Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

naomba kamati aya maadili ya chama ikae mapema kumshughulikia yule mzee wa kughani mashairi. inaonekana kuwa atakuwa kikwazo kikubwa kwa chama na mustakabali wake katika siku zijazo. shibuda ni tatizo kwa chama. naomba kuwasilisha.
 
yaonyesha kuwa Shibuda si mmojawapo wa CDM. Hana taarifa na yanayofanywa na WanaCDM kama wabunge. Yupo yupo tu kama mtu aliyekosea njia. Kama hayo ni maoni binafsi je na posho anachukua!!??
jaribuni mfe! Hivi mnamuonaje Shibuda? Mnamchukulia simple sana,sasa mkimtimua Chadema atahama na kwenda chama kingine na mtakutana bungeni.Mbowe take it frm me.
 
huyu muheshimiwa ana ka ugonjwa kanakoitwa BIPOLAR DISORDER.
Kwa sababu ametofautiana na wewe. Tatizo chenu si chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuwa kingekuwa hiko kingestawisha fikra huru na kukubali mtawanyiko wa mawazo. Haiwezekani chama kikaendekeza ukiritimba wa mawazo kiasi kwamba mtu akija na fikra zilizo nje ya wigo wa Slaa au Mbowe anahesabiwa kama muasi. Hizi si enzi za zidumu fikra za mwenyekiti. Hakuna sababu ya kubinya uhuru wa kujieleza. Mkishika nchi mtakuwa madikteta.
 
Kwa hili naona sasa viongozi wa CHADEMA watajifunza kwamba kuna umuhimu kuwachunguza kwa makini watu wanaotaka kuwapa dhamana ndani ya chama. Huyu jamaa alishakuwa wa hovyohovyo tangu bado yupo magamba na wasipomdhibiti mapema ataleta shida nyingi sana huko mbele. Mimi binafsi simpendi mtu huyu!
Kwa hiliCDM wanadhihirisha utoto wa kiwango cha juu. Mbona CCM wengine wamepinga suala la posho na wengine kama Makamba wameunga mkono lakini hatujawaona wakiitisha press conference za kizembe kuwafundisha watu jinsi ya kufikiri. Nawaambia na narudia tena. lazima muwe makini sana na jinsi ya kushughulikia tofauti za mawazo. Vinginevyo mtauharakisha mwisho wenu.
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.

mshikaji unajua kila siku huwa unatema pumba mpaka basi. mi nadhani umefunga ndoa na magamba na ujue Mungu atakuchoma moto kwa kuendekeza tamaa mbele
 
mshikaji unajua kila siku huwa unatema pumba mpaka basi. mi nadhani umefunga ndoa na magamba na ujue Mungu atakuchoma moto kwa kuendekeza tamaa mbele
JF, kuna watu wana akili masizi kama huyu, ngoja nikuulize kwa hiyo Mungu yupo Chadema?
 
wanajf huu msuguano wa chinichini kati ya viongozi wa juu wa cdm na huyu kibaraka shibuda hautaleta athari kwa cdm?nawasilisha,youk
 
Yule jamaa kibaraka sana, atimuliwe mapema tuu kabla hajaleta madhara zaidi!!
 
Hana madhara yoyote hata alivyoondoka ccm hajaonyesha madhara!
 
hali ya mambo ndani ya chama cha democrasia na maendeleo chadema si shwari baada ya mbunge wa maswa magharibi, john shibuda, kuwatolea uvivu viongozi wa juu wa chama hicho, akisema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi hao, alisema kutokana kutoka na hali hiyo, yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote, hivi karibuni amfadaiwa kwenda kinyume na msimamo wa chama chake, kuhusiana na suala la posho za wabunge,kitendo ambacho kimemfanya aonekane muasi ndani ya chamana hivyo kuundiwa tume ya kumchunguza. shibuda alibeza shutuma hizo na kuwataka viongozi wa kumuomc radhi hata hivyo atandaa mikutano ya hadhara kuwaeleza wanainchi tabia ya viongozi hao(mbowe na zitto)..... nukuu MTANZANIA la leo
 
Ndugu zangu katika hali ya siasa sijawahi kumuona mtu asiye na adabu wala hekima kama Shibuda. Shibuda alianza kwa kumtishia rais Jakaya kuwa angeweza kugombea na kumuondoa katika utawala ndani ya ccm. Baada ya kuona kuwa anaota ndogo za alasiri,aliamua kuchanga hela ya kumchukulia mh.rais fomu za kugombea urais. Shibuda aliamua kuhama ccm kwa kukejeli na kurusha vijembe vya ajabu ajabu kwa mwenyekiti wake wa zamani mh.Kikwete,akaenda chadema akapata ubunge. Alipoambiwa afuate masharti ya cdm ya kuisusia hotuba ya yule aliyesema hana uwezo wa kumuongoza na kuliongoza taifa,bado akaendelea kukataa na kuhudhuria. Pia akaudhuria sherehe ya kumwapisha waziri mkuu wakati chama chake kilipinga. Akaja katika maandamano ya cdm akawaponda na kuwadharirisha mh.Nape, mwakyembe na mzee sitta kuwa ni wanasaliti,wanafiki na ndumila kuwili kwa kuwa ni wanachama na waanzilishi wa CCJ. Watu wakajua siri nyingi zilizojificha katika nyoyo za wanaccm hawa. Pia kawaharibia uaminifu na uadilifu katika ccm. Kama haitoshi Shibuda alipewa ilani ya chadema ambayo pia ndani yake inayokataza kuwa na posho zisizo na mashiko pamoja na kuyakataa mashangingi,kama 'punguani' ameenda bungeni na kupinga hadharani na anataka posho ipande. Cha ajabu hata ccm kupitia waziri mkuu wameweka wazi kuwa posho zitaondolewa au kuunganishwa na mishahara ili ikatwe kodi. Sasa Shibuda anaipinga cdm akiwa ndani na anaipinga ccm akiwa nje,alaf anadai vyama vingne ni mamluki,je shibuda anasimama wapi? Kwa kumpinga Zitto na mbowe,nape,jk,6,mwakyembe,sasa anataka tuone kuwa yeye tu ndo yuko msafi??! Chadema ichukueni kadi ya shibuda muiweke makumbusho. Shibuda hatapata mwenyeji mwingine kwa tabia zake za ajabu. Kabla hapajakuwa na harakati za kudai haki sawa,zamani wazee wetu wangesema Shibuda ana tabia za kike. Ila kwa kuwa ishaonekana sio sahihi kuwasema wanawake,basi hata mi sitasema ivo. Shibuda kama ni mti basi ni mpapai,hafai kwa kujengea,hafai kwa kuni,hafai kwa kuchomwa hata mkaa,zaidi hatofaa hata kujengea daraja. Siwezi kumuita shibuda mamluki ndani ya cdm ila namuona kama mtu anayekosa malezi na kuota sharubu. Chadema muweke kando uyu mtu,arudishe kadi,turudi kwenye uchaguzi ili hata ikiwezakana twende maswa kama ccm na cdm kuwaomba wananchi kura bila ya kuwa na shibuda. Mwache aende kama mgombea binafsi au hata ajiunge chama cha tatu kama watamwitaji. Taifa lisisumbuke na mtu uyu maana alipotoka ccm tukajua labda kachoshwa, kaenda ccj hakukaa,kaja cdm na sasa analeta maajabu. Iyo inaonesha kuwa yeye ndo mwenye vilema. Chadema mfukuzeni Shibuda.
 
madhara itakuwa kwenye kugombania jimbo,kwa vyovyote ile takataka itaondoka na uchaguzi utafanyika
issue hapa je chadema itashinda tena jimbo la maswa??
 
Si lazima kushinda majimbo yote, pia kama chama kinasimamia haki ya wananchi juu ya POSHO nadhani kitashinda tena kwa kishindo. Afukuzwe mi mwenyewe mwezi uliopita nilikwaruzana naye pale Rombo Green view wenzake wapo bungeni yeye yupo Rombo mjinga sana. Huyu ni kansa mbaya aondoke wakati ndio huu.
 
hali ya mambo ndani ya chama cha democrasia na maendeleo chadema si shwari baada ya mbunge wa maswa magharibi, john shibuda, kuwatolea uvivu viongozi wa juu wa chama hicho, akisema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi hao, alisema kutokana kutoka na hali hiyo, yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote, hivi karibuni amfadaiwa kwenda kinyume na msimamo wa chama chake, kuhusiana na suala la posho za wabunge,kitendo ambacho kimemfanya aonekane muasi ndani ya chamana hivyo kuundiwa tume ya kumchunguza. shibuda alibeza shutuma hizo na kuwataka viongozi wa kumuomc radhi hata hivyo atandaa mikutano ya hadhara kuwaeleza wanainchi tabia ya viongozi hao(mbowe na zitto)..... nukuu MTANZANIA la leo

Shibuda siku nyingi ni huwa anajiamulia yeye mwenyewe hata misimamo ya chama chake huwa hajali,tabia za viongozi wengi huwa zinajulikana,lakini kama huwa wanakwenda kinyume cha maazimio ya chama huwa ni tatizo.Naona shibuda anataka kutangaza pivacy za viongozi wake,kwetu si hoja,hoja kwetu ni je wanatekelezaje maazimio na misimamo ya chama? kama hapo wanakwenda kinyume inabidi sisi wananchi tuwakemee au tuwaondoe uongozini,Shibuda aelewe kuwa Posho zinatumika vibaya na kwa manufaa ya wachache hivyo hazina budi ziondolewe kuanzia bungeni,ndio tunaweza kuwabana watumishi wengine wa serikali,mfano mkurugenzi wa idara ya serikali mshahara 500,000.00 posho za vikao kwa mwezi ni 3.0m huoni huo ni wizi,unakaa vikao kwa ajili ya kufuatilia na kupanga mipango jinsi idara yako itakavyo perfom,hii ni moja ya kazi yako unajilipa tena, huu ni wizi kabisa.Hawa wafanyakazi wa chini wanaosubiri maelekezo ya viongozi wao wanapiga miayo,Shibuda uelewe hili limetoka kwa wafanyakazi wa chini,sasa hivi tukiwa na matatizo tunapeleka CAHADEMA watusaidie kuyaweka vizuri na kuyapigia kelele,shibuda elewa hili limetoka kwetu wafanyakazi wa chini,kama ambavyo tuna omba CDM waitishe maandamano juu ya hali mbaya ya umeme,viwanda vimefungwa,wanyonge tunaotumia umeme kujiajiri hakuna tena ajira,
 
Ya Shibuda na CDM nawaachia wana-CHADEMA. Ila siku chache kabla ya uchaguzi, Rev. Kishoka aliwaonya CDM kuwa wasikubali kuchukua makapi ya CCM, na hawakumsikia. Ninaweza kuelewa iwapo katika swala la shibuda CDM walikuwa wanataka kupunguza idadi ya wabunge wa CCM, ila kuamnini kuwa Shibuda ni mwanaharakati mwingine nadhani walikosea; ni kama NCCR-Mageuzi walivyokosea kwa kumpokea Wassira akitokea CCM.
 
Ndugu zangu katika hali ya siasa sijawahi kumuona mtu asiye na adabu wala hekima kama Shibuda. Shibuda alianza kwa kumtishia rais Jakaya kuwa angeweza kugombea na kumuondoa katika utawala ndani ya ccm. Baada ya kuona kuwa anaota ndogo za alasiri,aliamua kuchanga hela ya kumchukulia mh.rais fomu za kugombea urais. Shibuda aliamua kuhama ccm kwa kukejeli na kurusha vijembe vya ajabu ajabu kwa mwenyekiti wake wa zamani mh.Kikwete,akaenda chadema akapata ubunge. Alipoambiwa afuate masharti ya cdm ya kuisusia hotuba ya yule aliyesema hana uwezo wa kumuongoza na kuliongoza taifa,bado akaendelea kukataa na kuhudhuria. Pia akaudhuria sherehe ya kumwapisha waziri mkuu wakati chama chake kilipinga. Akaja katika maandamano ya cdm akawaponda na kuwadharirisha mh.Nape, mwakyembe na mzee sitta kuwa ni wanasaliti,wanafiki na ndumila kuwili kwa kuwa ni wanachama na waanzilishi wa CCJ. Watu wakajua siri nyingi zilizojificha katika nyoyo za wanaccm hawa. Pia kawaharibia uaminifu na uadilifu katika ccm. Kama haitoshi Shibuda alipewa ilani ya chadema ambayo pia ndani yake inayokataza kuwa na posho zisizo na mashiko pamoja na kuyakataa mashangingi,kama 'punguani' ameenda bungeni na kupinga hadharani na anataka posho ipande. Cha ajabu hata ccm kupitia waziri mkuu wameweka wazi kuwa posho zitaondolewa au kuunganishwa na mishahara ili ikatwe kodi. Sasa Shibuda anaipinga cdm akiwa ndani na anaipinga ccm akiwa nje,alaf anadai vyama vingne ni mamluki,je shibuda anasimama wapi? Kwa kumpinga Zitto na mbowe,nape,jk,6,mwakyembe,sasa anataka tuone kuwa yeye tu ndo yuko msafi??! Chadema ichukueni kadi ya shibuda muiweke makumbusho. Shibuda hatapata mwenyeji mwingine kwa tabia zake za ajabu. Kabla hapajakuwa na harakati za kudai haki sawa,zamani wazee wetu wangesema Shibuda ana tabia za kike. Ila kwa kuwa ishaonekana sio sahihi kuwasema wanawake,basi hata mi sitasema ivo. Shibuda kama ni mti basi ni mpapai,hafai kwa kujengea,hafai kwa kuni,hafai kwa kuchomwa hata mkaa,zaidi hatofaa hata kujengea daraja. Siwezi kumuita shibuda mamluki ndani ya cdm ila namuona kama mtu anayekosa malezi na kuota sharubu. Chadema muweke kando uyu mtu,arudishe kadi,turudi kwenye uchaguzi ili hata ikiwezakana twende maswa kama ccm na cdm kuwaomba wananchi kura bila ya kuwa na shibuda. Mwache aende kama mgombea binafsi au hata ajiunge chama cha tatu kama watamwitaji. Taifa lisisumbuke na mtu uyu maana alipotoka ccm tukajua labda kachoshwa, kaenda ccj hakukaa,kaja cdm na sasa analeta maajabu. Iyo inaonesha kuwa yeye ndo mwenye vilema. Chadema mfukuzeni Shibuda.
Mkuu naona unaongelea watu wawili tofauti, unaeleza habari za Mpendazoe halafu unamtaja Shibuda, aliyetoka CCM na kwenda CCJ kisha Chadema ni Mpendazoe na kwa sasa sio mbunge, anayesuguana na Chadema kwa sasa ni Shibuda na ndo mbunge wa Maswa Magharibi.

Back to the topic; Chadema wanatakiwa kuwa makini jinsi ya kudeal na watu, kumbuka m/kiti wa chama siyo mwalimu mkuu wa shule kwamba lazima wanafunzi wamtii na wala sio kiongozi wa batalion kwamba lazima wanajeshi waliochini yake wakubali mtazamo wake, wangeruhusu uhuru wa mawazo kutofautiana kimawazo ni kitu ambacho kipo kila mahali hata makazini.

Sijaisoma sera ya Chadema kuhusu posho lakini nina uhakika haitaji posho specific kwamba watakataa posho ipi na watachukua ipi kwa hiyo wao wangewapa uhuru wabunge wao anayetaka achukue halafu wapiga kura wake watamhukumu hapo baadaye.

Pia lazima tukumbuke sera sio sheria kwamba lazima ifuatwe na kila mtu, labda watuambie sera yao ya posho inakataza posho zipi?
 
Back
Top Bottom