Sheria za kikristo zinaweza kumsaidia mwanaume anayehitaji watoto bila kuchepuka baada ya kuoa mke aliethibitishwa hawezi kuzaa?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Mfano pale Arusha alikuwepo Mr Shayo mkewe alithibitishwa hawezi kuzaa, akakataa kuachwa au kuwa na mke mwenza sababu ukristo hauruhusu, nako kanisa la RC Arusha hawakuwa na cha kufanya, Mr Shayo alizeeka bila watoto mpaka umauti ukamfika.

Ikitokea umeoa mwanamke ambae kathibitika yeye hawezi kuzaa ila wewe unaweza kutunga mimba, kuna solution ipi ?
 
Mfano pale Arusha alikuwepo Mr Shayo mkewe alithibitishwa hawezi kuzaa, akakataa kuachwa au kuwa na mke mwenza, RC Arusha hawakuwa na cha kufanya mpaka umauti ukamfika hakuweza kuwa na watoto

Ikitokea umeoa mwanamke ambae kathibitika yeye hawezi kuzaa ila wewe unaweza kutunga mimba, kuna solution ipi ?
hilo linabaki kuwa la wawili sio kanisa, kanisa kazi yake kufunganisha tuu
 
kuna solution ipi ?
Sheria ya Ndoa inachukua mkondo wake kifuatacho ni Talaka na wanatoa hio Kanisa Katoriki maana Ndoa ni takwa la Kiserikali na Ndoa zote zimesajiriwa na Serekali, kwa hio ni kupeleka maelezo Parokiani kifuatacho ni hivyo mnatenganishwa unatafuta Ardhi nyingine yenye rutuba unaumwagia mbegu za mzeituni
 
Mfano pale Arusha alikuwepo Mr Shayo mkewe alithibitishwa hawezi kuzaa, akakataa kuachwa au kuwa na mke mwenza sababu ukristo hauruhusu, nako kanisa la RC Arusha hawakuwa na cha kufanya, Mr Shayo alizeeka bila watoto mpaka umauti ukamfika.

Ikitokea umeoa mwanamke ambae kathibitika yeye hawezi kuzaa ila wewe unaweza kutunga mimba, kuna solution ipi ?

Bwana we..... Usitafute faraja ya short cut, yakiwa magumu na umechoka....... MUNGU akusaidie.

Iko clear, sana, ila kuacha mke au kuzaa nje kwa sababu hiyo inaitaji moyo sana. Maana Hakupenda.
 
Sheria ya Ndoa inachukua mkondo wake kifuatacho ni Talaka na wanatoa hio Kanisa Katoriki maana Ndoa ni takwa la Kiserikali na Ndoa zote zimesajiriwa na Serekali, kwa hio ni kupeleka maelezo Parokiani kifuatacho ni hivyo mnatenganishwa unatafuta Ardhi nyingine yenye rutuba unaumwagia mbegu za mzeituni
ni hoja dhaifu sana kwa kanisa la RC kuachana sababu mke hawezi kuzaa, mtaambiwa mvumiliane kwenye shida na raha.

Solution hapo huwa ni kuchepuka (kuzini nje ya ndoa na kumsaliti mkeo)
 
Sheria ya Ndoa inachukua mkondo wake kifuatacho ni Talaka na wanatoa hio Kanisa Katoriki maana Ndoa ni takwa la Kiserikali na Ndoa zote zimesajiriwa na Serekali, kwa hio ni kupeleka maelezo Parokiani kifuatacho ni hivyo mnatenganishwa unatafuta Ardhi nyingine yenye rutuba unaumwagia mbegu za mzeituni

taratibu za kanisa haziruhusu kutoa talaka, isipokuwa kwa sababu ya zinaa tu. tena kwa ushahidi ulionyooka
 
Na mimi nina swali hapo hapo. Je kwa mwanaume mwenye shida ya uzazi mkewe anaruhusiwa kutoka nje kutafuta mtoto?
 
Wembe ni ule ule, Hali itakuwa hivyo hivyo maana hakuna kuachana mpaka kifo, nae atazeeka bila watoto kwa kiapo cha kuvumiliana kwenye shida ma raha

ni mateso
 
Aliyekuambia Ukristo una sheria ni nani?
Maana Kristo Yesu ndie mwisho wa Sheria, hizo nyingine ni propaganda za Madhehebu tu maana hata mitume wenyewe hawakuwahi zungumzia maswala ya Familia zaidi zaidi walijikita kuhubiri habari za ufalme wa Mungu yaani Injili iletayo wokovu kupitia Bwana na Mwokozi Yesu Kristo,

Hizo nyingine ni ngojera za kirumi na kigalatia!
 
Kwa technology ilivyo advance miaka hii, hakuna mwanamke asiyeweza kuzaa, labda awe alizaliwa bila uterus kabisa au kikwazo kiwe pesa. Kwa upande wa kanisa sijajua sana linaweza kusaidia vipi.
 
Back
Top Bottom