Mjadala huu umeongea makosa makubwa ya Shibuda kuwa: Hana ushirikiano wa pamoja na wenzake, he is not well informed of what is going on in CDM, Anatoa msimamo tofauti na chama chake, ni CCM akifanya upelelezi CDM, Hahudhurii vikao vya chama/wabunge wenzake na anabwabwaja nje tu
Ambacho sikukiona na hoja muhimu aliyoisema shibuda katika habari kuu kwamba….
- Atashangaa sana na hatarajii kama CDM kuna viongozi wanaweza kudidimiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni huru, wakati chama kinafanya maandamano kutoa maoni huru kwa Watanzania. Kama yeye hatakiwi kufanya hivyo, basi nini maana ya kuandamana kutoa maoni kwa Watanzania".
- Mbunge anapozungumza bungeni anasema kwa maana pana kwa watu wenye mitazamo tofauti kwa lengo la kuleta fikra endelevu".
- Hana habari kama wabunge wote wa Chadema walikutana na kukubaliana kuikataa posho.
Nikiongelea highlights hapo juu, Moja: Je Demokrasia inayopiganiwa na CDM ni ile ya uamuzi wa (Chama) wa pamoja au ile ya mtu kuwa huru kutoa mawazo kwenye mambo yanayoathiri maisha yake? Pili: Je Shibuda ni mbunge wa Maswa kupitia CDM au mbunge wa CDM kupitia kupitia wilaya ya Maswa; Tatu: Je ni wabunge wote walikaa wakakubaliana kwenye hili, na kwa nini liwe hili tu la ‘posho' na isiongezwe na mishahara ya wabunge kama ilivyoainishwa katika ilani ya CDM ya mwaka 2010.
Swali la mwisho kwa mwenye kufikiri: Je kabla ya kumsajili Shibuda kuwa mchezaji wa CDM kuna sehemu yoyote iliyomtaka abadilishe misimamo yake ambayo ilifahamika sana toka alipokuwa jumuia ya wazazi? Labda kikubwa ni kwa CDM kuwa na orodha ya watu ambao ingependa wajiunge na chama chao ili kuepuka migongano iliyowahi kujitokeza kuanzia kwa kina Wangwe (RIP), Zito, Kafulila, na sasa Shibuda. Na ili hilo lifanikiwe itabidi wapate watu wenye sifa kuu ya kudumisha fikra sahihi za ‘kidemokrasia' za Mwenyekiti na Katibu wa CDM.