Written By Mohamed Said on Sunday, March 22, 2015 | 11:27 AM
Filamu ya Masheikh wa Bagamoyo ilikuwa ishafikia mwisho na wao kama jeshi lilikuwa lishateka nchi na sasa linaondoka likielekea kunakozama jua baada ya kuangamiza adui.
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]![]()
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Sheikh Abdulkadir bin Sheikh Mohamed Ramiyya
Sheikh wa BAKWATA wa Wilaya ya Bagamoyo
na Khalifa wa Tariqa Kadiriyya[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Hii ndiyo ilikuwa staili ya Hollywood kumaliza senema na baada ya mbabe kuelekea machweo ya jua ndipo inatokea ile "The End."
Enzi hizo mimi kijana mdogo niko Empire Cinema macho nimekodoa kwenye, "screen." Senema zetu zilikuwa za mchana siku ya Jumamosi na Jumapili.
Nakumbuka kwa masikitiko makubwa starehe niliyokuwa napata mwisho wa senema kumuona mbabe anondoka juu ya farasi wake kwa ushindi.
John Wayne au Clint Eastwood...
Hii senema ya Masheikh wa Bagamoyo ilikuwa kama vile wameshinda na ni wababe wanaondoka Dodoma kwa ushindi wanatokomea machweo ya jua la Maghrib, lile jua la rangi ya udhurungi.
Haikuwa.
Ghafla mlio wa risasi unasikika.
Kamanda aliyekuwa katangulia na jeshi lake linamfuata nyuma kuelekea machweo ya jua kapigwa risasi ya kichwa kaanguka.
Kinachofatia ni taharuki ya askari wake waliokuwa wanamfuata nyuma.
Risasi nyingine zinaanza kuvuma kila upande jeshi linashambuliwa na askari mmoja baada ya mwingine wanapigwa risasi mfululizo na kuanguka huku wakitoa vumbi kubwa.
Tahamaki jeshi zima limemalizwa.
Hapo ndipo senema inakwisha na ile "The End," inatokea...
Khalifa wa Qadiriyya Sheikh Abdulkadir Ramiyya anazungumza na waandishi wa habari na kuwapa taarifa ya BAKWATA kuwa hawatambui masheikh waliokwenda Dodoma kuonana na Lowassa...
Khalifa kapiga, "ambush."
Watazamaji senema wanapoondoka kuelekea majumbani wanalaumu wanasema, "Mbona hii senama imemalizika vibaya.
"Mimi sipendi mbabe anakufa," mmoja wa waliotazama senema analalamika.
Mimi najiuliza imekuwaje hii "script," imefanywa hivi?
Huyu Muongozaji Filamu anataka kutoa ujumbe gani?
Najisemea kirohoroho.
"Hapendi senema zenye kumalizika kwa furaha?" Jamaa mmoja anasema kwa mshangao.
"Huyu "director," mimi namjua senema zake zote yeye ni "tradegedies," tu. Hapendi kufurahisha watazamaji. Mara kazamisha meli, mara mchumba wake mbabe kanywa sumu, kagongwa na nyoka kafa ili muradi ni "director," mtata sana huyu..."
Kwani nani huyu - Oliver Stone au Spielberg?
Mtu mwingine anauliza.
Bla bla bla bla bla bla...
![]()
Picha ya Chini: Sheikh Abdulkadir Akizungumza na TV Azam Kuhusu
Masheikh wa Bagamoyo Waliokwenda kwa Lowassa Dodoma
![]()
Kadoda 11 na Cargo,
Enzi zetu kujipumzisha na kustarehe mwisho wa juma ilikuwa kusoma.
Nyie ni DVD tena muziki, muziki, muziki...
Ndiyo maana nikiandika mnafurahi...
Ni staili tu za waandishi mbalimbali tuliosoma miaka na miaka iliyopita.
we mzee kwa kurembesha maneno tu huna mfano nowe.point yako haikutakiwa kuzidi hata mistari mitatu.hata hivyo asante kwa taarifa.
Masumbuko...
Naomba nifahamishe nini BAKWATA wamefanya huko Moshi.
Duuuh umenikumbusha mbaaali enxi za video kwa jirani
Tusker...,
Hapana Ahmed Rajab ni mwingine lakini tunafahamiana sana toka Uingereza.
walijuaje kama wakienda watamkuta? walijuaje anapopatikana? ina maana hana pesa ya kuchukua fomu mpaka watu waanze kujichanga? mbona hawawezi kuchanga wachimbe hata kisima cha maji? je walijiorganise vipi? unapata wapi muda wa kuanza kuchangisha michango, kuswalisha, kutunza familia na kwenda dodoma kukabidhi pesa huku nyuma nani anashughulikia masuala yako ya familia? pesa ya kuchanga nauli ya dodoma, gharama zote za kukaa dodoma na oppotunity cost ya kuacha shughuli zako kwa nini usimpeleke mwanao shule? huu ni ujinga na upumbavu, watanzania nani katuambukiza ujinga
Hayahayahayaaaaaaaaa namuona sasa komando anaamka tena baada ya kumminiwa risasi kama sabini hivi,
Huyo ndiyo lowasa bwana najiuliza wanafunzi walijuaje kuwa leo atakuwa idodomia hivyo wakajiandaa kumtokezea?
Na je kesho atakuwa wapi ili mapadri na wachungaji wamtokezee, labda itakuwa mbeya,ngoja tuone