Sheikh wa Wilaya Bagamoyo amkana Lowassa

Sheikh wa Wilaya Bagamoyo amkana Lowassa

Siamini kwamba msafara ule ulikuwa na baraka za Jakaya.

Kama Mtu anajiundia "Mashehe" Wake , Then Mashehe hawa wakamuunga Mkono HUYU MTU SI WA KUOGOPA KAMA UKOMA?

Namwomba musa allan, simiyu yetu, f.foixy, rutashobya, tandale one , na wale misukule wengine waje hapa kudhibitisha wale wachumia tumbo no wao waliwatuma ama ni njaa zao ndizo zilizowapeleka pale.?
 
Huyo sterling fake haki ya nani atafia kwenye jukwaa! Kampeni za miezi miwili hataziweza, ile afya ni ya kupumzika na kutumia mafao uliyojilimbikizia! Lakini kwa vile watu wana tamaa za kukanyaga ikulu, wacha ajaribu ila hatutaki lawama!!
 
Lowasa atafute muandika script mwingine huyu wa sasa hana viwango FILAMU zinakosa uhalisia, aibuu Yao. Kama m2 anasifa maigizo ya nini jamani????? Candidate wa namna hii hana nia njema na taifa letu, hutakiwi kufanya maigizo ili uchaguliwe, na anae engineer hii mipango ni kilaza wa mwisho.
Anaitwa Abubakar Liongo, kilaza wa haja.
 
Mkuu mimi sio shabiki wa Lowasa na CCM yake kwa ujumla, ukiachilia mbali kuwa mshauri.
Nilikuwa tu najaribu kuangalia mapungufu ya ule waraka wa shehe, unaokanusha taarifa zilizoandikwa na magazeti.

usimfananishe Lowassa na marehemu Sokoine.nimeona kwenye andiko lako ukimwita sokoine Jr. Hawafanani hata kidogo si kwa sura wala matendo.
 
Tunazungumzia Masheikh wepi? Wa Bakwata? Je wale walioenda kwa Mh Lowassa ni wa Bakwata?

Hii nchi bana.....njaa zinatusumbua sana. Hatukawii kuambiwa hata hawa wa Bakwata wanaotoa tamko hili pia ni wanaganga njaa tu kutoka kwa potential candidate mwingine!

Kwa vyovyote vile, hii ya kuingiza dini kwenye minyukano ya kisiasa ina hatari na athari kubwa sana kwa Taifa letu.
 
Hapa tuweke udini pembeni ila tatizo la waislam ni kuruhusu dini yao iongozwe na serikal badala wao kujitegemea,hivi inaingia akilin bakwata kuwa chombo cha kiserikal kwa mwamvuli wa dini?eti kuna shehe wa mkoa,shehe wa wilaya,jaman kwanza waislam mnatakiwa kuwa independend ndo mtaweza hata kuwa na msimamo wa pamoja,ujue hata wanaowasikiliza mashekhe wa sasa ni wachache weng hawawaheshim tunachukuliana poa tu na mashekhe hawana nguvu,wapo wapo tu hawajielewi nao wamekua wizara ya dini serikalini
 
Watu wanachanganya mambo hapa, siyo wote ni mashehe wa Bakwata kwanza asilimia kubwa ya waislamu wanalipinga hili likitu linaitwa Bakwata so wale walio enda kwa Rais mtalajiwa wanaweza kuwa wanopingana Bakwata. Pasco we ukiwa mdau wa EL hebu tuweke sawa hili maana naona watu povu
 
Last edited by a moderator:
walijuaje kama wakienda watamkuta? walijuaje anapopatikana? ina maana hana pesa ya kuchukua fomu mpaka watu waanze kujichanga? mbona hawawezi kuchanga wachimbe hata kisima cha maji? je walijiorganise vipi? unapata wapi muda wa kuanza kuchangisha michango, kuswalisha, kutunza familia na kwenda dodoma kukabidhi pesa huku nyuma nani anashughulikia masuala yako ya familia? pesa ya kuchanga nauli ya dodoma, gharama zote za kukaa dodoma na oppotunity cost ya kuacha shughuli zako kwa nini usimpeleke mwanao shule? huu ni ujinga na upumbavu, watanzania nani katuambukiza ujinga
unasema zile pesa zilikuwa ni za umma!! au za mafisadi!!??:majani7:
 
He thinks he is successfully creating a fait acompli situation within CCM kwa hizi payed for stage managed antics. No way boss jamaa kaula wa chuya
 
Kwani kuwa sheik bagamoyo lazima utumikie bakwata? Kwanza bakwata au taasisi nyingine rasmi ya dini hatutaki wajihusishe na siasa. Kwahiyo walioenda kivyao hawajakosea ni haki yao na ndivyo inavyotakiwa. Maana hawajaenda kwa kofia ya dini bali as individuals. Suala kama waliratibiwa hilo sina sina la kusema. Kila mwanasiasa ana mbinu zake wacha wapambane na kama chama chake kitampitisha basi waamuzi wa mwisho ni wananchi kwenye sanduku la kura.
 
Kama watu wazima wameshawishika kuanza safari all the way kutoka bagamoyo kwa mabasi hadi Dodoma basi wanaweza kufanya hivyo hata siku ya uchaguzi. Na kama hao wanaoratibu wamefanikiwa kwa kiasi hicho kuwashawishi makundi mbalimbali katika jamii basi wanaweza kufanikiwa hats kushawishi wengi zaidi kuliko sasa nawe unayesoma ukawa mmoja wao. Ndiyo kwanini isiwezekane?
 
Siamini kwamba msafara ule ulikuwa na baraka za Jakaya.

Kwani aliyesema ulikuwa na baraka za Kikwete ninani?. Kikwete na familia yake wanamtaka Membe. Hata Lowasa hajasema wametumwa na Kikwete. Hivi nyinyi mnadhani Rizone amefurahi kuona mashekhe wamejaa Dodoma?. Lazma atahangangaika tu.




Ulichosema ndio ukweli wasiotaka kuusikia.
Haiwezekani watu wote wanaojitokeza kwenda kumshawishi Lowasa achukue form wawe wajinga.

Wanafunzi wa vyuo haiwezekani wote wakamuunga mkono Lowasa au wote wakampinga.
Hali kadhalika haiwezekani mashehe wote wa Bagamoyo wakamuunga mkono Lowasa au wote wakampinga.
Mtu anaposema kuwa Lile halikuwa tamko la mashehe wote wa bagamoyo yuko sahihi kwani kuna wachache wasio muunga mkono. Hawa kazi yao ni kusubiri na kukanusha.
Nje ya watawala wapo watu wengi wanaomuunga mkono Lowasa;Wanachama na wasio wanachama wa CCM.

Wanafunzi wengi kama wale wa UDOM hawawezi woooote kununuliwa.
Kama wanabisha basi wafanye utafiti hata kwa kupiga kura za siri kwenye vyuo au kwa wananchi wakawaida ili wapate kumhukumu kuwa hawa watu mbona utafiti unaonyesha kuwa UDOM wanaokuunga mkono ni watu 20 lakini maandamano tumeona watu 2000 .Hapa umefanya igizo la kununua watu.
Vinginevyo wengi tunaamini ni siasa za chuki na maji taka zinaoendelea ndani ya vyama vya siasa kwa wale wanaokubalika kwa wananchi ila kwa viongozi ni tishio.

Mpaka sasa Lowasa hajasema kwamba atagombea au bado? Je,tukisema kuwa mahasimu wake ndio wanao wanunua watu ili waandamane kumtaka Lowasa atoe tamko la kugombea kisha wapate pa kumhukumu kwamba ametangaza kabla ya muda tutakua tunakosea?
Tujiulize ni kwani nini hawataki kutoa tathmini ya adhabu waliyokuwa wametoa kwa wale makada 6 walioambiwa kuwa wamekiuka kanuni za chama? Je,hapa sio mchezo wa kuigiza unaofanya na kambi za mahasimu wa mh. Lowasa ili atangaze kuwa tagombea urais wapate pa kusemea? Majungu ,fitina na chuki ndivyo vinavyoimaliza CCM.

Yapo mengi yanayofanywa na watangaza nia wengine waliopo madarakani tena mpaka ndani ya vyombo vya dola lakini watu wanakaa kimya kulinda heshma ya nchi lakini baadhi ya wananchi wakiamua kumshawishi mtu wao wanayemtaka inakuawa ni uchu wa madaraka.

Mbona hatushughuliki na wale wanaotuhumiwa kutaka kumuua Dr. Slaa ili tu malengo yao yatimie?.Je,huo ndio usafi na uzalendo?

Kama ni kweli kwamba Lowasa anafanya igizo basi naendelea kuamini kuwa Lowasa na kambi yake ni wabunifu kuliko wenzake na kambi zao za majungu na fitina.
 
Soma hapa tamko la viongozi wa dini jinsi walivyopinga juu ya upotoshwaji wa vyombo vya habari.

View attachment 236919

siasa ni mchezo mchafu sana na.ndio uchafu huohuo unaowapa watu madaraka na kutuongoza..
hakuna mwanasiasa msafi hata siku moja,tusubiri wakati ufike wa kupitishwa apite tukatumie haki yetu ya msingi kumchagua rais atakayefaa..
kwa wakati huu tutarajie mengi tuu hata kama ni sibema ama uhalisia
 
Lowassa ni mwanasiasa mkongwe,shupavu na mwenye uzoefu na siasa za Tanzania,sina hakika sana kama ataweza kutumia trick za kinamnanamna kuonesha popularity yake (ingawa wengi wanamkubali ukiacha mijini)...
 
watu wapo makini na fursa, wameshapiga mpunga tayari..
 
Back
Top Bottom