Hawa wanaofanya haya ni miongoni mwa 'law enforcers' (kama ndio hao wanaoamrisha huyo mtu afanyiwe hivyo) wanaoishushia nchi yetu heshima kimataifa kwa kujichukulia sheria mkononi maana utaratibu wa kisheria upo kama mtu anatuhumiwa kwa kosa lolote.
 
Hata kama jamaa ana makosa haifai kufanyiwa hivyo.

Kila jambo lina utaratibu wake.

Kama jamaa ana makosa ni vyema akamatwe na kupelekwa panapo stahili

Ndugu zetu au wenye vyeo wakiamua hivi je sisi wananchi wa kawaida itakuwaje

Nishauri jambo hili likemiwe na wahusika waajibishwe kwa kujibu wa sheria.

Wasallam.
 
Huyu kaonewa huruma sana.

Kweli unaenda Uhamiaji unadanganya kuwa wewe ni PCCB?

Ametapeli Wangapi kwenye taasisi za kiraia?

Piga Mbwa huyo
Si vibaya ukajielemisha utofauti wa sheria na hisia au mihemko. sijui kama unaelewa maana ya kuheshim sheria au utawala wa sheria. usione kwa mkosaji yule kwa jambo lile fikiria wewe umeoverspeed ukavuliwa nguo uchi badala ya fine. fikiri kidogo.
 
Hawa wawe wanawapiga picha hivi hivi na kuwaweka hadharani ili wajulikane na mademu wao waliodanganywa kwamba ni maafisa usalama .hii ni tosha kabisa kuliko kuongeza idadi ya mafaili mahakamani mwisho wa siku mtu ana honga mahakimu nankiachiwa.

Sidhani kama atarudia tena huo uupuzi aliokuwa anafanya.

Hapa haina kusingiziwa wala nini.

Maana huo mwili na hiyo confidence ya Kihaya pamoja na gari anayotumia,lazima akutapeli tu.
 
Hivi huwa hamuelewi mama alishasema yeye na Jiwe ni kitu kimoja huoni kiongozi wa kudai katiba mpya katekwa na wasiojulikana ? CCM ile ile chupa mpya mvinyo uleule
Screenshot_20210528-133646.png
 
Huyu jamaa aende mahakamani afungue kesi ya kulipwa fidia baada ya kudhalilishwa kinyume na sheria.

Askari wengi ni wapumbavu na wengi wao hawafahamh sheria , ni watu wasio na utu kwa watu wajinga mimi nimewapeleka mahakamani wajinga kama hawa wanapigwa faini mpaka wanalia.
 
Hawa sio wale wa tuma kwenye number hii me tapeli siwezi muonea huruma ya asha liza wengi
 
Nimeona kuna video clip inazunguka ambayo inaonyesha maafisa uhamiaji wakimsulubu jamaa bila kujali ni kosa gani ametenda ni aibu kwa idara hii ambayo inatakiwa ku-enforce law badala yake amefanya kitendo ambacho kisheria hatujui tunakiitaje.

Mfumo wa haki jinai na makosa yake unaelekeza vyema kamata mtu peleka mahakamani na siyo kama inavyoonekana pichani.. kama umebainika kuingalia video hiyo kuna sehemu wana sema wamepata maelekezo kutoka kwa PCO (sijui ndio Nani)

Haya yote ni Madhara ya matumizi mabaya ya neno “jeshi” siku za hivi karibuni maafisa hawa wanajiita jeshi la uhamiaji nachojua uhamiaji inafanya kazi kimuundo kama inavyoelekezwa kwenye immigration act ya mwaka 1995 aliyesema uhamiaji ni jeshi ndio ametuletea Haya mods usifute huu uzi tafadhali uhuru wa kuongea uhuru maoni




97E6107A-8F44-487D-A705-3E532CB812ED.png


10447C33-F1B5-40E3-B04D-C299DCB90D14.png


62336BE6-66A2-4DE5-AC47-02C5D471FEE8.png


997B410B-A707-49CC-8A1A-AE1A5DA0C218.png

.
 

Attachments

  • 8ADB0703-A72F-43D4-9AB1-E6004B5D8A64.MP4
    9.8 MB
Wawajibishwe.

Na walivyo mataahira walichua wanachukua video clip.

Ndio mjue kweli majamaa hamnazo na CaG aliye pita alikuwa sahihi
 
Back
Top Bottom