Mwongozo wa Sheria ya kazi kwenye kukataza ajira ya mtoto, ajira ya shuruti na kupiga marufuku ubaguzi katika ajira

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Sheria imeweka kinga maalum za msingi ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa ya staha na heshima kwa kukataza ajira ya mtoto, ajira ya shuruti na kupiga marufuku ubaguzi katika ajira. Makatazo haya yanawahusu pia, Jeshi la Wananachi wa Tanzania, Polisi, Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa.

Katazo la ajira ya mtoto
Ni marufuku kuajiri mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na nne. Mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi, ambazo hazihatarishi au kuathiri afya yake, makuzi yake, mahudhurio shuleni au katika mafunzo, maadili n.k.

Hairuhusiwi kumuajiri mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na nane kufanya kazi katika migodi, viwanda na kwenye reli. Hata hivyo mtoto huyo anaweza kufanya kazi katika sehemu hizo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo chini ya usimamizi maalum.

Katazo la ajira ya shuruti
Hairuhusiwi kumshurutisha, au kumlazimisha mtu kufanya kazi pasipo ridhaa yake. Kazi za shuruti zinajumuisha pia kazi ambazo mtu hulazimika kufanya kulipia deni, kufanya akiwa amefungiwa au anazolazimika kuzifanya baada ya kupewa vitisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na kitisho cha kuadhibiwa.

Hata hivyo kazi zifuatazo sio kazi za shuruti:
(a) Kazi za kijeshi kwa mujibu wa sheria ya ulinzi wa taifa
(b) Majukumu ya kawaida ya raia
(c) Kazi katika kutekeleza hukumu au amri ya mahakama chini ya
usimamizi wa mamlaka za serikali.
(d) Kazi wakati wa hali ya hatari au majanga.
(e) Kazi za jamii ambazo jamii yenyewe wamekubaliana kidemokrasia kuzifanya.

Katazo la ubaguzi
Waajiri wanakatazwa kuwabagua wafanyakazi wao kwa namna yoyote ile kwa misingi ya rangi, utaifa, kabila au sehemu ya asili atokapo mtu, mbali, utaifa wa asili, daraja la mtu katika jamii, itikadi ya siasa au imani ya kidini, jinsi, jinsia, ujauzito, hadhi ya ndoa au majukumu ya kifamilia, umri na UKIMWI.

Unyanyasaji ni ubaguzi pia. Hata hivyo sio ubaguzi:-
(a) Kutoa upendeleo maalum kwa madhumuni ya kuleta usawa na kuondoa ubaguzi mahali pa kazi.
(b) Kumtofautisha, kumuondoa au kumpendelea mtu kutokana na mahitaji ya kazi.
(c) Kuajiri raia kwa mujibu wa sheria.

Waajiri ni lazima watengeneze mpango maalum unaoonyesha namna wanavyotoa fursa sawa na kuondoa ubaguzi mahali pa kazi na kuusajili mpango huo kwa Kamishna wa Kazi.

Ni marufuku kwa vyama vya wafanyakazi, Jumuiya za Waajiri kufanya ubaguzi katika:-
(a) Kuingiza wanachama, kuwakilisha wanachama na kusitisha uanachama;
(b) Sera na mazoea ya ajira;
(c) Makubaliano ya pamoja.
 
Kaka unaweza kuwa na Sheria ya Kazi na Ajira (Rev 2019). Kama ndio naomba ushare.
 
Mbona kwenye Majeshi ukiwa na HIV au albinism wanakataa kukuajiri,
Sheria zinasemaje hapa?
 
Back
Top Bottom