Sheria na taratibu za kuasili (Adopt) mtoto Tanzania

cheusimangala

cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,586
0
Imekuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu ku-adopt mtoto yatima awe wangu kabisa nimlee, kumsomesha na kumfanyia yote anayostahili kufanyiwa mtoto! Sasa naona nina uwezo na muda wa kuitimiza ndoto yangu!

hivyo naomba kujulishwa sheria na taratibu za kuasili/adopt mtoto hapa Tanzania!
Je, niende wapi kwa ajili ya kufanikisha jambo hili!

natanguliza shukrani!
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,826
0
hata mie sredi hii itanipa mwanya kidogo
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,826
0
link ulotupa imesaidia japo maelezo hayakuwa ya kutosha

ukitaka ku adopt unatakiwa wende wapi? na lazima tayari uwe ushajua unataka kum adopt nani au ukifika kwa wahusika wanakutafutia wao?
 
bht

bht

JF-Expert Member
May 14, 2009
10,336
1,250
link ulotupa imesaidia japo maelezo hayakuwa ya kutosha

ukitaka ku adopt unatakiwa wende wapi? na lazima tayari uwe ushajua unataka kum adopt nani au ukifika kwa wahusika wanakutafutia wao?
procedures huwa ni za kimahakama (nijuavyo mimi) mahakama kuu ndio wenye uwezo huo

mahakama haiwezi kukutafutia mtoto unatafuta mwenyewe au kupitia ustawi wa jamii wao wanuwezo wa kukukutanisha na wahusika wa vituo vya watoto yatima.

sasa baada ya hapo hatua za kisheria ndo zitafuata....
 
B

BeNoir

Member
May 6, 2008
97
0
Unaweza pia kujaribu kupitia kwenye baadhi ya orphanage ukapata idea ya umri wa mtoto, jinsia, n.k unayekusudia kuadopt na huenda watakufahamisha utaratibu stahili. Vilevile utapata nafasi ya kujifunza mengi ikiwa na pamoja wengine walioadopt na ushauri mwingine mwingi. Ni mawazo yangu tu.
 
K

kero

Member
Sep 23, 2008
46
0
Imekuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu ku-adopt mtoto yatima awe wangu kabisa nimlee,kumsomesha na kumfanyia yote anayostahili kufanyiwa mtoto!sasa naona nina uwezo na muda wa kuitimiza ndoto yangu!

hivyo naomba kujulishwa sheria na taratibu za kuasili/adopt mtoto hapa Tanzania!
Je niende wapi kwa ajili ya kufanikisha jambo hili!
natanguliza shukrani!
Nina wasiwasi na hizi fikra zako cheusi!
Sidhani kama ni sahii unless Cheusi wewe si muafrika.
Coz ninaamini uko na ndugu zako wengi masikini wengine hawana hata pakuishi, wanaumasikini mkubwa tuu wa kutosha kuwasaidia wanyanyuke.
Mbona haya mamboya kuadopt kids from other families in Africa bado sana, predicted may be in africa (Tanzania in particular) they can start for 200 years to come or more than that, of which I believe it is not in your generation.
Your clan net worth iko vipi cheusi, work it out a little bit and understand your responsibilities in a family and your clan before you go into other families business cheusi wee.
Acha kuigiza maisha yako.

"LIFE IS CHOICE LIVE IT" Tehe he heeeee....
 
Kwetunikwetu

Kwetunikwetu

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
1,540
1,225
Kweli huna ndugu huko Tanganyika wa kuweza kuchukua mtoto umlee? au mnataka misifa mbele za watu!
 
hujatenda dhambi kuwa na wasiwasi na fikra zangu na yote uliyoongea ni kweli lkn nisamehe tu maana sitabadili msimamo wangu niombee nifanikiwe!
 
cheusimangala

cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,586
0
Kweli huna ndugu huko Tanganyika wa kuweza kuchukua mtoto umlee? au mnataka misifa mbele za watu!
asante na mungu akubariki sana na anisamehe kwa kutaka misifa mbele ya halaiki!
 
N

Ngala

Senior Member
Sep 30, 2009
160
0
Cheusi mangala badili mwendo huo mangala eeh mangala eeh binti wa afrika. Tusimkatishe tamaa yawezekana yeye mwenyewe kashindwa kupata mtoto wa kumzaa kwa sababu yeyote ile. Kuchukua mtoto wa ndugu ni sahihi kabisa lakini ikumbukwe tu mtoto huyo atakuwa na wazazi wake na wazazi wake bado watakuwa na amri ya mwisho kwa mtoto wao jambo ambalo litamwathiri mlezi kwa kiasi kikubwa.NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI ******. na tumuulize ni chepi kimemsibu hadi kufikia uamuzi huo
 
sina matatizo yeyote ya kuzaa na siku moja nitakuja kuzaa muda utakapofika!
 
N

Ngala

Senior Member
Sep 30, 2009
160
0
sina matatizo yeyote ya kuzaa na siku moja nitakuja kuzaa muda utakapofika!
nakuombea kwa muumba akujalie wana wema wakufae na waifae jamii itakayowazunguka kikubwa wawe wacha MUNGU kama wewe japo kuna kipindi uliahidi kuiondoa AVAR yako maana ilisababisha mtaafaruku humu jamvini lakini bado umeikomalia.Mangala CHAKO NI CHAKO UKIKIONA CHA MWENZIO KITEME MATE.Ushauri wangu kwako zaa ulee damu yako kuliko kukimbilia mambo ya KIDHUUNGU. Na lau kama hupati bahati ya kuzaa si vibaya ukatekeleza uamuzi wako
 
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
39,014
2,000
watu humu ndani sijui mna mawazo ya aina gani?????????

muhusika amesema ana taka ku adopt mtoto,
huyo mtoto awe wake kisheria na
sio suala la kulea watoto wa ndugu na kuwapa matunzo

as if mnajua kuwa halei watoto wa ndugu,???????

watoto wa ndugu hata uwafanyie nini watabaki kuwa watoto wa ndugu......

suala hapa ni ku adopt kitu ambacho ni kizuri na tunatakiwa kumuunga mkono.........

Cheusi,,,,
ushauri wangu ni kuwa usife moyo.........
wengi tungekuwa na mawazo kama yako
watoto wengi wasinge teseka.

nenda adopt hata wawili.....
 
A

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
1,225
hujatenda dhambi kuwa na wasiwasi na fikra zangu na yote uliyoongea ni kweli lkn nisamehe tu maana sitabadili msimamo wangu niombee nifanikiwe!
acha kuogopa kuzaa........ kama hela imetulia zaa hadi waishe tumboni................ mambo ya kuiga kila kitu uzungu uzungu............ wao wana-adopt kwa sababu nyingi sana, kwanza baadhi ya nchi wana one-child policy sasa akiona ana uwezo wa ziada ndo anaangalia alterlatives..... tena walitaka wanalazimika kutafuta nje ya nchi zao manake ndani kila mtu ana mmojammmoja na wengi hawashindwi kutnza............ sometime, wanadopt watu wazima kama wanafunzi, wanasemina nk wanaotembelea nchi zao ili wawatendee hsani kama sehemu ya interest zao......... nk.nkn.k..... kuna mambo mengi sana hapo...........

acha kukurupuka mtoto wa kike wewe........... kwa mazingira ya tz ni ulimbukeni tu huu unaoufanya......... kaangalie watu wa ntumbani mwako uwasaidie (kumbuka maneno ya Mungu:.... yule asiyewaangalia watu wa nyumbani mwake mwenyewe, ni mbaya kuliko mtu asiyeamini...), labda kama wameisha na tumboni kwako nako hakuna kitu, naweza kufikiria wazo lako................
 
A

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
1,225
sina matatizo yeyote ya kuzaa na siku moja nitakuja kuzaa muda utakapofika!
kumbe hujazaa hata mara moja????!!!.............. basi una matatizo makubwa sana kuliko hata hayo ya kuzaa............ kawaone wataalam wa saikolojia wakupe usjauri nasaha..............

nakushauri hivi kwani hata watoto walioasisliwa wan mambo yao, wengi wamefikia hata kuwachinja wazazi wao waliowwasili baada ya kubaini si waliowazaa...... haya japo ni mambo ya kizungu, nayo ni mkanganyiko wa saikolojia tupu.......... kama unaona vipi, tafuta yatima miongoni mwa ndugu zako mtendee memea ama juilize nanai aliyewatendea mema wazazi wako ama mababu zako umtendee meme a mmoja kutoka huo ukoo kama shukrani kwa niaba yao............ ni jambo linalopendeza zaidi kama una uwezo.......... kumbuka kisa cha mfalme daudi na mlemavu wa viungo mephibosethi wa nyumba ya sauli.............. aliamua kumtendea mema kwa heshima ya rafiki yake jonathanai ambaye kwa wakati ule daudi anakuwa mfalme alikuwa no more........... angalau this can work in our society............
 
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,281
1,225
cheusi kwanini usiniadopt mimi?:behindsofa:
 
Kwetunikwetu

Kwetunikwetu

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
1,540
1,225
asante na mungu akubariki sana na anisamehe kwa kutaka misifa mbele ya halaiki!
Amina! Tupo pamoja.......Mungu akusaidie uwakumbuke ndugu zako walio maskini zaidi kuliko hao uliokuwa unawawaza wa-kuadopt
 
D

Dina

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
3,061
1,500
Mbona mimi sioni tatizo la wazo Cheusi? Mmeshafanya safari za kutembelea orphanage centers jamani mkaona watoto (wapo wachanga pia) waliopoteza wazazi wao?

Sasa kuna ubaya gani kama atatokea mtu ampatie malezi ya kudumu, kama Mwenyezi Mungu atamjalia mlezi maisha marefu? Na uzungu wa kuadopt unatoka wapi hapa?

Hao watoto wa ndugu si wana wazazi wao, hata Cheusi akiamua kuwasaidia ni kuongezea pale palipopungukiwa! Unless kama yupo huyo mtoto wa ndugu asiye na wazazi.

Na tatizo la watoto hawa akishakuwa na link na ndugu wengine, basi kutwa kucha maneno..ooh mtoto hatunzwi vizuri kwa kuwa sio wake, angekuwa wake asingefanya vile....blah blah blah....

Cheusi wala usikate tamaa, kuna watoto wengi sana wanasubiri watu wa aina yako wajitokeze. kama moyo wako unakutuma kufanya hivyo, basi na Mungu akutangulie.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom