PRINCE CROWN
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 5,210
- 4,182
Kadhi wa mkoa wa dsm, Sheikh hamid jongo, mwakilishi wa kundi la dini katika bunge la katiba ametoa machozi ya uchungu ya kutukanwa waasisi wa taifa hili mwalim j.k nyerere na sheikh abeid karume. Ameeleza kusikitishwa kwake kwa tabia hiyo ya kutoa matusi na kejeli kwa wazee hao yaliyofanywa na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo akisema kuwa mtu akishakufa huachwa bila kusemwa vibaya kwa sababu tayari anakutana/amekutana na mungu ambaye ndio hakimu wa kweli.
amelia na kudondosha chozi na kuwaomba wabunge watumie lugha za staha na kistaarabu
Unacheza na pesa ya CCM? Usishangae kumskia anamsafia Lukuvi.
Inamaana hicho kilio kitakuwa kimeingia kwenye ansad, maana hajakikanusha kifutwe. Kweli ukiwa msanii hufi njaa.....
Unafiki, anaacha kulia Lukuvi kuongea ujinga kanisani, Komba kutishia kuingia kichakani, bi Asha kuporomosha matusi bungeni ana lia kumkosoa Mwl. Nyere? Kichekesho.
Huyu Sheikh Ubwabwa nae njaa tu inamsumbua, kuna vitu vingi vya maana vya kutoa machozi lakini sio hilo jambo. Kuna watanzania wangapi wanakufa kutokana na kukosa huduma muhimu za afya lakini hatoi machozi, kuna wakina mama wangapi mahospitalini wanaolala chini na wengine wanne kwenye kitanda kimoja lakini hatujamsikia anamwaga chozi, kuna wanafunzi wangapi wanaishia kukaa chini huku wakikosa walimu mashuleni na hatujamsikia akilalamika.
Na hii iwaendee viongozi wote wa dini wanaoweka maslahi ya matumbo yao kwanza kuliko mahitaji muhimu katika jamii yetu.