Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Nina hamu sana kusikia wasaliti wa sera mbadala za wananchi wakichinjiwa baharini...Mimi binafsi simkubli Shibuda toka amehamia CHADEMA. Ni mtu mwenye jazba, hasira, mropokaji, mswahili halafu top in top ni mpenda madaraka saaana. Asije akajidanganya kuwa Shinyanga wamechagua mtu. Wale wanachagua jembe lolote toka CHADEMA hata akiwa bwana Eliesikia ndio anaomba kura. Majimbo 8 Manne CHADEMA, Moja mjini liliharibika na CCM matatu(moja la jembe Lembeli).myVision:Mi ninachotaka CHADEMA wasimung'unye maneno wala kufinyanga hiyo kesho au kesho kutwa baada ya kikao tumpe Tiketi apotelee mbali.Tuacha woga lile jimbo tunashinda sisi kama sisi CHADEMA.
uko sawa kwani ni bora kubaki na wabunge wachache walio makini kuliko kuwa na wabunge wengi wa aina ya Shibuda!
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.
Acha fikra potofu za ubaguzi wa kikanda na kikabila. Mchango wako umejaa uchonganishi na siasa za chuki.
 
mkuu uko sawa kabisa.
Mi binafsi namdharau sana Shibuda, mnafiki sana huyu baba. Anakwaza watu kwa makusudi. Akifukuzwa itakuwa poa sana.
 
unajitahidi kufitini ili CDM iingie kwenye mgogoro usio wa lazima lakini utashindwa tuuuuuuuuuuuuuuuuuuu aliyekuajiri kwa hilo ameula wa chuya CDM wanayo mambo makubwa ya kushughulikia siyo hilo la Shibuda. CCM waanze kufukuza Mwakyembe, Sita na Mnauye

Mimi sio mgumu ww? Kama hujui historia yangu humu JF usichafue hewa humu.. Nenda pale juu kwenye search andika Eliesikia halafu uone hizo thread zangu.
Mimi nimefungiwa wiki kazaaa kisa kugundua janja ya Nape na Akaunti yake ya Achebe. Si umeona hatusikii tena ya Achebe zaidi ya utumbo wa Jr Live..
Twende kazi...
Kama ww ni Shibuda I'm sorry. Sisi tutamfukuza chamani
 
Kwani CHADEMA msukuma ni yeye tu....Sheikh Makani yupo muda mrefu...hoja yako dhaifu sana

Makani ni scrap kwa sasa.
Pia ujue kuwa hayuko kwenye ngazi ya Shibuda kuhusiana na ushawishi kwa wazee.
Makani alikuwa brainwashed zamaani baada ya kupata elimu na kupata madaraka makubwa serikalini akawasahau wazee wa eneo anakotoka.
Iwapo Shibuda atafukuzwa, CDM itapata hasara kali .
 
I think it is not advisable for CDM to throw out Shibuda on such an issue. CCM as a party is prone to such actions. CDM should be a forward looking political party which can tolerate dissent as long as it does not harm the main fabric of the party.

Democracy in its true sense cannot subject an individual to party dictatorship. The point is, CDM much as it is fighting for broader democracy in the country, it should not forget that it must build internal democracy within the party as well. I don't know if there was a meeting in which Shibuda was involved which forged a party stance on the matter.

CDM should view this MATTER AS A CHALLENGE on its internal procedures in force for such situations.

The point I am driving at is that, what rules and procedures are there that guide the behaviour of its members whether in parliament or in other fora? What are the policies in place for members who cross over to CDM from other parties?, etc.

On more than one occasion, Zitto Kabwe has maintained a stance which was different from the mainstream thinking of CDM officials. But Zitto is still a member, and a good member at that, of CDM.

Lets not prejudge Shibuda. Time will tell and the truth is bound to come out soon or later; that is whether Shibuda is really committed to the cause that CDM has embarked on.
 
Nimeipenda hii Comment from one of Mwananchi Newspaper readers:

SILAHA MOJA KUBWA YA USHINDI WA CCM NI UPANA WA DEMOKRASI KATIKA CHAMA CHENYEWE,WATANZ ANIA SIO [NENO BAYA],CUF IMEPOTEZA NGUVU KWA KUKANDAMIZA DEMOKRASI NDANI YA CHAMA CHENYEWE WAGOMBEA URAISI WA CUFU WATAENDELEA KUWA WALEWALE JAPO WANAJUA HAWANA JIPYA LAKINI WATAENDELEA MPAKA WAFE.CHADEMA WAPI CHACHA JAH MAN,WAPI KAFULILA UTARATIBU GANI ULITUMIKA KUWAPATA WABUGE WA KUTEULIWA,TUMEO NA ORODHA YA WALIOMBA WENGI NI WAKE AMA JAMAA WA VIONGOZI WA JUU WA CHADEMA,KWANGU BINAFSI UONGOZI WA JUU WA CHADEMA HAUSTAHILI KUONGOZA CHAMA KIKUBWA CHA UPINZANI KAMA CHADEMA NA HILI KWAKUWA NAWAJUA BINAFSI NI WATU WA AINA GANI AMINI WANA CHADEMA MTASHANGAA KITAKAVYO POROMKA UMAARUFU KABLA 2015 KAMA KITAENDELEA NA TABIA HIYO YA UDIKTETA JE HAWA WAKISHIKA MADARAKA JESHI LAO,POLISI YAO,TAKUKURU YAO WIZARA YA BIASHARA YAO,KWELI WATASIKIA MAONI YA WANANCHI.SHIBUDA YUKO HIVYO ATA ALIPOKUWA CCM MARANGAPI ALITOA HOJA ZINAZO PINGANA NA CHAMA CHAKE NA HAKUTIKISIWA VICHWA NA KIONGOZI WAKE KIONGOZI MAKINI HAWEZI KUONYESHA ANAPINGANA NA MBUNGE WAKE HATA KABLA HAJAMALIZA HOJA.CHADEMA IMEKAA KI NGO ZAIDI MWANA DEMOKRASI WA KWELI HAWEZI KUKAA PALE.
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.

wasukuma sio wajinga kiasi hicho unachofikiria wewe na wala hawadanganyiki na kwa taarifa yako hakuna watu wenye msimamo kama wasukuma wakikupenda wamekepend na wakikuchukia wamekuchukia jumla kwa sasa wameshaichukia ccm na hawatorudi nyuma. Nadhani ni wakati wa kumtimua shibuda na kumsimamisha dr slaa agombee jimbo hilo.
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.
Bata kasoro manyoya we.
 
Nadhani shibuda yuko sasa. Anastahili kuheshimiwa kwa mawazo yake. Cdm wajifunze nini maana ya demokrasia. Mie nakubaliana naye kuwa posho za wabunge ni kidogo, lakini ningempongeza kama angeishauri serikali jinsi ya kuongeza mapato ili angalau hata kima cha chini kingekuwa milioni moja, mbunge angepata hata 20m si tatizo. Hoja ya cdm kupunguza posho haina mashiko kwani kwa kipato cha wananchi wengi wanalazimika kutafuta njia nyingi. Maisha bora si kupunguza kipato. Huu mjadala ni mpana, na kila mmoja atoe maoni yake, asifukuzwe mtu. Wajifunze kutoka ccm, hawafukuzani kwa hoja, vinginevyo leo hii mwakyembe, sitta, kilango, sendeka , n.k wangekuwa nje.
 
when i joined this forum,JUST YESTERDAY, I made a promise not to argue with NON THINKERS, unfortunately I couldn't resist lol - I didn't know that WASUKUMA are from the SOUTHERN Tanzania(and this explains all about your void, i think i have to go back to school!!!My Prof. used to tell me never discuss anything with fools as they will let you fly low where they used to and eventually they'll defeat you with their flying low experience, absit iniuria verbis Mr. Ritz!!! My Prof didnt know that some fools do not fly at all and Ritz is a living example!!!I apologize to my mind for engaging in this useless conversation with a far useless person like Ritz!!!!
Thanks mkuu heshima mbele.
 
Mjadala huu umeongea makosa makubwa ya Shibuda kuwa: Hana ushirikiano wa pamoja na wenzake, he is not well informed of what is going on in CDM, Anatoa msimamo tofauti na chama chake, ni CCM akifanya upelelezi CDM, Hahudhurii vikao vya chama/wabunge wenzake na anabwabwaja nje tu


Ambacho sikukiona na hoja muhimu aliyoisema shibuda katika habari kuu kwamba….
- Atashangaa sana na hatarajii kama CDM kuna viongozi wanaweza kudidimiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni huru, wakati chama kinafanya maandamano kutoa maoni huru kwa Watanzania. Kama yeye hatakiwi kufanya hivyo, basi nini maana ya kuandamana kutoa maoni kwa Watanzania".
- Mbunge anapozungumza bungeni anasema kwa maana pana kwa watu wenye mitazamo tofauti kwa lengo la kuleta fikra endelevu".
- Hana habari kama wabunge wote wa Chadema walikutana na kukubaliana kuikataa posho.

Nikiongelea highlights hapo juu, Moja: Je Demokrasia inayopiganiwa na CDM ni ile ya uamuzi wa (Chama) wa pamoja au ile ya mtu kuwa huru kutoa mawazo kwenye mambo yanayoathiri maisha yake? Pili: Je Shibuda ni mbunge wa Maswa kupitia CDM au mbunge wa CDM kupitia kupitia wilaya ya Maswa; Tatu: Je ni wabunge wote walikaa wakakubaliana kwenye hili, na kwa nini liwe hili tu la ‘posho’ na isiongezwe na mishahara ya wabunge kama ilivyoainishwa katika ilani ya CDM ya mwaka 2010.

Swali la mwisho kwa mwenye kufikiri: Je kabla ya kumsajili Shibuda kuwa mchezaji wa CDM kuna sehemu yoyote iliyomtaka abadilishe misimamo yake ambayo ilifahamika sana toka alipokuwa jumuia ya wazazi? Labda kikubwa ni kwa CDM kuwa na orodha ya watu ambao ingependa wajiunge na chama chao ili kuepuka migongano iliyowahi kujitokeza kuanzia kwa kina Wangwe (RIP), Zito, Kafulila, na sasa Shibuda. Na ili hilo lifanikiwe itabidi wapate watu wenye sifa kuu ya kudumisha fikra sahihi za ‘kidemokrasia’ za Mwenyekiti na Katibu wa CDM.

hapa kuna kazi kubwa wamfukuze Shibuna na wale madiwani wa Arusha siyo kazi ndogo hiyo. lakini last time walimsamehe Zitto nadhani na hawa watasamehewa
 
[h=3][/h]

SIKU moja baada ya uongozi wa CHADEMA na Kambi ya Upinzania kuahidi kumshughulikia Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA), Bw. John Shibuda kwa
kutofautiana wazi na msimamo na sera yao, yeye amesema kuwa yuko tayari kuhojiwa iwapo kama atatakiwa kufanya hivyo lakini akasisitiza kuwa hakupingana na sera wala ilani ya chama hicho.

Alisema kuwa alichokifanya bungeni cha kuiomba serikali kuongeza posho hiyo, ilikuwa na maana ya kumsaidia mbunge 'maslahi ya jamii wa chama jamii' ambaye lengo lake ni kuwatumikia wananchi kwa muda wowote na kwa shida yoyote.

Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu, akiwa mjini hapa, Bw. Shibuda alisema pamoja na msimamo wake kuonekana kuwakera baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu wa chama, hawezi kubadili msimamo au mtazamo wake kwa kuwa yuko sahihi kwa alichokifanya.

Alisema kuwa anasikitikika kuona chama kama CHADEMA ambacho ndio tegemeo kubwa kwa wananchi kutokana na namna kinavyotetea maslahi ya wananchi kuona hakiishi migongano.

“Nawasubiri waniite, nikiitwa nitakwenda kuhojiwa lakini natoa tahadhari kwamba hao ambao wamezungumza katika vyombo vya habari vya leo (jana) wasishiriki katika vikao vya kunihoji kwa kuwa tayari wamepoteza sifa ya kufanya hivyo,” alisema.

“Mbowe na Zitto ambao tayari wamenihukumu hawana sifa za kunihoji kwa sababu tayari wameshanihukumu, ila nasema baada ya kunihoji nitakwenda kwa Watanzania, nitakwenda kwa wananchi wa Maswa kuwaeleza mtazamo wangu na ukweli wa msimamo nilioutoa bungeni.

“Nitakwenda kufafanua mchango wangu 'mbunge masilahi ya jamii ambaye hafungi simu na ambaye anashiriki mambo mengi, mimi ni kiongozi kiyoyozi kwa wananchi kwa kuwa nashiriki kila jambo la wananchi na shida zao,” alisema Shibuda.

Pamoja na hayo mbunge huyo alisema hana ugomvi na mtu yeyote wakiwamo wanachama wa CHADEMA kwa sababu kukosana kwa askofu au kukosana ma shekhe siyo kukosana na msahafu au biblia.

Alisema kuwa, siku zote ukweli hauogopi mahakama wala polisi kwa sababu ukweli haubadiliki kwa ukaidi wa unyapara wa mtu yeyote bali ukweli utabaki kuwa ukweli siku zote.

Alisema kuwa anatarajia kufanya mikutano ya hadhara na kueleza ukweli wa hoja yake ili wananchi wajue ukweli wa suala hilo.

Kutokana na hali hiyo, aliwaomba wananchi na wanachama kwa ujumla kutulia katika kipindi hiki kwa kuwa yeye ni mtu anayesimamia uwazi na ukweli na kamwe hatafunika ukweli kwa maslahi ya wachache.

“Umaskini wa cheo si ufukara wa hekima, hivyo wasitugandamize kwa vyeo walivyonavyo…nimejifunza mengi na ninajua nilichokifanya,” alisema Bw. Shibuda.

Source:Majira
 
Kwa hili naona sasa viongozi wa CHADEMA watajifunza kwamba kuna umuhimu kuwachunguza kwa makini watu wanaotaka kuwapa dhamana ndani ya chama. Huyu jamaa alishakuwa wa hovyohovyo tangu bado yupo magamba na wasipomdhibiti mapema ataleta shida nyingi sana huko mbele. Mimi binafsi simpendi mtu huyu!
 
Back
Top Bottom