mbogo31
JF-Expert Member
- Nov 28, 2008
- 711
- 173
Jamani kumjadili Shibuda ni kupoteza muda, kwa sisi wengine tunaomfahamu wala hatutii presha, Chadema wameshamtumia shibuda kama yeye alivyoitumia chadema kurudi bungeni, ila kwa sasa aliyeshika mpini ni Chadema, kama wanaweza kumfukuza uanachama inamaana hata ubunge kakosa na kitakachotokea ni uchaguzi wa ubunge kurudiwa na ninauhakika kwa moto ulivyo sasa chadema wakisimamisha mtu anaekubalika watachukua tena jimbo hilo kwa tayari wameshajulikana huko na watu wamebadilika kiukweli, watu kama Shibuda, Mrema, Cheyo ni watu wa kuangalia tu ni wanafiki na wanaangalia maslahi yao binafsi.
Mimi naushauri uongozi makini wa Chadema kuangalia uwezekano wa kisheria kuondoa watu kama shibuda ndani ya chama, hao wapo kwa maslahi ya ccm ili kuanzisha vurugu ndani ya Chadema, au kutoa picha kwamba chadema sio shwari wakati tuliomakini tunafahamu kwamba Chadema wapo imara na wanaelekea kwenye njia sahihi.