Sherehe ya Kichuguu Kufikisha Miaka 11 Jamii Forums

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
16,659
21,860
Miaka sita iliyopita, niliandika thread hii Nitafikisha Miaka Mitano Kama Memba wa JF.

Utaona kuwa miezi michache ijayo nitakuwa nafikisha miaka 11. Nina mpango wa kufanya sherehe kubwa sana kukumbukia siku ya mimi kujiunga na JF. Siku ninajiunga nilikuwa nimetoka kusaini makaratasi ya kuuza nyumba yangu ya zamani ambayo ilikuwa haitoshelezi mahitaji yangu ya maisha wakati huo, na nilikuwa nakaribia kumaliza ujenzi wa nyumba kubwa ninayoishi sasa. Hata hivyo ilinichukua miezi miwili ya kuishi kwenye apartment kabla sijahamia nyumbani hapa rasmi, ambako nilihamia December 21, 2006 nikiwa sina connection yoyote ya cable TV na internet. Hivyo wakati Saddam Hussein anayongwa sikupata taarifa za matukio hayo hadi January 5th, 2007 ndipo nilipopata TV tena. Ukifuatilia posts zangu utagundua kuwa kati ya December 22 hadi mwanzoni mwa Januari 2007 huenda sikupost chochote hapa, labda kama nilifanya kwa kutokea kazini ambako wakati huo tulikuwa kwenye chrismas/new year break, au kwa kutokea kwenye apartment ambako nilikuwa na lease ya mwezi mzima zaidi.

Nia ya post hii ni kuomba ushauri wa kusherehekea siku hiyo ambayo ni kama miezi sita ijayo. Tafadhali nipe maoni yako kuhusu mambo mazuri ya kufanya kuhusu kumbukumbu ya siku hiyo. Ninaamini kuwa uanachama wangu hapa ulichangia kwa namna fulani kuwepo kwa mada za kuelimisha, kukosoa na hata za pumba. Samahani sana kwa zile mada zangu za pumba, naomba mwelekeo wa mbeleni.
 
Mkuu Kichuguu hongera kwa kufikisha umri huo hapa jukwaani. Ushauri wangu kwako sherehekea kwa kuridhisha matakwa ya hisia zako mwenyewe. Tofauti na hapo unaweza kuumiza nafsi yako. Tambua kwamba hii Forum haiko tena kifamilia kama ilivyokuwa mwanzo. Kila la kheri.
 
Sherehekea upendavyo, si vibaya ukawaalika rafiki zako wa jf mnaofahamiana, na kama huna rafiki yoyote humu jf haina faida kwako kivile, basi usherehekee kukumbuka kuingia nyumba kubwa
 
Kichuguu ni legendary hapa JF ...ni moja ya members watu wazima ambao wametusaidia sana kujua historia na kumbukumbu nyingi za nchi hii. Binafsi namuheshimu sana kwa jinsi anavyojenga hoja kwa ustarabu hata pale mnapopishana. Hawa akina Kichuguu ndio waliowafundisha siasa na namna ya kujenga hoja wanasiasa wengi ambao ujasiri wao ulianzia hapa JF akiwemo marehemu Regia Mtema .....ombi langu kwake na wazee wetu wengine humu akina Shwari wasikerwe na uelekeo wa mijadala humu bali waendelee kutoa elimu bila kuchoka maana lengo la JF haikuwa wabaki werevu wachache kama ilivyokuwa mwanzo bali tulitamani waje Watanzania wengi zaidi ili tubadili fikra zao ....hongera sana Kichuguu usisahau kunipa mwaliko tafadhali ....
 
Mkuu hizo post na huto tu like ndani ya miaka ichumi na imwe..daah
Wewe umejiunga wakati jukwaa limeshabadilika kutoka Jambo Forums na kuwa Jamii forums, na vile vile idadi ya post za kila mwanachama kuwa zimeshaaza kuhesabiwa upya nadhani mara mbili hivi, kwa hiyo hujui kuwa tulishawahi kuwa na posts zaidi ya elfu kumi na likes zaidi ya elfu saba kabla ya mwaka 2010. Uchaguzi wa 2010 ulileta wachangiaji wengi wasiokuwa na mantiki hivyo wengine tukapunguza spidi ya kupost mambo hapa. Idadi ya post na likes siyo kipimo cha uchangiaji mzuri; hata hiyo post yako ya msitali mmoja nimekupa like japokuwa haina mantiki yoyte.
 
Kichuguu ni legendary hapa JF ...ni moja ya members watu wazima ambao wametusaidia sana kujua historia na kumbukumbu nyingi za nchi hii. Binafsi namuheshimu sana kwa jinsi anavyojenga hoja kwa ustarabu hata pale mnapopishana. Hawa akina Kichuguu ndio waliowafundisha siasa na namna ya kujenga hoja wanasiasa wengi ambao ujasiri wao ulianzia hapa JF akiwemo marehemu Regia Mtema .....ombi langu kwake na wazee wetu wengine humu akina Shwari wasikerwe na uelekeo wa mijadala humu bali waendelee kutoa elimu bila kuchoka maana lengo la JF haikuwa wabaki werevu wachache kama ilivyokuwa mwanzo bali tulitamani waje Watanzania wengi zaidi ili tubadili fikra zao ....hongera sana Kichuguu usisahau kunipa mwaliko tafadhali ....
Niliwahi kusoma historia ya sarafu, kweli ilinisaidia kuzifahamu hata sarafu ambazo sijawahi kuziona wala kuzisikia.
Kichuguu
 
Kweli akili ni nywele.

Hauna jambo la maana la kufanya?
Mkuu Sumu
Huyu Kichuguu ni mmoja kati ya "Wazee" wenye heshima sana humu ndani.Tumewapoteza wengi sbb ya aina ya uchangiaji kama wako wa kumshambulia mtu.Hawa kina Kichuguu JokaKuu Mag3 Field Marshal Mzee Mwanakijiji na wengine wengi,ndio walitufanya sisi kuipenda hii forum.

Mimi ID yangu ya kwanza kabla ya kusahau nywila,nilijiunga 2007 sbb ya hawa nguli.Tuwape heshima yao
 
Miaka sita iliyopita, niliandika thread hii Nitafikisha Miaka Mitano Kama Memba wa JF.

Utaona kuwa miezi michache ijayo nitakuwa nafikisha miaka 11. Nina mpango wa kufanya sherehe kubwa sana kukumbukia siku ya mimi kujiunga na JF. Siku ninajiunga nilikuwa nimetoka kusaini makaratasi ya kuuza nyumba yangu ya zamani ambayo ilikuwa haitoshelezi mahitaji yangu ya maisha wakati huo, na nilikuwa nakaribia kumaliza ujenzi wa nyumba kubwa ninayoishi sasa. Hata hivyo ilinichukua miezi miwili ya kuishi kwenye apartment kabla sijahamia nyumbani hapa rasmi, ambako nilihamia December 21, 2006 nikiwa sina connection yoyote ya cable TV na internet. Hivyo wakati Saddam Hussein anayongwa sikupata taarifa za matukio hayo hadi January 5th, 2007 ndipo nilipopata TV tena. Ukifuatilia posts zangu utagundua kuwa kati ya December 22 hadi mwanzoni mwa Januari 2007 huenda sikupost chochote hapa, labda kama nilifanya kwa kutokea kazini ambako wakati huo tulikuwa kwenye chrismas/new year break, au kwa kutokea kwenye apartment ambako nilikuwa na lease ya mwezi mzima zaidi.

Nia ya post hii ni kuomba ushauri wa kusherehekea siku hiyo ambayo ni kama miezi sita ijayo. Tafadhali nipe maoni yako kuhusu mambo mazuri ya kufanya kuhusu kumbukumbu ya siku hiyo. Ninaamini kuwa uanachama wangu hapa ulichangia kwa namna fulani kuwepo kwa mada za kuelimisha, kukosoa na hata za pumba. Samahani sana kwa zile mada zangu za pumba, naomba mwelekeo wa mbeleni.

Uplatinum unapatikanaje mkuu
 
Hongera sana tumuombe Mungu akufikishe salama siku tarajiwa
 
Mkuu Sumu
Huyu Kichuguu ni mmoja kati ya "Wazee" wenye heshima sana humu ndani.Tumewapoteza wengi sbb ya aina ya uchangiaji kama wako wa kumshambulia mtu.Hawa kina Kichuguu JokaKuu Mag3 Field Marshal Mzee Mwanakijiji na wengine wengi,ndio walitufanya sisi kuipenda hii forum.

Mimi ID yangu ya kwanza kabla ya kusahau nywila,nilijiunga 2007 sbb ya hawa nguli.Tuwape heshima yao

Nimekuelewa mkuu.

Samahani sana mkuu Kichuguu. Nimefuta kauli.

Hongera sana na Mungu azidi kukuongezea busara.
 
Back
Top Bottom