanachama hivi karibuni. Kwa mtizamo wangu, CDM bado wanasuasua kufikia kiwango cha kuaminika bila maswali. Na kama kungekuwepo chama kingine cha upinzania kilicho makini na kushindanishwa na CDM, basi maumivu ya chama hiki (CDM) yangekuwa makubwa zaidi.

Uamuzi wao haukupimwa kwa mapana na marefu ya kutosha. Napendekeza kwa think tanks wa chama wakusanye data mapema na ku-analyze ili waweze kukishauri chama on the mitigation steps to lessen the consequences. Dr Slaa, Dr Kitila na Mh T Lisu... chukueni hatua haraka na mwafaka kunusuru CDM. Asanteni
 


napita tu!
 
Nilikuwepo kwenye kikao mwanzo hadi mwisho. Mengi yanayoandikiwa hapa ni hisia zinazotokana na mazoea. Tatizo ni kwamba tumezoea siasa za ndiyo mzee, kitu ambacho hakipo CHADEMA. Ndani ya vikao vya CHADEMA tunajadiliana sana, mvutano ni mkubwa, tena wakati mwingine kwa ukali hadi mwafaka unapopatikana. Na mwafaka hupatikana kwa kuzingatia uzito wa hoja na ushahidi wa kutosha. Kwa sababu ya mazoea ya siasa za ki-CCM za funika kombe mwanaharamu apite, watu wakiona CHADEMA wakivutana kihoja wanatafsiri kwamba ni mgogoro au tatizo.

Ukweli ni kwamba kwenye kikao kulikuwa na mjadala mkali juu ya mambo mbalimbali. Mwisho wa siku tumefikia mwafaka na maamuzi yamefanyika kidemokrasia na amani ni tele.

Kuhusu Shinyanga, ni kwamba ukaimishaji haukufuata taratibu na kanuni za Kikatiba. Viongozi wetu wa Shinyanga walikiri kosa lao na wamekubaliana na maamuzi ya kutengua uteuzi huo hadi hapo taratibu zitakapofuatwa. Tofauti ni hio tu, kwamba CHADEMA huchukua hatua madhubuti na mapema, badala ya kufunika kombe mwanaharamu apite.

Hivyo, ndugu zangu wapenzi wa mabadiliko katika nchi hii msinyong'onyee, there is total peace in CHADEMA and the struggle continues.
 

clear and decisive

asante sana mkuu
 

Kitila, thanks for your prompt and clear clarification. I am now somehow encouraged ...
 

unaogopa ukweliiiiiiiii eeeeeeeeeeeeehhhhhhhhhhhh
 
Ama kweli Zito si Mwana CDM, bora ahamie NCCR mapema kuliko mkusubiri uchaguzi mkuu ukaribie ndipo ahamie huko ili agombee Urais kama alivyowaahidi wananchi wake kwamba uchaguzi wa mwaka 2015 atarudi Kigoma akiwa ni mgombea urais. Kwa akili yangu hawezi kuwa mgombea urais wa CDM hata siku moja mpaka mwisho wa dunia.
 
Kwa kweli Huyu Zitto haeleweki, kila controversial ya CDM lazima ahusike. Isije ikawa amepandikizwa kuiua CDM.

Hivi kuna mtu bado hajajua harakati za Zitto na Mbatia hawa si wapinzania wako kazini
 

  • Hii yadhihirisha yale yote niliyokuwa nayasema sana humu jamvini kuwa upendeleo, udini, ukabila na ukanda vitawatafuna sana CHADEMA. Na dhambi hii katu haita waacha
  • CD Mina wenyewe, na wenyewe ndio hao walio mng'oa Shibuda na kutaka kumuweka kibaraka wao
  • Ubabe wa Lema ( mzee wa funga mlango tupigane) unadhidi kujidhirisha , badala ya kushindwa kuwahudumia wananchi amekuwa mwana masumbwi
 

  • Hii yadhihirisha yale yote niliyokuwa nayasema sana humu jamvini kuwa upendeleo, udini, ukabila na ukanda vitawatafuna sana CHADEMA. Na dhambi hii katu haita waacha
  • CD Mina wenyewe, na wenyewe ndio hao walio mng’oa Shibuda na kutaka kumuweka kibaraka wao
  • Ubabe wa Lema ( mzee wa funga mlango tupigane) unadhidi kujidhirisha , badala ya kushindwa kuwahudumia wananchi amekuwa mwana masumbwi
 
Kwa usahihi ni kwamba maamuzi yalishatenguliwa na kamati kuu na baraza kuu lenye sauti ya mwisho tukaridhia pendekezo la kamati kwa kwa sababu hayakufuata desturi ya kitanzania na kanuni za chadema. Sababu za kutengua ni hizi kwa ufupi sana zilizo wasilishwa katika baraza kuu na kamati kuu.
Haiwezekani wengine wanazika na wengine wanajaza nafasi ya anyayezikwa kwa wakati mmoja. Desturi ya wapi?
Pili, Ni majuzi tu Shibuda alitoa kauli tata Bungeni huku akisifia CCM. Kauli ile ilwaumiza wengi sana nikiwepo mimi mwenywe.
Tatu, alipewa kazi rahisi sana ambayo ingemchukua kamat dk 10 kumaliza tatizo hili akitaka. Kazi hiyo ni kuandika barua ya kuwaomba radhi wabunge wa chadema. Hakufanya hivyo. Je, huyu awe msemaji wa mkoa wa Shinyanga unaoamka kwa kasi kubwa kutaka mabadiliko?
MAAMUZI YALIVYOFIKIWA.

Kamati kuu Mjumbe 1 alipinga, 3 waliabstain, na 18 waliunga Shibuda kuondolewa.
Baraza kuu,
Waliunga mkono hoja kwa asilimia mia moja bila kubadili chochote.
kwa hiyo, hii si maamuzi ya Slaa au mbowe au Zitto ama mtu yeyote bali vikao husika.
Nimeona nitoe taarifa hii maana naona wengine wanapotosha watu humu ndani.
 

With due respect, Dr. Kitilb amekuwa mtetezi mkubwa wa ukandamizaji wa demokrasia ndani ya cdm, tunakumbuka maelezo yake juu ya chaguzi za Vijana, wabunge wa viti maalumu na hata uchaguzi mkuu wa cdm.
 

Hapo kwenye red utakuwa unamsingizia kamanda wetu bana bwahaaaa haaaa.
 
With due respect, Dr. Kitilb amekuwa mtetezi mkubwa wa ukandamizaji wa demokrasia ndani ya cdm, tunakumbuka maelezo yake juu ya chaguzi za Vijana, wabunge wa viti maalumu na hata uchaguzi mkuu wa cdm.

Kumbe na wewe umeliona hilo.
 
kweli au sio kweli.. kama kuna aliyekosea lazima aambiwe ukweli, this things do happen everywhere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…