Sheria na taratibu za kuasili (Adopt) mtoto Tanzania

Nani anaweza kuasili mtoto

Ndugu au mtu yeyote anayeishi Tanzania mwenye umri wa miaka 25 na angalau mwenye miaka 21 zaidi ya mtoto anayeasiliwa; mwanamke asiyeolewa aliye raia wa Tanzania au wenza –mke na mume– waliokubaliana kumwasili mtoto kwa maslahi ya mtoto. Mahakama itabidi ijiridhishe kwamba wenzi hao wamekubaliana kumuasili mtoto.

Sheria hii inamruhusu mwanamume kutuma maombi ya kumwasili mtoto ikiwa mahakama itajiridhisha kwamba yapo mazingira maalumu yanayohalalisha utaratibu huo. Wenzi wanaoishi bila kuwa na ndoa inayotambulika kisheria hawawezi kukubaliwa kuendelea na utaratibu wa kumuasili mtoto. Ndio kusema watu wanaoishi kinyumba bila kuwa na ndoa hawawezi kuasili mtoto.

Hata hivyo, ili maombi yoyote ya kumuasili mtoto yakubalike, lazime mwombaji awe ameishi na mtoto husika kwa angalau miezi sita mfululizo kabla ya tarehe ya maombi husika.

Mwombaji asiye raia wa Tanzania anaweza kuasili mtoto ikiwa ameishi Tanzania kwa angalau miaka mitatu mfululizo; amemlea mtoto kwa angalau miezi mitatu chini ya uangalizi wa afisa ustawi wa jamii; hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai na mahakama ya nchini kwake inaheshimu na kutambua maombi yake.

Utaratibu wa kufuata

Sheria ya Mtoto inaelekeza kwamba maombi ya kuasili mtoto yatatumwa Mahakama Kuu baada ya kupata ridhaa ya mlezi au mzazi wa kumzaa mtoto. Mahakama itajiridhisha ikiwa mlezi au mzazi wa mtoto husika anaelewa matokeo ya mwanawe kuasiliwa na ikiwa kweli ameshindwa kumtunza mtoto au amekuwa na tabia ya kumnyanyasa mtoto.

Katika mazingira ambayo mzazi au mlezi hana uwezo wa kutoa ridhaa mahakama lazima ijiridhirishe kuwa utaratibu wa kumuasili mtoto unazingatia maslahi ya mtoto na kwamba matakwa ya mtoto yamezingatiwa. Kwa mtoto mwenye umri wa angalau miaka 14 lazima ridhaa yake izingatiwe isipokuwa kama mtoto hana uwezo wa kujieleza.

Katika maombi ya kuasili mtoto, taarifa zifuatazo zitahitajika. Tarehe na mahali alikozaliwa mtoto; jina, jinsia na jina la ukoo la mtoto kabla na baada ya kuasiliwa; jina, jina la ukoo, anuani, mahali pa kuzaliwa, mahali anapoishi, uraia na kazi ya mzazi anayemuasili mtoto.

Wakati utaratibu wa kuasiliwa mtoto ukiendelea kufanyiwa kazi, mtoto atakuwa chini ya uangalizi wa afisa ustawi wa jamii na hatasafirishwa nje ya nchi bila ruhusa ya mahakama.
 
Umenipa mwangaza, Asante mkuu
 
watu humu ndani sijui mna mawazo ya aina gani?????????

muhusika amesema ana taka ku adopt mtoto,
huyo mtoto awe wake kisheria na
sio suala la kulea watoto wa ndugu na kuwapa matunzo

as if mnajua kuwa halei watoto wa ndugu,???????

watoto wa ndugu hata uwafanyie nini watabaki kuwa watoto wa ndugu......

suala hapa ni ku adopt kitu ambacho ni kizuri na tunatakiwa kumuunga mkono.........

Cheusi,,,,
ushauri wangu ni kuwa usife moyo.........
wengi tungekuwa na mawazo kama yako
watoto wengi wasinge teseka.

nenda adopt hata wawili.....
kweli kabisa ingawa imepita miaka mingi ila acha nichangie tu ivyo ivyo🤗🤗
 
Kweli huna ndugu huko Tanganyika wa kuweza kuchukua mtoto umlee? au mnataka misifa mbele za watu!
Nafikiri hujui sababu za watu kuadapti mtoto,

Nikupe sababu moja tu ya msingi,

Kuadapti mtoto ni kumfanya mtoto asiye wako kuanza kumiliki,Kuwa WAKWAKO ,Ataitwa kwa majina yako.Atarithi mali zako.

Na yeye atakutana ndiye mzazi wake.Ukizeeka atakutunza kama wafanyavyo watoto wengine kwa wazazi wao.

Sasa wewe unamwambia akachukua mtoto wa ndugu yake amsomeshe ili hali hawezi kuwa na mamlaka naye ya ama kumuozesha au hata kumtangaza mbele za watu huyu ni mwanangu na siyo kusema huyu ni mtoto wa fulani umeona utofauti hapo?Acha kuwa na Kebehi kama wewe siyo tasa shukuru Mungu.Ukisikia watu wanatafuta watoto kwa udi na uvumba na hawapati mwisho wa siku wanafanya kuadapti kama huyu.

Zipo sababu zinazowafanya watu kuadapti watoto mojawapo ni ugumba au tasa, Au kutaka mtoto wa jinsia nyingine,Au kutaka kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
 
Nina wasiwasi na hizi fikra zako cheusi!
Sidhani kama ni sahii unless Cheusi wewe si muafrika.
Coz ninaamini uko na ndugu zako wengi masikini wengine hawana hata pakuishi, wanaumasikini mkubwa tuu wa kutosha kuwasaidia wanyanyuke.
Mbona haya mamboya kuadopt kids from other families in Africa bado sana, predicted may be in africa (Tanzania in particular) they can start for 200 years to come or more than that, of which I believe it is not in your generation.
Your clan net worth iko vipi cheusi, work it out a little bit and understand your responsibilities in a family and your clan before you go into other families business cheusi wee.
Acha kuigiza maisha yako.

"LIFE IS CHOICE LIVE IT" Tehe he heeeee....
Adoption is very African. Only that we adopt kids from our own relatives and help them to the highest, without claiming them to be ours or changing their names to ours.
 
watu humu ndani sijui mna mawazo ya aina gani?????????

muhusika amesema ana taka ku adopt mtoto,
huyo mtoto awe wake kisheria na
sio suala la kulea watoto wa ndugu na kuwapa matunzo

as if mnajua kuwa halei watoto wa ndugu,???????

watoto wa ndugu hata uwafanyie nini watabaki kuwa watoto wa ndugu......

suala hapa ni ku adopt kitu ambacho ni kizuri na tunatakiwa kumuunga mkono.........

Cheusi,,,,
ushauri wangu ni kuwa usife moyo.........
wengi tungekuwa na mawazo kama yako
watoto wengi wasinge teseka.

nenda adopt hata wawili.....
Mimi mwenyewe nina mpango wa ku adopt mtoto wa kike. Nibaishi na ndugu na nimekuwa nikiwasaidia kwa miaka 10 sasa, . Hawa watoto wa ndugu wakishajitegemea mara nyingi hawana habari na wewe. Nimeshaona kwa watu wengi. Mwisho wa siku unabaki mwenyewe kama hukujaaliwa mtoto.
 
Bila ndoa haiwezekani kabisaa? Wengine hatujaolewa tunatamani kuadopt hapo ndo hatuna nafasi au kuna namna nyingine?
 
Back
Top Bottom