Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,420
- 33,982
JokaKuu,..I know all that.
..lakini hapa kinachoendelea ni SIASA.
..kwa hiyo unatakiwa ukitizame kwa jicho la kisiasa.
..sit back and enjoy the "movie". huu ni mchezo unachezwa hapa kuhalalisha candidacy ya mgombea fulani.
..CCM kwenye mkutano mkuu unaochagua mgombea Uraisi huwa wanasema "tusipoteua mgombea anayeungwa mkono huko nje..." sasa huyu anayecheza mchezo huu anajibu hoja hiyo.
..Hii script ilichezwa hata wakati wa Kikwete. Aliyeandika script hiyo ndiyo huyo huyo alieandika hii script inayochezwa sasa hivi.
..This is politics and has nothing to do na historia ya Bagamoyo.
You knew all this!
Really...hapa Majlis au kabla.
Hii ya masheikh wa Bagamoyo ina kila kitu na historia yake kama
ngome ya TANU kisha sasa CCM.
Huwezi kuwa sheikh hapa Bagamoyo kama si murid wa Qadiriyya.
Murid hana sauti mbele ya Khalifa wake.
Wewe huwezi kuyajua haya ndipo nilipokupa rejea usome ili uwe
mjuzi wa hizi "politics" za Uislam na Siasa hapa nchini.
Wakati wa kupigania uhuru katiika uchaguzi mmoja kuna kisa hiki
mashuhuri.
Khalifa wa wakati ule Sheikh Mohamed Ramiyya alitaka TANU
ishinde sana.
Sheikh Ramiyya akaitisha maulid kubwa na yeye mwenyewe
akapanda kwenye membar kavaa joho lake la ukhalifa.
Hiyo ni usiku wa manane maulid yamewiva.
Khalifa akawaambia murid wake:
"Mimi Khallifa wenu nimesimama hapa kukuambieni kuwa yule
asiyeipigia kura TANU basi ajue kesho kiama hatafufuliwa na mimi."
"Tariqa," maana yake ni "njia."
Mwenye kuongoza watu wake kwenye njia ni Khalifa.
Ndiyo maana hadi leo hakuna sheikh yoyote wa Bagamoyo kasimama
kumjibu Khalifa Sheikh Abdulkadir bin Sheikh Ramiyya.
Hawatathubutu kwa kuwa wanajua nini kitafuata.
Nadhani unajua "excommunication," katika Ukatoliki.
Usipuuze ushauri wangu rudi kasome kitabu hicho cha Nimtz.
Nakuongezea na mengine.
Soma historia ya Mahdi wa Sudan uone ni vipi akiwa na jeshi la
Ansar aliweza kupambana na Waingereza katika miaka ya mwishoni
1800s.
Jeshi la Ansar lilikuwa jeshi la murid.
Closer to home.
Vipi TANU na Nyerere aliweza kupata wafuasi wengi juu ya kuwa
yeye alikuwa mgeni Dar es Salaam.
Waliomuunga mkono huko mashamba kama Rufiji na majmbo ya
Kusini walikuwa murid chini ya uongozi wa masheikh wao akina
Sheikh Hassan bin Amir, Mohamed Yusuf Badi na wengineo.