Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

1. Ni vizuri Shibuda apate nafasi kueleza CHADEMA ndani ya uongozi kukoje.

2. Nilishawaambia CHADEMA kitambo hapa, kabla hata ya uchaguzi, kwamba huyu Shbuda atawaharibia chama, anachotaka yeye ni fahari ya uongozi tu bila kujali chama, nikaonya CHADEMA wasikimbilie kumpa uongozi.

Sasa inakuwa habari ya sikio la kufa halisikii dawa na majuto mjukuu.

I hate to say I told you so, but I told you so.


Nakumbuka sana na kuna watu walikupinga!
 
Nilipoona title nilishituka kweli. Lakini nilipoangalia chini na kukuta source ni mtanzania, hata habari yenyewe sijaisoma.

Siwezi kuweka pazia kiasi hiki, maana kuna habari nyingi nzuri tu katika magezeti yetu, hoja ya kwamba linamilikiwa na fulani basi sitasoma gazeti hilo si mtazamo wangu. Hatuna chuki na mtu ila tunachukia matendo au kauli mbaya ya mtu.
 
Shibuda mbio zake ni ulaji bungeni si itikadi ambazo wengi wa wabunge wa Chadema wanazo.
Shibuda anaangalia nini anatia mfukoni leo, kesho hana habari, ndo maama ameshupa kama kenge mkubwa aliyepo mawindoni.
 
Shibuda anakubalika sana kwao, hata akiwa mgombea binafsi atapata tu ubunge ndio maana haogopi kufukuzwa na magwanda
 
Hakuna ubishi Shibuda ni wa kufukuza kutoka Chadema, lakini kuna habari ambazo nimezipata kuwa Shibuda ameshaahidiwa na uongozi wa juu wa CCM kuwa awe free kufanya chochote kwani wamemhakikishia hata Chadema ikitaka kumfukuza watatumia influence yao kwenye vyombo vyo dola na mahakama ili wasifikie hilo lengo....Wamemwahidi wana uhakika wa kumlinda mpaka 2015 utakapofanyika uchaguzi mwingine
Mimi nadhani atawahangaisha sana Chadema.... wasipofanya mambo kwa kisayansi. Wamfukuze lakini plan ya hali ya juu itumike, japo nina hakika watakutana na vikwazo vingi.
 
For shibuda this is expected . Its just a matter of when not if.
 
Tangu Mheshi,iwa atoke CCM kuja Chadema, wananchi wa jimbo lake wamepata ubunifu wowote alioutoa kwa kusaidia jimbo lake? Shule za kata hazina maabara na maji ya bomba, vyoo vya kuflush kama vya kwenye mjengo hakuna, almasi Shy kibao , lakini faida ya hiyo haijengi hata nyumba ya mwalimu. Shibuda atueleze sisi wasukuma wenziye ana uxhungu gani wa kutuletea maendeleo? Pamba tunayo lakini hata viwanda vidogo vya handlooms Shy hakuna, viwanda visivyoyumia umeme. Naona alihama CCM kwa ajili ya manufaa yake binafsi. Tuambie Wasukuma una mpango gsni wa maendeleo kwenye jimbo letu? Wisdom starts at Home.
 
Shibuda anakubalika sana kwao, hata akiwa mgombea binafsi atapata tu ubunge ndio maana haogopi kufukuzwa na magwanda

Mkuuu hi ni siasa za zamani unadhani wannachi wanaokufa kwa kuosa dawa Huko maswa wakisikia anateteta posho za ajabu ataendelea kukubalika. Bora aongelee hayo madhambi ya mbowe na Zitti hilo la "posho" litammaliza kwenye ramani ya CCM.
 
Tangu Mheshi,iwa atoke CCM kuja Chadema, wananchi wa jimbo lake wamepata ubunifu wowote alioutoa kwa kusaidia jimbo lake? Shule za kata hazina maabara na maji ya bomba, vyoo vya kuflush kama vya kwenye mjengo hakuna, almasi Shy kibao , lakini faida ya hiyo haijengi hata nyumba ya mwalimu. Shibuda atueleze sisi wasukuma wenziye ana uchungu gani wa kutuletea maendeleo? Pamba tunayo lakini hata viwanda vidogo vya handlooms Shy hakuna, viwanda visivyoyumia umeme. Naona alihama CCM kwa ajili ya manufaa yake binafsi. Tuambie Wasukuma una mpango gani wa maendeleo kwenye jimbo letu? Wisdom starts at Home.
 
Hivi huyo shibuda ni mtu?Mi nadhani ni dinosaur hivyo sina chakuchangia dhidi ya kiumbe cha ajabu
 
1. Ni vizuri Shibuda apate nafasi kueleza CHADEMA ndani ya uongozi kukoje.

2. Nilishawaambia CHADEMA kitambo hapa, kabla hata ya uchaguzi, kwamba huyu Shbuda atawaharibia chama, anachotaka yeye ni fahari ya uongozi tu bila kujali chama, nikaonya CHADEMA wasikimbilie kumpa uongozi.

Sasa inakuwa habari ya sikio la kufa halisikii dawa na majuto mjukuu.

I hate to say I told you so, but I told you so.

Hayo ni maono yako, mimi msukuma sijapendezeshwa na hayo, let Chacha rest in peace is a hero. Shibuda tangu yup ccm , sasa Chadema amesaidia nini jimboni kwake? plant ya kutengeneza au kuvuna maji kwa njia ya hewa itakayo sambaza kwenye kaya 190 inagharimu usd 3,000 na ya maji ya kuchimba kisha yavutwe kweny reseivoir inagharimu usd 5,800 ,ya uwezo wa kupeleka kwenye kaya 300. Kwa nini asishughulike na haya ambayo yatfanya zahanati za vijiji, shule za kata kuwa na maji ya bomba na salama?
 
hakuna ubishi shibuda ni wa kufukuza kutoka chadema, lakini kuna habari ambazo nimezipata kuwa shibuda ameshaahidiwa na uongozi wa juu wa ccm kuwa awe free kufanya chochote kwani wamemhakikishia hata chadema ikitaka kumfukuza watatumia influence yao kwenye vyombo vyo dola na mahakama ili wasifikie hilo lengo....wamemwahidi wana uhakika wa kumlinda mpaka 2015 utakapofanyika uchaguzi mwingine
mimi nadhani atawahangaisha sana chadema.... Wasipofanya mambo kwa kisayansi. Wamfukuze lakini plan ya hali ya juu itumike, japo nina hakika watakutana na vikwazo vingi.
lengo lake hilo? Wasukuma tuko shidani. Tunauzwa na wasukuma wenzetu kazi kweli kweli
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.

Acha ukabila, jadili hoja
 
Hayo ni maono yako, mimi msukuma sijapendezeshwa na hayo, let Chacha rest in peace is a hero. Shibuda tangu yup ccm , sasa Chadema amesaidia nini jimboni kwake? plant ya kutengeneza au kuvuna maji kwa njia ya hewa itakayo sambaza kwenye kaya 190 inagharimu usd 3,000 na ya maji ya kuchimba kisha yavutwe kweny reseivoir inagharimu usd 5,800 ,ya uwezo wa kupeleka kwenye kaya 300. Kwa nini asishughulike na haya ambayo yatfanya zahanati za vijiji, shule za kata kuwa na maji ya bomba na salama?

Hujapendezwa na nini sasa? Kwamba Shibuda anataka kutumia haki yake ya kikatiba kusema anachoona kibaya katika uongozi wa CHADEMA?

Au hujapendezwa na ukweli kwamba niliwaonya CHADEMA kwamba huyu Shibuda ni timebomb lililokuwa linangojea kulipuka wakati wowote ?

Ukiangalia swala hili kama tofauti na juhudi za kupeleka maendeleo kwa wananchi unakuwa unakosea. Kupeleka maendeleo kwa wananchi kunachangiwa sana na uongozi bora. Uongozi bora unachangiwa sana na uwazi kama huu anaotaka kutuonyesha Shibuda ( kama ana hoja makini, maana mpaka sasa ana equal chances za kuwa na hoja makini as well as political bullcrap ).

Swala langu la kwanza hapo juu lilikuwa ku point out kwamba nafurahi Shibuda anataka kuanika uongozi wa juu wa CHADEMA ulivyo. Ingawa Shibuda ana credibility ndogo, na wengine wamemuita "malaya wa kisiasa", lakini watu wote walio reasonable hawawezi kutaka kum dismiss kabla ya kusikiliza story yake ikoje. Kwa hiyo swala la kwamba Shibuda anataka kuongea dukuduku lake ni jambo zuri, kama CHADEMA wana rebuttal na wao wana nafasi ya kusema tiutawasikiliza wote na kuamua.

Swala la pili, kwamba Shibuda atakuja kuwapa matatizo CHADEMA ni jambo nililoliona tangu mwanzo kwa kumsoma Shibuda. Lakini hili halina maana kwamba hata kama Shibuda ana a valid case ku present kwa watu tumpuuze tu. CHADEMA sio saints, wanachemsha mambo mengi tu, na kama itabidi Shibuda aonyeshe ubaya wa CHADEMA kwa wananchi, so be it.

Nasimama pale pale.

Nimefurahi Shibuda anataka kuongea ili wananchi waweze kupata nafasi ya kuamua kama ana makapi au nafaka. Why, watanzania si wajinga, kama anataka kuleta uzushi mambo yata backfire na watu watamuona mzushi tu anayehangaika kuanzisha mizozo kila chama anachoenda. Akiwa na point wananchi watamshukuru kwa kukimulika CHADEMA. Hapa kuna watu tunajaribu kuwa objective bila kujali jina la mtu wala chama, lete hoja tuzisikilize na ku judge on the merit.

Nilishawaambia muda mrefu kwamba Shibuda hana interests na chama, ana interest na ukubwa.

Naweza kupinga hoja za Shibuda ( au kumponda kwa kukosa hoja) lakini nitatetea uhuru wake wa kikatiba wa kujieleza, na swala zima la kupeleka mambo kwa wananchi moja kwa moja.
 
Msimamo wake
Lakini Shibuda alilimbia gazeti hili jana atashangaa kama atatuhumiwa kwa maoni yake binafsi aliyoyatoa bungeni juzi juu ya kutaka wabunge waendelee kulipwa posho za vikao vya Bunge.

"Nitashangaa kama nitaitwa na kiongozi yoyote wa kambi yetu ya upinzani au Chadema kwa tuhuma za kutoa maoni yangu huru niliyoyatoa bungeni jana (juzi), hata nilipokuwa CCM nilipenda kusahihisha palipokuwa na makosa".

"Sitarajii Chadema kuna viongozi wanaweza kudidimiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, wakati chama kinafanya maandamano kutoa maoni huru kwa Watanzania. Kama mimi sitakiwi kutoa maoni huru basi hakuna maana ya kuandamana kutoa maoni kwa Watanzania".

"Tusitafute hila na visa kwa maslahi binafsi, tutambue kwamba mbunge anapozungumza bungeni anasema kwa maana pana kwa watu wenye mitazamo tofauti kwa lengo la kuleta fikra endelevu".

Alisema kwamba hana habari kama wabunge wote wa Chadema walikutana na kukubaliana kuikataa posho ya vikao vya Bunge.

Shibuda akifafanua zaidi suala hilo la posho japo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chake ilitaka kupunguza posho hizo za vikao pamoja na mshahara wa mbunge, alisema, "Ilani ya Uchaguzi ni mpango kazi wa kuendeleza programu ya chama kilichopo madarakani, kwa hiyo hivi sasa hapa bungeni bila kujali itikadi zetu wabunge tunaunganishwa na programu ya kuendeleza nchi, utawala bora na uongozi wa kuongoza fikra za Watanzania".
Add this page to your favorite Social Bookmarking websites





Sijui!! Lakini kuna ka ukweli hapa na ndio maana wakubwa wa humu (Jamii Forum) hamleti mjadala!

Nadhani John Magare Shibuda ni pandikizo baya sijapata kuona...ni bora tumfukuze CHADEMA na tuonekane hatuna Demokrasia kuliko kukaa na huyu mtu ni sumu kali sana kwa mapambano yetu...Mimi nadhani kuna mambo ambayo yanahitaji mtazamo wa kichama japokuwa huyapendi...ishu ya posho ni nzito,na hata watu nje ya siasa wameliona hilo,juzi nimemsikia Ndugu Deus M/kiti wa Jukwaa la sheria/katiba hakisemea jambo hili la posho...na limebeba hisia kali kwa watanzania wengi..sasa anapotokea mtu kwa maslahi yake binafsi na kuropoka uharo bungeni hapaswi kuvumiliwa...ni bora hafukuzwe tuonekane hatuna demokrasia kuliko kukaa na huyu mtu....ukifanya COST-BENEFIT ANALYSIS ni bora kumfukuza itakuwa ni heri kwetu...........
 
Nimefuatilia harakati za chama cha cdm tangu 1992 chini ya uongozi wa Edwin mtei, nimeshindwa kushawishika kabisa kujiunga na chama hiki, kila mwanachama anapolalamikia uongozi wa chama shutuma anazotoa utasikia chama kina ukabila, ukaskazini leo tena ameibuka shibuda anasema viongozi hawana demokrasia bali wamejaa umimi na uyeye kila siku ni migogoro, kwanza chama kilipasuka wakatoka watu wakaenda kuunda SAU, kisha ikafuatiwa kuondoka KABOUROU akafuata Akwilombe wote hawa wanalalamikia ukabila, marehemu chacha naye alipita humo humo kwenye ukabila
 
Nimefuatilia harakati za chama cha cdm tangu 1992 chini ya uongozi wa Edwin mtei, nimeshindwa kushawishika kabisa kujiunga na chama hiki, kila mwanachama anapolalamikia uongozi wa chama shutuma anazotoa utasikia chama kina ukabila, ukaskazini leo tena ameibuka shibuda anasema viongozi hawana demokrasia bali wamejaa umimi na uyeye kila siku ni migogoro, kwanza chama kilipasuka wakatoka watu wakaenda kuunda SAU, kisha ikafuatiwa kuondoka KABOUROU akafuata Akwilombe wote hawa wanalalamikia ukabila, marehemu chacha naye alipita humo humo kwenye ukabila
Baki tu kwenye magamba usitafue visingizio! Chama kipo kila kona ya nchi wewe umeaminishwa mambo ya u-kaskazini na kwa akili yako ya panzi unaamini kwamba ni kweli! Kweli ufisadi umewafunika macho!
 
shibuda hajawahi kuwa na msimamo, ni mmachinga i.e. A marching guy. Hawezi kutulia chama kimoja.
 
Swala la kulipwa Posho sio swala la Kiitikadi, ni swala linalohusu makubaliano ambayo yanaweza kuunda sheria ndani ya katiba yetu hivyo kila mmoja anaweza kuwa na mtazamo wake kwa sababu maamuzi yake yataendelea kutumika hata baada ya utawala wa JK na kila kiongozi atakayeingia atafungwa na sheria hiyo.

Kwa hiyo sioni sababu ya kumhukumu mawazo ya Shibuda ktk hili kama vile wengine wanavyotaka kuwashutumu wote waliopendekeza katiba mpya hali ni wanaCCM. Swali la kumuuliza huyu Shibuda lazima litokane na sababu zipi ambazo yeye kaziona ni muhimu kuendeleza posho hizi ambazo ni mzigo kwa wananchi walipa kodi..Tumsikilize sababu zake kisha tujenge hoja lakini sidhani kama swala hili linahusiana na kelele tunazopiga..

Ila naweza kusema kwamba kwa mawazo kama haya kunaweza kumgharimu yeye uchaguzi ujao toka ndani ya kiti cha mgombea wa Chadema ikiwa ataonekana hauziki tena kwa wananchi. Na Chadema lazima wawe makini sana itakapofikia wakati huo kwani kumweka mtu ambaye hakubaliki itakigharimu chama. Ushauri wangu kwake ni wa bure kabisa..
Mwanasiasa yeyote mpevu husimamia maslahi ya wananchi anaowawakilisha hivyo mawazo yako binafsi lazima yawe sambamba na msimamo wa wananchi unaowawakilisha - Without their support Ur doomed to fail!
 
..................Juzi waziri mkuu wa zamani Edward Lowasa aliiambia serikali na CCM kuwa wanapaswa kuchukua maamuzi magumu japo yatakuwa na maumivu makali dhidi yao................Mimi naomba uongozi wa CHADEMA uchukue maamuzi magumu kumtimua Shibuda katika chama,kwa kuonyesha dharau dhidi ya chama na kuwa kibaraka wa CCM ndani ya CDM. Hata kama maamuzi hayo yawe na madhara kwa chama chetu kwa kiasi gani..........Nawasilisha!!!
 
Back
Top Bottom