Sheikh wa Wilaya Bagamoyo amkana Lowassa

Sheikh wa Wilaya Bagamoyo amkana Lowassa

Hebu pitia waraka huu, je Lowassa alichonga masheikh feki?

11076281_813096822073528_3680534241173890727_n.jpg
 
Ppp
Wewe ni mwanachama wa vyama viwili,CCM na ACT kwa pamoja?hii ni kwa mujibu wa mabandiko yako humu!
Mimi nipo ACT Tanzania mkuu.lakini sikatazwi kutoa maoni yangu hapa jf is the place where we dare to talk openly.ina maana wewe unachangia topic zinazohusu chadema pekee.?
 
Sunday, March 22, 2015 Maoni: 0





​

Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Sheikh Abdulkadir Mohamed Ramiya akiongea na mwandishi wa Azam TV Bw. Octaviana baada ya kutoa tamko lake (hapo juu) leo mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani​



source; MichuziJR
 
Lowassa anazidi kuaibika sijui wale masheikh ubwawa wa jana aliwatoa wapi.
 
Nashindwa kuelewa bado ni nini kilichomfanya EL afanye alichofanya.
 
usimfananishe Lowassa na marehemu Sokoine.nimeona kwenye andiko lako ukimwita sokoine Jr. Hawafanani hata kidogo si kwa sura wala matendo.
My apology mkuu, kuna watu nilisikia mahali wanatumia hilo jina, ila walimwita kwa kuwa tu yuko jimbo la Sokoine.

Ni kweli kabisa, Sokoine na Lowasa ni vitu viwili tofauti. My apologies again.
 
Naomba konekisheni na EL jamani au kama kuna mwana JF anajua jamaa anakata fuba kiasi gani aniwekee hapa,nataka namie ni organize kikundi fulani tumwibukie, mwaka wa mavuno huu,by election ya udiwani Kirumba 2012,ilinipatia bajaji 2,na kipindi chote cha kampeni bia na nyamachoma vilinihusu sana tu,sasa nataka nichange karata zangu vizuri kwenye u prezidaa wa EL,walahi lazima ninunue chopa
 
Mjasiria,
Ukitaka kuwajua BAKWATA na nafasi yao katika siasa za Tanzania inabidi
usome kitabu cha Abdul Sykes Sehemu ya Tatu niliyoipa anuani - "Njama
Dhidi ya Uislam."

Kwa mistari minne mitano hapa Majlis hakuna atakaeweza kuieleza BAKWATA.
Nakipata wapi hicho kitabu?
 
Nakipata wapi hicho kitabu?

Mjasiria,
Ikiwa uko Dar es Salaam kitabu kipo Tanzania Publishing House,
Samora Avenue hapo utakipata kwa T.Shs: 15,000.00.

Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro na Msikiti wa Manyema
hapo ni shs: 10,000.00.

Book Centre Mbezi ni shs: 10,000.00

A Novel Idea Slip Way Masaki 15,000.00

Cafe Bookshop, Mikocheni (sina hakika ya bei)

Arusha Kase Bookshop (sina hakika ya bei)
 
Hawa wafu wananifurahisha sana wanavyoanza kupasuka vipande vipande
 
Ma Presdent is Lowassa. ...ujumbe ulishawafkia watanzania...mnaokanusha tunajua team bm imepagawa kwa nguvu isiyo na mfano ya EL ..napta
Lowasa anahangaika bure
 

Attachments

  • IMG-20150323-WA0000.jpg
    IMG-20150323-WA0000.jpg
    66.7 KB · Views: 162
JokaKuu,
Niko upande wa BAKWATA kwa vipi?
Kuhusu masheikh wa Bagamoyo kuwa BAKWATA au vinginevyo...

Inabidi ujue siasa za Bagamoyo toka enzi za kupigania uhuru 1950s
wakati Sheikh Mohamed Ramia akiwa si tu mmoja katika viongozi
wakubwa wa TANU bali alikuwa ndiye Khalifa wa Tariqa Kadiriyya.

Bila ya kujua haya hutaelewa nini kinaendelea sasa na kwa nini
Khalifa wa sasa mtoto wa Sheikh Mohamed Ramiyya kawakana
masheikh hao waliokwenda kwa Lowassa.

Ukitaka kujua ushawishi wa ukoo wa Sheikh Mohamed Ramia katika
siasa za Bagamoyo msome August H. Nimtz Jr, Islam and Politics in
East Africa, University of Miannapolis, 1980.

0


Kushoto: Idd Faiz Mafongo (Mwekahazina wa TANU), Sheikh Mohamed
Ramiyya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro, Haruna Taratibu.
Idd Faiz
na Sheikh Ramiyya walikuwa mabinamu.

..I know all that.

..lakini hapa kinachoendelea ni SIASA.

..kwa hiyo unatakiwa ukitizame kwa jicho la kisiasa.

..sit back and enjoy the "movie". huu ni mchezo unachezwa hapa kuhalalisha candidacy ya mgombea fulani.

..CCM kwenye mkutano mkuu unaochagua mgombea Uraisi huwa wanasema "tusipoteua mgombea anayeungwa mkono huko nje..." sasa huyu anayecheza mchezo huu anajibu hoja hiyo.

..Hii script ilichezwa hata wakati wa Kikwete. Aliyeandika script hiyo ndiyo huyo huyo alieandika hii script inayochezwa sasa hivi.

..This is politics and has nothing to do na historia ya Bagamoyo.
 
Hawa wafu wananifurahisha sana wanavyoanza kupasuka vipande vipande

Emma na Wanamajlis,
Katika mashujaa wangu niliokuwa nikiwahusudu sana wakati mimi mdogo
ni Muhammad Ali wakati ule 1964 akijulikana kama Cassius Clay.

Baba yangu akifanya kazi posta na alikuwa akijua ni vipi nampenda Clay.

Yupo kazini mara tu alipopata habari kuwa Clay kampiga Liston akanipigia
simu kunifahamisha.

Leo nikiangalia nyuma zama zile huwa sisemi mengi hubakia kushukuru.

Kwa umri ule wa miaka 12 tayari nishakutana na "somo" yake Cassius Clay
Cassius
katika "Julius Caesar," ya William Shakespeare.

Leo watoto ukiwauliza kuhusu kitabu hicho watakuuliza, "Kwani baba video
yake hakuna?"

Kusoma vitabu imekuwa adha kwa wanetu wepesi ni kuangalia DVD.
Tuyaache haya turudi kwa Muhammad Ali.

Katika vitabu vyangu nivipendavyo (nami ni mpenzi wa "biographies,") kimoja
ni "The Greatest My Own Story," alichoandika Ali kuhusu maisha yake.

Katika kitabu hiki kuna sura naipenda sana.
Ali anaeleza pigano lake na George Foreman mwaka 1974, Kinshasa, Zaire.

Ali anaeleza kuwa mchuaji wake (mtu wa massage) alikuwa mzee mmoja
kutoka Cuba.

Wakati wako kambini kwa matayarisho ya pigano lile yule mzee wa Kicuba
akampa changamoto Ali akamwambia, "Ali usijisifu kwa kumpiga Sony Liston.
Liston alipokutana na wewe umri wake ulikuwa ushapea mtu yoyote angempiga.
Ikiwa wewe kweli unataka kuudhihirishia ulimwengu kweli wewe ni, "The Greatest,"
basi mpige Foreman. Huyu ni simba ana nyama ndani ya tundu lake. Ingia ndani
ya tundu uichukue hiyo nyama."

Wakati ule Foreman ndiye alikuwa na mkanda wa dunia na kila mpinzani
alikuwa hakatizi mzunguko wa tatu tayari anakuwa keshawekwa chini yu
taabani janga lilomkuta Joe Frazier kutoka kwa Foreman dunia nzima ilishuhudia.

Ali aliingia katika tundu la simba na akatoka na nyama.

Alimpiga Foreman katika mzunguko wa saba na akawa bingwa wa dunia
kwa mara ya pili.

Hiki kisa nakileta kwa kuangalia hali ya mbio za urais katika CCM.

Picha inayojitokeza ni kwa wananchi kwenda kwa EL nyumbani kwake
Dodoma kumshawishi na kumuomba agombee urais na wao watampa kura
zao.

Katika "hope fulls," tuliokuwanao katika CCM hakuna ambae aliyeweza
kuonyesha kupendwa kama anavyopendwa EL.

Natamani kuweka "inverted commas," lakini naogopa kuwaudhi wapenzi wa
LE naona nende hivi hivi juu - kwa juu.

(Katika raha mojawapo ya Majlis hii ni kuwa vijana wanakufunza msamiati
mpya wa kueleweka haraka - "juu kwa juu," maana yake haifati sheria yaani
"deviation from the norm").

Kwa hizi kampeni za wananchi kutoka kila pembe kwenda Dodoma nyumbani
kwake LE kumshawishi hakuna mpinzani wake hata mmoja aliyekanyaga
ardhi hiyo hata kwa pembeni yake.

LE kawaacha wenzake kwa mbali sana.
Hata hivyo kuna mengi yanayosemwa.

LE keshakuwa simba na ana nyama ndani ya tundu lake.

Shujaa gani katika CCM atakuwa na ujasiri wa kuingia katika tundu lile kuichukua
nyama ile?

Hakika ni wazi kuwa atakaeweza kupanda ulingoni na LE na kumshinda kwenye
ulingo njia kwake itakuwa nyeupe ndani ya CCM kupeperusha bendera ya kijani.

Lakini naogopa hata kuliwaza hili kwani naamini damu itakuwa nyingi sakafuni
hiyo siku ya pambano.

Sasa naona nimalize kwa kurejea tena kwa Cassius katika "Julius Caesar."
Caesar kamtazama sana Cassius kisha akasema maneno haya:

"Yond Cassius has a lean and hungry look.
He thinks too much. Such men are dangerous."

Hapana sipigi, "alarm bell."

Ni wapi unaweza kumfananisha LE na Cassius na ni nani wakati utakapofika atasema:
"Et Tu Brute..."

Hiki ni kitendawili ambacho muda pekee ndiyo utaweza kukitegua.



 

Naam! lakini pia anaitumia vema taaluma yake ya Uigizaji. Ndo fani alosomea pale mlimani. Alisoma shada ya Theater and performing Art.

Mungu wangu kumbe EL kasoma shahada ya theatre and performing arts aisee île si niyamaigizo igizo basi kumbe anafaa kuwa prezdaa nchi yenyewe hii ya kisanii sanii full usanii tu
 
Back
Top Bottom