Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Kuna kirusi Marando bado anawapimia Cdm siku akiuhitaji ukatibu Mkuu wake kujikumbushia kama alivyokuwa NCCR Mageuzi miaka ya tisini mtamtaka maake itakuwa ama zake ama za CDM kisha akibwagwa atarudi magamba akidai ''mwana mpotevu''.Marando si mvumilivu kutumikishwa tena na Slaa,wakati alikuwa bosi katika siasa katika ngazi ya Taifa wakati Slaa ndio kwanza anajifunza siasa katika ngazi ya ubunge.

CDM watch Marando,ni mzuri kwa muda tu na hubadilika iwapo watu watataka kung'ang'ania kwenye viti vyao huku na yeye amechoka kusimama,anataka kiti akae.''sweet part of it''.
 
Hana madhara yoyote hata alivyoondoka ccm hajaonyesha madhara!

Unasema haujaleta madhara kamuulize JK jimbo la Maswa alipata kura ngapi na hao CCM waulize kutoka Maswa walipata wabunge wangapi wakishakupa majibu njoo tena useme kama ulikuwa na madhara au haukuwa na madhara.
 
Shibuda kama ulizoea kuropoka CCM sawa, lakini huko ulipo upo kwenye taasisi ya wenyewe mawaza yao ndio sahihi
 
*Avaa viatu vya marehemu Chacha
*Asema CHADEMA inanuka ubinafsi
*Ajipanga kueleza maovu ya Mbowe, Zitto
*Asema hatishiki, yupo tayari kufukuzwa.
*Awashutumu Mbowe Zitto wameigeuza Chadema kampuni
*Ajiandaa kuzunguka nchi nzima kuueleza umma ukweli
*Mbowe ajibu, asema hapendi malumbano, wakati utafika

HALI ya mambo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), si shwari, baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, kuwatolea uvivu viongozi wa juu wa chama hicho, akisema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi hao. Alisema kutokana na hali hiyo, yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote. Hivi karibuni, Shibuda amedaiwa kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake, kuhusiana na suala la posho za wabunge, kitendo ambacho kimemfanya aonekane muasi ndani ya chama na hivyo kuundiwa tume ya kumchunguza.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili mjini Dodoma jana, Shibuda alibeza shutuma hizo zilizoelekezwa kwake na kuwataka viongozi wa juu wa chama hicho kumwomba radhi kutokana na kumchafua. Shibuda aliwataja viongozi hao ambao alidai wanamchafua kupitia vyombo vya habari kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto. Hata hivyo Shibuda alisema mbali ya kuombwa radhi, pia atalazimika kuandaa mikutano ya hadhara yenye lengo la kuwaeleza wananchi tabia za viongozi hao.


“Natarajia kusafiri kwenda nje ya nchi kwa shughuli za kibunge, nitakaporudi, nitaitisha mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali nchini kuwaeleza wananchi juu ya Zitto na Mbowe, ambao tayari wameshanishutumu kupitia vyombo vya habari. “Mikutano hiyo nitaianzia jimboni kwangu mwishoni mwa mwezi huu, nitaweka wazi kila kitu kwa sababu wananchi ndio wenye chama na wana haki ya kujua nani anasema ukweli na nani anasema uongo. “Hata hivyo, kabla mimi sijaenda kwa wananchi nawaruhusu wao waende kwa wananchi wakanishitaki, wakaeleze ubaya wangu ili mimi nitakapowaeleza wananchi basi wao ndio wapime wenyewe. “Mimi nayajua mengi sana ya CHADEMA, kwa muda mfupi niliokaa katika chama hicho nimejionea mengi sana na nalazimika kusema kuwa alichokuwa akikisema Chacha Wangwe (marehemu) ni sawa kabisa na hakukosea kitu. “Nakwambia sura ya CHADEMA ukiwa nje ya chama ni tofauti na sura ya CHADEMA ya ndani, ni tofauti kabisa kwa sababu yanayofanyika humo ni mambo ya ajabu sana.


“Mbowe anaendesha chama kibabe na anaungwa mkono na Zitto ambaye anaonekana kuwa na tabia ya ukuwadi na unafiki, mimi siwezi kunyamaza, siwezi kufumbia ukweli katika jambo ambalo naamini ni sahihi. Niliyosema nimeyasema na kama hayakuwafurahisha sitawaomba radhi na sina tabia ya kuomba radhi, kwani hata nilipokuwa CCM sikuwahi kuomba radhi. “Lakini kwa kuwa wao ndio wamenikosea kwa kunichafua kupitia vyombo vya habari, basi nawataka waniombe radhi kwa waliyonizushia na pia nawataka wawaombe radhi Watanzania kwa kutowaambia ukweli,” alisema Shibuda.


Katika maelezo yake, Shibuda, ambaye alihamia CHADEMA mwaka jana akitokea CCM, baada ya kushindwa katika kura za Mahon, alisema pamoja na kwamba Mbowe na Zitto wanaamini wako sahihi, ukweli utabaki pale pale kwamba wanasiasa hao wanahatarisha demokrasia katika chama hicho. “Hili suala la posho ambalo ndilo chanzo cha haya, nakwambia siyo msimamo wa chama kama wanavyowaambia Watanzania, huo ni uamuzi wao wawili tu kwa sababu katika vikao walikuwa wanawatisha wabunge na kuwatishia kwamba watawafukuza kama hawatakubali kukataa posho.


“Huwezi kuendesha chama kwa nguvu kwa sababu hizo posho ndicho kipozeo cha mbunge, kwani kama ng’ombe anayekamuliwa akikosa malisho ukimkamua ujue atatoa damu. “Sasa kama ndivyo hivyo, wabunge wasipolipwa posho kazi zao watafanyaje, katika hili siwezi kunyamaza, nitaendelea kuheshimu uongozi kwa ajili ya kujenga ufanisi wa maslahi ya chama ya kutajirisha masikini dhidi ya vatu, cheo ni dhamana. “Sitoona haya kukosoa tabia ya umimi na uyeye kwa mtu yeyote, sitahama CHADEMA kwa sababu sikutofautiana na chama bali nimetofautiana na watu wachache kutokana na kutoridhishwa na uongozi wao,” alisema.


Akimchambua Zitto, alisema anajifanya mzalendo machoni pa watu wakati tabia na matendo yake ni tofauti na anavyowaambia Watanzania. “Zitto siyo mzalendo, namtaka aache tabia ya ukuwadi na kuunda uzandiki wa kufunika uwazi na ukweli kwa dhamira ya ubinafsi wa kujikweza kisirisiri ili apendwe na uongozi na kuidanganya jamii kwamba yeye ni mwadilifu. “Zitto asigandamize haki za watu, wanaojua stahili zao kwa sababu yeye anajipamba ili asihitilafiane na kiongozi wake kwa masilahi yake binafsi, aache tabia ya kujifanya mzalendo wakati ni mnafiki anayetaka kujenga matarajio yake binafsi huku akificha ajenda ya siri ya umimi na uyeye. “Ili kutambua tabia yake na mwenzake huyo ni sawa na mwenye kiatu ambaye ndiye anayejua jinsi kinavyomuumiza badala ya mtazamaji ambaye anafurahishwa na rangi ya kiatu, aache kabisa tabia hiyo awe wazi na asitafute umaarufu,” alisema. Alisema kinachomgombanisha na
wenzake ndani ya chama hicho ni tabia yake ya kupenda uwazi, wakati baadhi ya wenzake wanataka ukweli usielezwe kwa wananchi.

“Chuki iliyopo ni kwamba mimi Shibuda napinga chama kuwa kama kampuni ya kuingiza wanachama wa kutekeleza masilahi binafsi ili kudumisha ukabila, uyeye, umimi, uwao, umajimbo ambao umefichwa na msemo usemao siri ya mtungi aijuaye kata. “Binafsi sitarudi nyuma, naahidi kulinda maslahi na kutetea shabaha ya CHADEMA kwa maslahi ya wananchi, nitaendelea kupingana na tabia ya kuwaonea watu kwa sababu wabunge maskini kama mimi tunapata fedha za kuwahudumia wananchi kwa kudunduliza fedha za mishahara na posho.

“Wabunge matajiri wao wana mapokeo ya hisa kutoka katika biashara zao binafsi, kwa hiyo ndondondo za mapato kutoka bungeni hawazihitaji, ndiyo maana wanawalazimisha wenzao wasiokuwa na kitu wafuate nyayo zao hata kama wanawaumiza,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, Shibuda alisema atahutubia mikutano ya hadhara wakati wowote mwishoni mwa mwezi huu baada ya kurejea nchini, ili kuweka wazi tabia za badhi ya viongozi wa chama hicho. Juni 28 mwaka huu, akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka wa fedha 2011/2012, Shibuda aliitaka serikali iongeze posho za wabunge kutoka Sh 150,000 hadi Sh 500,000 kwa siku, kwa kuwa kiwango cha sasa hakitoshi. Akijibu shutuma hizo, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, alisema hapendi malumbano kupitia biombo vya habari. “Kamanda sipendi malumbano kwenye vyombo vya habari, tusubiri muda ukifika ukweli utajulikana tu,” alisema Mbowe

Mtanzania


 
Mkuu hii ni habari ya kesho au ya gazeti la leo?....anyway, Shibuda ngoja ajidanganye tu..atafukuzwa na sidhani kama kutakuwa na chama cha kumpkea maana tabia yake inajulikana huyu
 
Daaaa, jamaa heri aanze vita kati yake mwenyewe na minuso ya bure.

Anaweza hata kuacha msiba nyumbani kwake na kwenda kwenye minuso ya Magambaz....

jk+na+kijana+wake.JPG


[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Shibuda amgwaya JK [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Wednesday, 16 June 2010 09:11 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Habel Chidawali,Dodoma

HATIMAYE mbunge wa Maswa, John Shibuda hatapambana na mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa tiketi ya CCM baada ya kutamba kwa muda mrefu kuwa hakuna atakayemzuia kutekeleza azma yake.

“Sitaki kuwa kama maji ya kuzimuni yasiyokata kiu ya malaika hivyo niendeleze kuzurura ovyo na fikra za wana-CCM za je, Shibuda atagombea kiti cha urais na anampinga Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete,” alisema Shibuda ambaye ni mwingi wa misemo anapofafanua jambo.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Bungeni si pahala pa kuganga njaa,kwa style hiyo this guy anajibainisha true colours zake zinazoumiza macho.
 
we said long ago... shibuda ni malaya wa kisiasa
 
Nilipoona title nilishituka kweli. Lakini nilipoangalia chini na kukuta source ni mtanzania, hata habari yenyewe sijaisoma.
 
Chadema haina demokrasia siku zote! Kila mwana chama ana haki ya kutoa mawazo yake! Shibuda aliongea anacho amini hata suala la madiwani arusha ni ubabe tu wa mbowe! Huyu mbowe anaona ana hati miliki ya Chadema kisa chama cha baba mkwe wake Mzee Edwin Mtei! Mbowe badilika sasa ipi chadema sura ya kitaifa na sio kampuni ya mtu binafsi!
 
Shibuda ni garasa tu hana lolote !asijilinganishe na hayati chacha wangwe hata kidogo.cdm piga chini hili lizee likaombe radhi ccm.
 
Kinachonishangaza kwanini haya wasiyaongelee kwanza kwenye chama kuliko kupashana hadharani kama mipasho. Najiuliza kwanini Shibuda kabla ya kusimama na kuunga mkono posa alijua fika chama chake kinamsimamo gani, kwanini hakupinga kwanza ndani ya chama kabla ya kuamua kuwapinga wenzake.Labda Shibuda atueleze ni jitihada gani alizowahi kuzifanya kupinga mambo anayoyaona hayaendi sahihi ndani ya chama? Anataka kutuambia viongozi wa chama chake si wasikivu?
 
Hakuna kitu kizuri unapopambana na adui unaemjua uwezo wake! Shibuda anaeleweka na ilitarajiwa ataleta vurugu, hivyo cdm ilishajiandaa kumdhibiti! Mpaka hapo alipo amedhibitiwa vilivyo!!!!!!!
 
1. Ni vizuri Shibuda apate nafasi kueleza CHADEMA ndani ya uongozi kukoje.

2. Nilishawaambia CHADEMA kitambo hapa, kabla hata ya uchaguzi, kwamba huyu Shbuda atawaharibia chama, anachotaka yeye ni fahari ya uongozi tu bila kujali chama, nikaonya CHADEMA wasikimbilie kumpa uongozi.

Sasa inakuwa habari ya sikio la kufa halisikii dawa na majuto mjukuu.

I hate to say I told you so, but I told you so.
 
Ni aibu sana tena sana kwa mtu mzima kutokuwa na jambo la msingi unalosimamia (without principles). Shibuda bado yuko kwenye siasa za miaka ya 1947, siasa za kitengo cha PROPAGANDA. Na aibu zaidi ni kuwa huyu Mheshimiwa amejiaminisha kuwa ana 'nguvu' mbele ya watanzania. Anaweza akawa mahiri kwa kutunga beti za kiswahili na kuchekesha bunge lakini kamwe hawezi 'weapon of mass destruction' kwa CHADEMA. Walimtuma wajue sasa hivi wanachi ndio wameshika hatamu na hata umaarufu wa CHADEMA unatoka na wao (chadema) kugundua hilo na hivyo kufanya 'people's politics' na sio huu umamluki na uposho wa Shibuda.

Hata hivyo burudani ni burudani tumsikilize huyu bwana akitunga beti za kujimaliza. Shibuda we were delighted to have you around!
 
Unajua kuna watu wengune utafikiri wanafikiri kwa kutumia sehemu za chini ya mgongo badala ya ubongo. Sasa atashtaki kwa wananchi atawaambiaje? Kwamba yeye anataka posho na Chama chake kinataka hizo posho zitumike kwa maendeleo ya wananchi? Ni nani ataonekana mkosaji? yeye au chama?
 
kamanda mbowe fukuza pandizi la magama..wapambanaji hawana tabia za kijinga kama zake...
 
source: mtanzania

Kwa mtazamo huu hatuendelei. Hili ni gazeti lililosajiliwa kihalali na linatoa habari kwa kiwango kinachokubalika. Mhariri wa gazeti alifanya mahojiano na Shibuda na kuandika habari hii, na anana ushahidi, sioni hoja ya kubeza habari wakati hali ilivyo juu ya Shibuda na Chama chake tunafahamu.
 
Back
Top Bottom