Sheikh Ponda yuko sahihi

mimi ntajiandikisha kama muislam maruhani
 

...mkuu,sidhani kama kuna anaeogopa kujua asilimia,but the isssue is itatusaidia nn kwny kuleta hayo maendeleo?yes mnataka kujua mbona ni rahisi sana kufanya wenyewe bila kusubiri serikali iwafanyie km ambavyo wakristu wanafanya!sidhani km serikali itawakataza kufanya wenyewe!....hizo nchi ulizotaja kuna waislam wengi,yes,ni sawa na zambia,italy,uingereza n.k.....nazo zina wakristo wengi!..bt in reality hata mkihesabiwa, the fact is wakristo ni wengi kuliko waislam,kumbuka hapa unaongelea madhehebu mengi sn ya kikristo na c RC
 

MFUMO KRISTO!!!Mzee nimipenda hilo NENO. Cha msingi waislam kama wanasem inchi inaongozwa na mfumo JESUS kwa nini wasiandamane ili wampinge RAIS WAO MWISLAM wamuulize mzee mbona UMEOKA kuwa mkristo maana yeye ndiye Amiri jeshi mkuu wa huo wanaouita mfumo kristo TENA HATA MAKAMU WA RAIS KATOKA HUKO MFUKO KRISTO ULIKOSHAMIRI SANA YAANI ZANZIBAR
 

Kwa hali hii tunakokwenda hata makabila makubwa nchini yataomba kiongezwe kipengele cha ukabila ili tujitambue kwa makabila yetu.Na katika hili, wapo watakaosema kuwa wasukuma ni wengi sana lka ni wachache TRA, wakwale wachache na wametoa RAIS, na waha nao watadai kuwa ni wengi na hawakupelekewa shule. PLEASE wanajamii forums, sensa ni kwa maendeleo ya nchi yetu.Kitendo cha kuanza kujua ni waislam au wakristo wangapi nchini kinachochea udini Tanzania. Nia ya serikali ni nzuri na katika hili kuna jambo nyuma ya Pazia ambalo si jema.
 
Hivi kule serikalini kuna mambo ya ibada? Na Wasukuma kwa wingi wao katika nchi nao waje juu kutaka uwakilishi sawa serikalini kulinda maslahi ya desturi na mila za kisukuma. Kwa mwendo huu tutafika? Panapotokea tatizo na hata kama pale dini inahusika tulizungumze mahususi kama lilivyo na kulitatua na kusonga mbele. Haya ni maoni tu kwa mtazamo wangu.
 
Vyovyote nitakavyoonekana, lakini suala la kujua mgawanyiko wa watu kiimani (tuite dini) ni moja ya madhumuni makubwa ya sensa.
 

Kwangu mimi nikibainisha msomi ninakusudia ,Msomi si kuhudhuria au kumaliza skuli tu BALI KUSOMA NI KUELIMIKA. kUMBUKA KUWA MSOMI NI YULE aliyeweza kuyamiliki na kuyatambua mazingira yake na kujua haki na wajibu wake wa kuumbwa kwake na kukemea kwa nguvu zake zote aina yoyote ya dhulma na batili na kusimamisha haki daima.

Lakin vile vile Nje ya Muungano hakuna tena Tanzania bali kuna Tanganyika na Zanzibar. Na kwa mujibu wa historia za ukoloni nani ya EAfr. Utaona Ndani ya Kenya na Uganda kuna Ukabila. Na ndani ya tanganyika kuna UDINI. Hivyo katika Tanganika kuna Ukristo na Uislam kitu ambacho mlikificha siku nyingi saaana na sasa kinawameng'enya.

Je ulisikia kauli ya Mtei kuhusu tume iliyoteuliwa ya Katiba.

Je umeipata kauli ya Bakwata kuhusu Sensa,
Je umesikia madudu ya baraza la mitihani kuhusu dhulma iliobainika kwa waislam.

 
Ni nani alikwambia kuna maeneo yanatengwa maalum kwa ajili ya misikiti au makanisa? nadhani wahusika huwa wanajipanga na kuomba eneo kunako husika, ndo maana misikiti na makanisa siku hizi yapo kila mahali
Mkuu kwenye maeneo yaliopimwa nadhani huwa wanapanga maeneo kabisa kwa ajili ya nyumba za ibada. Sijui kama siku hizi utaratibu umebadilika lakini ilikuwa hivyo enzi za mwalimu
 
Wasukukuma tuko kama 8m ambayo ni 20% ya Watanzania. Vipi hilo Sheikh Ponda from Burundi?

ha ha ha ha ha ha ha sasa huyu Mrundi nae bana anapiga kelele za nn??Mbona waisilamu kibao tu tumesoma nao na wengine tunapiga nao kazi tu kama mtu kilaza unataka Baraza la Mitihani au Mwajiri amuwezeshe afaulu bure bure??
 

Mkuu unaposema "waislamu" maana yako ni nani. Kuna watu wanajiita masheikh ambao wanachochea vurugu na kuwarubuni watu, kuna watu wanaojiita waislamu ambao wanasema Tanzania inafuata mfumo wa kikrosto wakati hata amfumo wa kikristo hawawezi kuueleza ni upi, kuna wengine wanajiita waislamu lakini ukiangalia unaona wao ndio wanaongoza kula kiti moto, kuna wengine hata shule wanazitakaa wanasema ni za kikristo (wana akili kama za bokoharm kwa elimu ya Ulaya ni haram), wengine mafisadi, wezi, wachochezi....wote hawa niliowataja hawapo kwenye kundi la waislamu. Maana waislamu wa kweli ni watu wa amani, ukweli na upendo. NI waislamu gani hao unaowasema?
 
Nyerere alisema Tanzania haini dini kwa maana ya serikali ,na sense na kwa ajili ya kujua kuna watanzania wangapi na umri wao sasa hili la dini linakujaje hapa sisi tuna hesabu watanzania hapa na si vinginevyo kama kuna dini yeyote wanataka kujijua ni mko wangapi anzisheni daftari lenu la usajili kwa gharama zenu wenyewe mtapata idadi yenu .
 
kwani ni kweli kila nchi inayofanya sensa inaweka kipengele cha dini? Nisaidieni hapa kidogo wadau...
 

Mkuu najua kuwa Zanzibar ni Unguja + Pemba, na na si sawa na makabila ya huku bara, unless you educate me now that upemba na uunguja, ni sawa na uhaya, usukuma na uchagga huku bara. Najua pia kuwa Zanzibar inakuwa Zanzibar pale swala la bara linapoingia, au lile swala la chako chetu, changu changu.

Jaribu kutafuta nyaraka yoyote inayoweza kukwambia Tanganyika iko wapi, inatambuliwa na nani na inaishi kwa sheria ya nani, hapo ndio utajua kama hiyo nchi unayoiita Tanganyika ipo. Wanaozungumzia ile iiliyokuwa inaitwa Tanganyika huku bara ni makaburu, na ndio maana unaona hakuna anayewakubali, ni wabuguzi na waliokosa ubinadamu. Kuna watu wengi Tanganyika wanaisikia vitabuni tu, hiyo kitu haipo ndugu. Nilizaliwa Tanzania asili yangu ni tanzania, mimi ni mtanzania.
 
Mnaobeza haya Maneno inaonyesha hata uwezo wenu wa kufikiri ni mdogo au pengine hamkutani na wageni wanaotoka nchi za kigeni kwa sababu wao siku zote huulizia maswali kama, KUNA DINI NGAPI, DINI ZIPI NI KUBWA NA PIA IDADI YA WAUMINI WA HIZO DINI wanatengeza idadi ya watu wa nchi hii

TAZAMENI HILI SWALA BILA KUANGALIA DINI ZENU, jiulize je wewe MPAGANI HUTAKI KUJUA NYIE MKO WANGAPI?
 
]Kauli ya Ponda inazungumzika kwa maslahi yetu zote bila kujali tunakubaliana naye au hatukubaliani naye si jambo la kututengenisha bali kujenga hoja kushawishi umuhimu na ubaya wa kuwa na kipengere cha dini katika sensa.


[/COLOR]
Ni maoni yangu kwamba ni upuuzi na upumbavu uliopita mipaka kulazimisha jambo ambalo kimsingi maslahi yake ni machache kama hayapo kabisa. Dini ina maslahi gani mpaka tumbambue kilammoja kwa dini yake?? Sensa inatka kujua mwanamke, mwanaume ili kujua kwamba tupange mfano maswala ya uzazi wa mpango lakini DINI?? Mimi sioni, leo kuna watu kibao wanahama kutoka dini moja kwenda nyingine na hili si swala la serikali, na je takwimu zitakzo patikana leo si zitakuwa za uongo? Pia wewe unasema ni vizuri kulijadili sawa sasa Shekhe Ponda anajadili au analazimisha?? Afya ya majadiliano ni wengi wape wachache wasilikilze. Huwezi kwenda kwenye majadiliano huku ukisema kama langu halifuatwi TUNAGOMA. Jamani choko choko hizi hazitatuacha salama. Tuna umaskini wa kutisha mbona hatulazimishi haya ya kuondoa ufisadi??? EEE MOLA TUEPUSHE NA KIKOMBE HIKI
 

Mkuu Waislam kama Watanzania na walipa kodi wana haki ya kuhesabiwa na serikali ambayo aina dini.
 

ASANTE Mkuu coz wanaeropoka tu wakidhania ule mkakati wao wa kuzaliana kwa hali na mali ushafanikiwa na ndo maana walikua na mkakati wa kujenga misikiti hata maporini (Tazama njia nzima tokea morogoro hahi Iringa utagundua hili) kwa msaada wa OIC.....
 
Kuna nchi kama sierra leone ina muslim majority lakini its one of the most religious torelant nation na ikiwa na rais mkristo so why do muslims have to complain always mbona huko wakristo hawalalami afu isitoshe dini zenYEWE ZA KULETEWA
 
Mkuu kwani mnatishwa na nini si nanyie mtajijua exactly mko wa ngapi sasa hii ya kuwatisha inatokea wapi?Nina hakika hata nyie wakristo hamna idadi sahihi ya waumini wenu sijui kitu gani mnogopa jamani.Au dhuluma zenu ndo iakuwa mwanzo wa kwisha tehe tehe natania.
 
Well said, mie sina shida kabisa na kipengele cha dini kuwekwa kwenye sensa bali hiyo sumu ya kuwa Tanzania inaendeshwa na mfumo kristo nahisi ni kali na ngumu kusafishwa kwenu.
Kwenye swala la ajira mfano hiyo sekta ya afya huo ubaguzi wa dini unaoongelea nasikia kwako. Labda kuanzia sasa ingekuwa vyema kwa serikali iwe ina data base kwa watu wanao-apply post flani ili hata hao waislam wachache waliokosa kazi wasisemee mioyo ya wengine kwa kisingizio cha udini. Mana imekuwa hulka ya kwenu kulalamikia hampati kazi au hampati fursa flani ilihali hata hamwombi. Pia ni vyema nyie kama taasisi baada ya kujua idadi ya waumini wenu kupitia sensa kwa mfano kama ni 64% kama mlivyo speculate itakuwa bora pia mfanye sensa ya ndani kujua proffessional people within you and illiterate. Baada ya hapo kufikiria hatua gani mtachukua ili kuwasaidia hao ambao hawajasoma ili kuingia kwenye soko la ajira.....ni vyema viongozi msiwe wabinafsi kama mmeamua kuwasaidia waumini wenu na sio kulalamika tu. Au pia mnaweza mkawauliza makafiri wao wanafanyaje kuhamasisha waumini wao wasome.
Mfano mie nafahamu kuna makanisa flani wamejiwekea mikakati ya kuwa ili kusoma mafundisho ya dini ya kikristo mtoto anatakiwa awe amefika darasa la 5 na awe anajua kusoma na kuandika, huoni hapo inahamasisha mapokeo yote ya elimu.
Nimesema haya yote pia ni kwa nia ya kuendeleza kizazi kijacho chenye possitive attitude, hivi imagine kwa mtoto wa kiislam ambaye atakuwa legelege na shule mnahisi matamkomboa au atakuwa na notion kama "haina haja hata na hivyo hata nikisoma sana mwisho wa siku ntafelishwa au hata nikipita sitapata kazi mana wanaopewa ni wakristo sababu ya mfumo wao waliojiwekea serikalini"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…