Sheria na taratibu za kuasili (Adopt) mtoto Tanzania

Masika

Masika

JF-Expert Member
Sep 18, 2009
725
195
Dada cheu, unataka kuleta fujo jamvini au una maanisha! niadopt mimi please, nataka kwenda shule mambo hayajakaa vizuri ni pm please
 
father-xmas

father-xmas

JF-Expert Member
Mar 23, 2010
530
0
cheusi usikatishwe moyo mamaa......timiza ndoto yako na mimi nakupigia makofi kabisa kwa hilo.....sijui watu wakoje yaani wanataka kina madonna watuchukulie madogo zetu lkn akisema cheusi maneno yanakuwa meeengi.....Mungu atakubariki sana kwa moyo wako huo mama.....,huwezi jua mibaraka itakayomiminika nyumbani kwako kwakujitolea kumlea huyo yatima......!safi sana onyesha mfano!
..........ila cheuthi eeh natamáni ningekuwa ntoto uniadopt mimi maana kila saa ningekua nalilia unibebe hapo mgongoni.......!
 
cheusimangala

cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,586
0
The Boss,
asante kaka yangu kwa maneno mazuri!
 
cheusimangala

cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,586
0
Akili Kichwani,
hahaa unajua akili kichwani pamoja na vijembe vyako ulivyonipiga siachi kukupenda kaka yangu wewe sbb huwa unaongea vitu vinavyonichekesha sana,kama hapa nimecheka sana ujue!

hata hivyo mimi ni mimi huwa nikiamua kitu changu hakuna maneno matamu wala machungu kutoka kwa mtu yatakayofanya nibadili msimamo wangu kirahisi! nita-adopt mtoto na hivyo ndivyo itakavyokuwa,period!

mimi sio tajiri wala ukoo wangu sio matajiri,lkn hivyo ndivyo nilivyoamua kuspend kidogo changu alichonibariki mungu,sihitaji kujielza sana ili nielewekee as long as sijasema nataka kuipindua nchi,hivyo kwa vile ninachotaka kufanya ni kitu halali basi nipeni maelzo yatakayosaidia kutimiza lengo langu na sio porojo ndeeeeefu za sijui sungura kambaka fisi huku jogooo akishuhudia!

hamuwezi kujua ni kitu gani kimenisukuma kufanya hivi, hivyo msianze kunitajia sijui nisaidie watoto wa ndugu zangu, je kama na mimi ni yatima sina ndugu nilikulia vichochoroni bila msaada wa mtu mpaka nikafika hapa nilipo mwenyewe mtajuaje?

hakuna mwanamke anayeogopa kuzaa sbb kuzaa ndio uanamke wenyewe! ninachotaka mimi ni mtoto mdogo asiye na wazazi na wala sina uwezo wakusaidia mtu mzima kusoma sijui ,maana hata mimi sikusaidiwa na mtu kusoma nilifight kivyangu!

---hata mkinisema sibadili msimamo wangu ng'oo na habari ndio hiyo cheusi is soon going to be in love with a cute angelic baby from anaza maza,na akikua kidogo nitaadopt mwingine na mwingine hadi roho yangu itakaporidhika!

nyie pesa zenu mkitaka kunywea gongo na wanzuki au kuhonga machangudoa kinondoni makaburi au kujinunulia magari ya kifahari na nguo kutoka marekani kwa calvin clain na arman ni uamuzi wenu mimi zangu nimeamua kuzitumbua kwa mtindo huu!

no words will stop me my kakaz,nimeshaamua imebaki utekelezaji tu!
 
queenkami

queenkami

JF-Expert Member
Feb 8, 2010
1,346
2,000
Nimeumia sana kuona jinsi watu wanavyomrushia cheusi maneno makali ilhali jambo analotaka kufanya ni zuri sana na la kupigiwa mfano.

nimefurahi kuona cheusi hujayumbishwa na maneno!!!hata biblia inasisitiza tuwajali yatima!!!
Cheusi tafadhali usibadili mwendo huo hakikisha unatimiza lengo lako na milango ya mibaraka itafunguliwa na utasaidia wengi zaidi na zaidi!

Mungu aliye juu akubariki sana mpendwa cheusi nyota yako ing'ae hata iweze kuleta mwanga ktk maisha ya yatima wengi zaidi!

tuna kikundi chetu maalum cha maombi nakuahidi niwaambia tufanye maombi maalum kwa ajili yako!!
 
M

Mama Joe

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,505
1,225
Hongera mdogoangu kwa wazo jema. Hata mtu ukizaa yatima ni muhimu wachukuliwe na kulelewa ktk familia ambapo watapata upendo na attention kama binadamu wengine. Sio uzungu, mbona wako watu wengi tu nchini wanafanya hivo?

Nenda Uhuru hostel, Moshi watakupa maelezo ya Amani children watakupa details ya mtoto mmoja mmoja. Msimbazi centre hapa Dar pia wanao. Ukiishamchagua unapewa maelezo uende wapi kukamilisha zoezi. Kumbuka mtoto wanapewa mume na mke na wanakuja ustawi wa jamii kumuangalia ktk kipindi maalumu kuona unamleaje.

Waweza google Amani children watakupa maelezo otherwise pm nikupe contacts zao. Blessings.
 
bht

bht

JF-Expert Member
May 14, 2009
10,336
1,250
Cheusi nimeufurahia msimamo wako

aftaroo wazo lako limebarikiwa sioni tatizo la kuyumbishwa na vijineno vya watu amabao nahisi hawana uhakika na dhamira yako

pamoja shostito tena kwa maelezo zaidi au ukikwama plz PM me ntakupeleka mpaka kwa advocate anayefanaya hizi process and ge will be more than happy to assist you in the process!!
 
B

Babuyao

JF-Expert Member
Jun 6, 2009
1,731
1,250
cheusimangala,
Cheusi, umeongea sana mama. Maneno yako yameuchoma sana moyo wangu mpaka kilindini kabisa. Tungepata watu wachache wenye moyo huu naamini vituo vya kulelea yatima vingebaki na watoto wachache mayatima. Umenigusa sana kwa kweli.

Tusisubiri wazungu waje kuasili watoto w tz kana kwamba watz hatupo kabisa. Mimi nakutakia safari njema ya adoption. Mungu abariki nia yako na mipango yako.

Mi sijui sana utaratibu wa adoption lakini ninachojua kuna kupitia katika Wizara inayoshughulika na mambo ya jamii. Hao watakupa mwongozo wa kisheria.
 
Nkamangi

Nkamangi

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
642
0
Cheusimangala wanawake wote tungeweza kusimamia maamuzi yetu kama wewe mbona tungefika mbali!!
Sio kuwa bendera trying to please every tom dick, harry, mwanahamisi, neema, mwajuma and haruna.
 
Original Pastor

Original Pastor

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
1,269
1,195
Mimi katika Kanisa langu wapo wengi watoto njoo tukupe mwanga
 
R

Realist

Member
Dec 11, 2006
90
95
Cheusimangala; Je ulifanikiwa kuasili mtoto? hebu tujuze taratibu zikoje . . .
 
Tulizo

Tulizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
849
225
Imekuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu ku-adopt mtoto yatima awe wangu kabisa nimlee,kumsomesha na kumfanyia yote anayostahili kufanyiwa mtoto!
Nilikuwa natafuta Mtu Mwenye mawazo Kama hayo..ili nimrudishie Mungu yote aliyonifanyia ...
 
autorun255

autorun255

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
1,110
0
Niajeee wadau wa jamvi.

Niomba kujulishwa kuhusu sheria za tanzania je zinaruhusu kuasili/adopt mtoto/watoto??

Nimekuwa nikiskia wadhungu hasa hasa mastaa wanapenda kuasili watoto kutoka africa na nchi nyingine.

Inashangaza sijawahi kuskia mtoto kuasiliwa/ adopt hapa tanzani.
Je sheria haziruhusu!!??
Au mitoto ya kibongo ni balaa??

Maana watoto wanazidi kujaa mitaani.

Huenda kama hili lingefanyika hapa nchini watoto wa mitaani wangepungua.

Ni mtazamo wangu.
Karibuni tujadili...
 
Burungutu la pesa

Burungutu la pesa

Senior Member
Feb 21, 2015
117
195
ndugu wana jamvi nahitaji mtoto yatima wa kulea ila sijui process za kumpata na kukabidhiwa ili ni mhudumie. naomba yeyote mwenye ukaribu na suala hili anisaidie hatua za kufuata na mahali sahihi pa kuanzia na ikiwezekana naomba hata mawasiliano ya kituo chochote cha kulea watoto yatima.
 
Zamiluni Zamiluni

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
11,541
2,000
God Bless you......
 
Zanzibar Spices

Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,413
2,000
Mkuu inaonekana nyumba za Ibada huendi wewe.
Kila kanisa au msikiti basi ukiwauliza wanajua nyumba za watoto yatima zilizo karibu.

Utaratibu ni kwamba uyatima una nama nyingi sana.Kuna waliofiwa na wazazi wote na kuna aliefiwa na mzazi mmoja.

Sasa aliefiwa na mzazi mmoja
nahisi sio nzuri sana kumchukua,maana akianza kupata uelekeo kunakuwa na conflict kubwa saana kutoa upande wa mzazi wake.Tena inaweza kukufanya ukajuta kumlea,maana hadi huyo mtoto anaweza kuona hujafanya kitu,au akachukia upande mmoja,na inaweza pia akakuchukia wewe pia.Maana mama yake anaweza kuwa ameolewa na mwanaume mwingine kisha akalazimisha waje wamchukue,hapo inabidi umuache.

Nakushauri tafuta mtoto aliefiwa na wazazi wote,huyu atakuwa huru zaidi na atakuona kwamba nyie ndio wazazi wake in full,licha ya kwamba atajua wazazi wake wameishafariki,ila atajua nyie ndio wazazi wake wa pili mliompa dunia na kuijua na kumsaidia,

Na ndio maana kwa Sie waislam hata wakristo kama sikosei,ni kwamba kama ukimlea yatima kama mungu anavyotaka,basi kama na wewe utakuwa mtu wa mungu,nyumba yako na maisha yako yatakuwa na baraka sana.Na huto athirika na maisha ya dunia hadi mungu atakapoamua kukupa mtihani wake tu wa kukujaribu.Neema na thawabu kwa Mungu ni kubwa saana.Ila wengi sana wanafeli ikifika hatua fulani.

Wazo:- Ila sijajua uwezo wako na hali yako,ila ningekushauri uwachukua wawili,wa kiume mmoja na wakike mmoja.

Najua hakuna ulezi mwepesi ila fanya kama ni watoto wako,na usifikirie kwamba hao ni malaika,la, hao ni binaadam na watoto kama walivyo wengine,kuna manunda,wagomvi,wadokozi,kuna watoto wamepinda kupita maelezo,ila hayo yote uyajue.

Na isije siku ukajuta kwamba unajuta kumlea mtoto yatima,ni dhambi kubwa sana kwa mungu na hata kusamehe.

Hata kama huyo mtoto atakuwa kibaka au kama ni wa kike atakuwa Malaya,tambua huo ni mtihani mungu anakupa,maana hata mwanao wa kumzaa anaweza kuwa kama hivyo.Sasa mungu anakupa mtihani huo ili kuona uwezo wako wa kupambana nahali hiyo.

Jingine,nakushauri sana,chukua mwenye umri kati ya 3 - 5yrs.

Jinsi ya kuwapata:Kwanza uwe unatambulika na kazi yako kwa ujumla,baadhi ya vituo huweka ukaguzi wa kustukiza,maana huyu mtoto lazima kituo kiwe na ushirikiano wa karibu sana na wewe,na pia kama utakuwa muungwana basi siku moja moja unampeleka aende kwa wenzie akakumbuke alipotoka ili na yeye mungu akimpa huko ukubwani,basi afanye zaidi ya umevyofanya wewe kwake.

Ustawi wa jamii pia lazima wahusishwe kwa kushirikiana na serikali za mitaa na wajumbe wake.
Na muhim zaidi tafuta mwanasheria ambae atasimamia taratibu zako,hili ni muhim saana tena saana.

Ubarikiwe kwa lengo lako.
 
The Businessman

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,421
2,000
Zanzibar Spices umeandika vuzuri, mtoa mada fata hayo maelezo.
 
Last edited by a moderator:
T

TOWASHI

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
295
195
Ubarikiwe sana kwa nia yako njema
 
124 Ali

124 Ali

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
7,516
2,000
Zanzibar Spices kaweka fasaha kila kitu na ewe ndugu yetu zamilunizamiluni Mwenyezi Mungu aitie wepesi nia yako hii njema !amin!
 
J

jae

New Member
Nov 1, 2011
4
20
Ubarikiwe sana kwa uamuzi wako, ila mi nilitaka kujua nn kimekusukuma kwa uamuzi huu?
 
Top Bottom