Sheikh Ponda yuko sahihi

juzi Sheikh Ponda Issa ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Kutetea Haki za Waislamu alitanabahisha kuwa iwapo serikali haitoweka kipengele cha dini katika fomu za sensa ya mwaka, jumuiya yao itahamasisha Waislamu wasishiriki katika zoezi la sensa.Alisema kuwa nchi hii siyo ya Kikristo lakini INATAWALIWA NA MFUMO KRISTO. alisema kutokana na mazoea, Waislamu wanabaguliwa katika mgawanyo wa keki ya taifa khasa upande wa ajira. ofisi na idara za serikali zinaongozwa na Wakristo kwa asilimia kubwa kulinganishwa na waislamu. alitoa mfano wa TRA, NECTA, Wizara ya Eimu, Wizara ya Ujenzi, Afya, Mahakama nk........... kwa mujibu wa Sheikh Ponda, wastani wa ajira ni karibu Wakristo 77% na Waisalmu siyo zaidi ya asilimia 20%. Licha ya hoja inayojengwa kuwa Waislamu hawajasoma lakini akasema waliosoma wapo. akatanabahisha kuwa kwa maslahi na umoja wa kitaifa, kupuuza watu ambao ni sehemu ya jamii ktk keki ya taifa ni jambo hatari sana! kwa kuwa wtu wanadai waislamu ni chini ya 20% katika nchi hii, akapendekeza sensa ya mwaka huu kiwekwe kipengele cha dini ili idadi ya watanzania kidini ijulikane. Kwa mujibu wa Sheihk Ponda, anaamini kuwa waislamu ni takriban 64% ya rais wa Tanzania. "SIYO SAHIHI WATU WENYE IDADI HII KUPUUZWA KATIKA UWIANO WA AJIRA SERIKALINI", alisema Sheikh Ponda.Alitoa mifano wa nchi karibia zote za Ulaya, Marekani, asia pamoja na Afrika, kipengele cha dili kipo kwenye fomu za sensa zao. "Ukisoma country profile au fact file uingiapo katika nchi mbalimbali, utakuta wameandika wastani wa idada ya raia kidini" alisisitiza Ponda. "Mbona mnajifanya kama hamtembei au hamjui kinacho endelea ulimwengunu jamani!" alilalama Ponda.HOJA YANGUNdugu znaguni Watanzania, tufike sehemu tuache ukweli udhihiri. kama Waislamu wanalalamika kuwa wanabaguliwa katika ajira labda kutokana na uchache wao, kwa nini suala la dini lisiwekwe wazi? au utakua udini? au uchochezi? au uvunjifu wa amani? kama ni hivyo, mbona karibu 98% ya sensa zote duniani zina kipengele cha dini!? je huko wameuana kutoakana na kipengele hicho? TUBADILIKE!!!!!!!!naomba kuwasilisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Naona hii habari yako umechanganya habari. Unataka kutuaminisha kuwa, kuhusu keki ya Taifa huwa inagawiwa kufuata dini? Pia unataka kutuaminisha kuwa Dini ndiyo interview ya kupata kazi? Badala ya kung'ang'ania kazi za upendeleo maalumu, ningeshauri watanzania tujikite kwenye elimu kisawasawa kwanza na kipigania mazingira ya elimu.
 
tatizo la waislamu nadiriki kuwaita wengi ni vilaza
kutwa kulalamika. niwaulize mkuu wa nchi ni nani, makamu wake, jaji mkuu???wakristo hao?
wanataka wapewe mgawanyo sawa wa madaraka nani aliwaambia nchi hii ina dini? wanataka kutupeleka wapi?
wao wanakaa vijiweni na kunywa kahawa na walikataa kusoma shule za wakristo eti ni makafiri sasa wanataka wapewe vyeo bila kusoma? wamuulize JK alisoma shule ya watu gani? angesoma madrasa na kuishia kunywa gahawa leo angekuwa rais?
suala la ukabila na udini Nyerere alilikataa siku nyingi sana

pili wakubali kwa Tanzania asilimaia 62 ni wakristo, 35 ni waislamu na 3% ni watu wa dini zingine. kwa hivo tukiamua leo wakristo hata kupiga kura bado tunaweza kuwapita kwa mengi na pia idadi kubwa ya wasomi ni wakristo, nakumbuka nikiwa chuo kati ya wanafunzi 240 darasani 40 tu ndi walikuwa waislamu. acheni kelele pelekeni wanenus shule.
sijaona mantini ya wao kulalamika,
katika kazi hatuajiriwi kwa kigezo cha udini wala ukabila bali ni elimu na ujuzi wako.
 
Halafu wakokotoe kwenye idadi itakayopatikana ya watanzania wote ili wajue waislam ni roughly asilimia ngapi ya population ya tzii
katika imani ya kiislam imebainisha wazi kuwa tofauti ya muislam na yule asiyekuwa muislam ni kuswali mara tano kwa siku......kwa hiyo kama wewe huswali basi wewe ujue siyo muislam....sasa kama tuna imani ya kweli ya dini sijui kama hii sensa itasaidia vipi kwa waislam wao binafsi nadhani sensa nzuri ya waislam wa kweli ifanyike misikitini japo nadhani haitakuwa sahihi kwani siyo lazima sana kuswali misikitini
 
Hizo takwimu zitakataliwa,watadai mfumo Kristo umezichakachua! Maana wamekua wanajidanganya kwamba wao ni wengi,bila kutumia akili tu ya kawaida kwamba ktk mikoa 10 yenye wakazi wengi Tanzania,takribani yote inakaliwa na Wakristo. Kwamba mikoa kama Pwani,Lindi na Mtwara ni kati ya mikoa yenye idadi ndogo ya watu ktk Tanzania!
Halafu wakokotoe kwenye idadi itakayopatikana ya watanzania wote ili wajue waislam ni roughly asilimia ngapi ya population ya tzii
 
Kauli ya Ponda inazungumzika kwa maslahi yetu zote bila kujali tunakubaliana naye au hatukubaliani naye si jambo la kututengenisha bali kujenga hoja kushawishi umuhimu na ubaya wa kuwa na kipengere cha dini katika sensa.
 
katika imani ya kiislam imebainisha wazi kuwa tofauti ya muislam na yule asiyekuwa muislam ni kuswali mara tano kwa siku......kwa hiyo kama wewe huswali basi wewe ujue siyo muislam....sasa kama tuna imani ya kweli ya dini sijui kama hii sensa itasaidia vipi kwa waislam wao binafsi nadhani sensa nzuri ya waislam wa kweli ifanyike misikitini japo nadhani haitakuwa sahihi kwani siyo lazima sana kuswali misikitini

Na wanaoua wenzao bila sababu yoyote nao inakuwaje? Siamini kama hao nao wanatimiza masharti ya dini. Maana kama kigezo ni hicho kimoja tu, watu watajipa uhalali wa kufanya hata mambo haramu na kuamini watafika kwa Mwenyezi Mungu....tafadhali nieleweshe mkuu
 
ahsante mwongozo kwa taarifa hii.
Nakufagilia sheikh ponda, hayo uliyosema ni kweli tupu. Nafurahi pia kusikia mkutano wa jana wa sensa dodoma waislamu wote pamoja na bakwata wamekubaliana kususia sensa ya mwaka august 2012 kama kipendele cha dini hakitakuwepo kwenye fomu ya sensa. Cha kushangaza zaidi maaskofu wao wanataka kipengele hicho kisiwepo ati kitahatarisha amani. Amani itaharibika vipi ikiwa tutajua idadi ya waislamu wangapi na wakristo wangapi? Maaskofu walishindwa kujibu swali hili!!!!!! What is behind the scene maaskofu??? Kuna jambo gani limejificha hapa mpaka hamtaki tujue idadi yetu kutokana na dini zetu?!!
Acheni ulimbukeni ndugu, ikiwa mnataka kujua mko wangapi ili kudai uwiano katika ajira je na makabila, kwa mfano Wasukuma nao wadai hivyo? Wahaya na wachaga nao wadai uwiano wa kikabila? Ni mtu mbumbumbu asiyeweza kuona hatari mbele na kushabikia ujinga wa namna hii
 
Ninacho kiona kwa huyu Sheikh na wengine wenye mtazamo kama wake ni kutaka kila kitu cha dini yake kifanywe na serikali, mfano, wanasema Mahakama ya Kaadhi ni sehemu ya ibada yao lakini igharamikiwe na serikali, hivi inaingia akilini serikali igharamie ibada ya dini? mara uongozi uwe wa kuachiana, wa dini hi kipindi hiki na kipindi kingine dini nyingine, sasa hapa kuna mtego wanataka kuutega, issue hapa wanataka kujua Waislam wako wangapi? mi sidhani kama ni hii ni kazi ya serikali, hi ni kazi ya masheikh kama yeye, conduct your own Censor ili mjue mko wangapi? Ninahakika kama Kadinari Pengo anataka kujua kuna wakatoriki wangapi hapa nchini, ni yeye kuwasiliana na maaskofu wake ambao nao watashuka kwa mapadre then atajua tu wako wangapi, hali kadhalika Anglican, Lutheran Walokole kwa madheebu yao the same, hivi nyie waislam mnashindwa nini kufjua idadi yenu hadi serikali iwafanyie?

Kigezo kwamba dini zingine zinafanyaje nadhani si issue, kuna serikali humu duniani zina sheria ya kuruhusu mashoga, je na siye tu copy toka kwao? kuna nchi waislam hawaruhusiwi kuvaa Hijabu, tukopi na hiyo pia? Hebu tuwe realistic na masuala common na muhimu kwa nchi yetu, umasikini ni mkubwa sana Tanzania ambao kimsingi haungalii dini ya mtu, tuwekeze nguvu zetu huko, mlitaka rais mwislam, naye mmempata then mnakuja na story nyingine, ninahakika mkikubaliwa hili na la Kaadhi, kesho mtasema kuhiji Makka ni ibada, serikali iwagharamikie.
 
hivi ktk ajira mliona mtu akiulizwa jina,au elimu na uwezo wake ndio vigezo!!
kama dini fulani ina wasomi wachache kwenye soko wekezeni zaidi ktk elim=suluhisho la mda mrefu
tatizo la watz tunapenda vitu vya haraka haraka na pia fanyeni sensa zenn misikitini,mahekaluni, matambikoni na makanisani
napinga hoja za udini na ukabili ktk sensa
 
Kuna kitu kimejificha hapo.

Mbona mkiwa mnatoa maelezo Polisi mnaandika sio tu kabila mpaka dini mnabainisha. Kwenye vitabu vya wageni hotelini na nyumba za kulala wageni mbona kunakipengele cha dini na kabila. Kwanini msikiweke hata kwenye sensa zenu.

Nafikiri kiuchumi wanazuia kuona ni misada au misamaha ya kodi kiasi gani wanayopata dini moja dhidi ya zingine na kunufaika kwa namna gani kiuchumi dhidi ya wengine.

Kuna mengi sana . Lakin msingi mkuu ni mipango ya nchi yenu kuweka usawa wa kitabaka na kijamii kwa kupata taarifa sahihi ndani ya sensa.
Nadhani huko ulikotaja wanataka taarifa hizo ili kumtambua mtu iwapo tatizo lolote litatokea ili iwe rahisi kufahamu mgeni au mhalifu huyu ni nani hasa. Lakini katika mipango ya taifa hilo la dini na kabila halina mashiko hata kidogo
 
Barubaru,
Kwani namba ya waamini wa dini yako, hata kama ni kubwa ina faida gani kwa uwepo na ustawi wa Taifa hili? Kama namba ni tija, waafrika tulivyo, tunaweza kuanzisha mashindano ya kuzaana bila utaratibu, bila kujua kwamba anayeongoza dunia ya leo sio kwamba ana namba kubwa, la hasha!!! Ana elimu, uwezo na ujuzi mkubwa.
Ndio maana waisrael kwa idadi ni wadogo lakini pale walipo waliwahi kupigana na mataifa karibu yote yaliowazunguka kwa wakati mmoja na kuwashinda. It was not by chance....it was by design and intelligence to come with victory. So hoja hapa kwetu sisi wengine ni kuhakikisha generations zetu zina aim higher kwa kutafuta mambo ya msingi yatakayotusukuma huko. Sio haya mambo ya kujua nani ni dini gani! So what?

Idadi ya watu ni muhimu ktk taifa lolote ujitaka kujua faida yake angalia China na inavyokuja juu kiuchumi. Resources zilizopo Tanzania zinaweza kutosha Africa nzima kama zikitumiwa vizuri na kukawa na ktk ugavi muhimu ni kujipanga tu. Kuhusu dini ni muhimu kujulikana kwa sababu karibi million
 
Ninacho kiona kwa huyu Sheikh na wengine wenye mtazamo kama wake ni kutaka kila kitu cha dini yake kifanywe na serikali, mfano, wanasema Mahakama ya Kaadhi ni sehemu ya ibada yao lakini igharamikiwe na serikali, hivi inaingia akilini serikali igharamie ibada ya dini? mara uongozi uwe wa kuachiana, wa dini hi kipindi hiki na kipindi kingine dini nyingine, sasa hapa kuna mtego wanataka kuutega, issue hapa wanataka kujua Waislam wako wangapi? mi sidhani kama ni hii ni kazi ya serikali, hi ni kazi ya masheikh kama yeye, conduct your own Censor ili mjue mko wangapi? Ninahakika kama Kadinari Pengo anataka kujua kuna wakatoriki wangapi hapa nchini, ni yeye kuwasiliana na maaskofu wake ambao nao watashuka kwa mapadre then atajua tu wako wangapi, hali kadhalika Anglican, Lutheran Walokole kwa madheebu yao the same, hivi nyie waislam mnashindwa nini kufjua idadi yenu hadi serikali iwafanyie?

Kigezo kwamba dini zingine zinafanyaje nadhani si issue, kuna serikali humu duniani zina sheria ya kuruhusu mashoga, je na siye tu copy toka kwao? kuna nchi waislam hawaruhusiwi kuvaa Hijabu, tukopi na hiyo pia? Hebu tuwe realistic na masuala common na muhimu kwa nchi yetu, umasikini ni mkubwa sana Tanzania ambao kimsingi haungalii dini ya mtu, tuwekeze nguvu zetu huko, mlitaka rais mwislam, naye mmempata then mnakuja na story nyingine, ninahakika mkikubaliwa hili na la Kaadhi, kesho mtasema kuhiji Makka ni ibada, serikali iwagharamikie.
Sensa ya mwaka 1967 ilionyesha kuna wakristo wangapi, waislamu wangapi, na wapagani wangapi. Tunaweza kuanzia hapo. Mambo ya kuhesabu watu kwa dini zao hayana tija katika serikali ambayo haina dini.
 
Naunga mkono hoja na Waislaam wote tususe sensa, kwani itakuwa nini? Amma waweke hicho kipengele halafu wakachezee kompyuta kama walivyofanya mitihani wa Waislaam amma sensa tuisusie.
 
Akina Ponda wapo hata ktk nchi za Kiislamu,wengi wao wanaozea jela kwasababu ya kupandikiza chuki na mifarakano ktk jamii!
 
Nadhani hii ni busara kwani muanisho huu wa kipengele cha dini ni muhimu hasa kukiwa na mipango inayohusu dini.. kama kujua tunahitaji kutenga ardhi kiasi gani kwa ajili ya misikiti/makanisa... au makaburi

It doesn't make any sense
 
ahsante mwongozo kwa taarifa hii.
Nakufagilia sheikh ponda, hayo uliyosema ni kweli tupu. Nafurahi pia kusikia mkutano wa jana wa sensa dodoma waislamu wote pamoja na bakwata wamekubaliana kususia sensa ya mwaka august 2012 kama kipendele cha dini hakitakuwepo kwenye fomu ya sensa. Cha kushangaza zaidi maaskofu wao wanataka kipengele hicho kisiwepo ati kitahatarisha amani. Amani itaharibika vipi ikiwa tutajua idadi ya waislamu wangapi na wakristo wangapi? Maaskofu walishindwa kujibu swali hili!!!!!! What is behind the scene maaskofu??? Kuna jambo gani limejificha hapa mpaka hamtaki tujue idadi yetu kutokana na dini zetu?!!
Na maaskofu walikuwepo kwenye mkutano wa waislamu? wakaulizwa juu kipengele hiki wakakataa wakasema KITAHATARISHA amani!! Kuna kazi!!
 
Baada ya mauaji ya kimbari Rwanda walijua hatari ya 'ukabila' kwenye mustakabali wa taifa. Wameondoa kipengele cha ukabila kwenye mambo mengi sana. Tanzania tunaweza tusiwe na tatiza la ukabila lakini 'udini' unaanza kutunyemelea na sasa watu kama Sheikh Ponda 'wanatumiwa' kupanda mbegu ya udini.

Kwa maoni yangu mtu yoyote anayetaka kujua waaumini wa dini fulani wako wangapi basi afanye hayo na waumini husika. Serikali ya Tanzania ijishughulishe na watanzania (walio na dini na hata wale wasio na dini). Sheikh Ponda awafuate hao wafadhili wake wampe hela ya kuzunguka kila msikiti ili apate idadi ya waislam, au azunguke kila kanisa, temple na kupata idadi wa waumini. Lakini sio kutuelea hoja ambazo hazijaenda shule.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom