Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,226
Ningependa kupata mfano mzuri wa jinsi waislam wanavyobaguliwa kwenye ajira. Hivyo naomba mtu anipe data kamili, Sheikh Ponda ana ujuzi/elimu gani na aliomba/ameomba ajira wapi na majibu yalikuwaje? Pia mtu anayejua Sheikh Ponda amesomesha watoto wake (wa kuzaa) hadi kiwango gani, na sasa wanafanya nini? Hili litatusaidia kuelewa huyu sheikh anaongea nini.
Pili, lingekuwa jambo la maana sana kama tungepata profile (qualification wise) ya kamati ya Sheikh Ponda hasa wale walio mstari wa mbele kudai haki za waislam. Inawezekana tuna ma-profesa wa physics wanazagaa mitaani bila ajira kwa sababu ya dini zao!
Pole kwa kujikuta kwenye imani inayoona kila wakati inaonewa....
Na kila wakati inlazimisha mambo...
Pia haipendi maandiko yake yachunguzwe..
Hapo nilipo bold.... kama makanisa yanafanya sensa zao , kwanini nyie hamuwezi?
Kwanini mnataka msaidiwe na serikali?
Hivi hamna umoja kwenye nyumba zenu za ibada (misikiti) hamna network inayoweza kujua idadi yenu?
Kama kuna watu hawaendi misikitini hao achaneni nao, sio waislamu....
Hamna kinacho watisha watu hapa, ni kuwashangaa tu kwanini hawa watu hawawezi kujihesabu
wenyewe!!..wanajifananisha na walemavu wasiojiweza....!!! ujinga huu kwani walemavu wananyumba zao za ibada
wanazokutania?
....
Mkuu unatakiwa kujua kuchanganua mambo kwa mujibu wa hali halisi na elimu uliyopata. Ukiangalia nilichosema nimesema waislamu wa bara na waislamu wa Zanzibar, sikusema watu wa "Tanganyika" na wa Zanzibar, hata hao unaosema wazanzibar wengi wanaokwenda mlimani na kusoma ni wapemba, kwa hiyo kama tukiendelea na hiyo "sera" ya kijinga ya kuwagawagawa watu unaweza kuona kuwa ni wapemba na si wazanzibar ndio wanaosoma. By the way hakuna nchi inayoitwa Tanganyika, it does not exist in any form know to any intelligent person, it ceased to exist since the unification. And on top of that nimebahatika kufundishwa na finest professors kutoka Zanzibar na wanaoweza kueleza hali halisi kwa kuona na kwa usomi, si kama Ponda type.
Kama kweli wewe ni msomi ungejua kabisa kwamba Nationalists who disguise themselves in the blanket of religion are as evil as Nazis who disguised themselves in skin colour, hapo ndio suala la elimu linakuja. Na siku zote these kind of people are proven to be ******.
Hivi sensa kwa nchi kama
TZ inasaidia nini au imewahi kusaidia nini? nani anaweza kunipa mifano
hai?
Mkuu mtu mwenye mawazo kama hayo kazi pekee ana anayoweza kupata anaijua yeye, siwezi hata kumruhusu mtoto wangu kwenda kwenye madrassa anayofundisha mtu kama huyu, angekuwa na elimu angesema issues za maana.
Barubaru umeandika:
Kwa kuliangalia hili unahitaji AKILI ZA ZIADA KUANGALIA KWA MAPANA YAKE.
kWANI KIPENGELE CHA JINSIA KINA SAIDIA NINI KATIKA SENSA ZENU?
Nadhani tuweke rekodi sawa!
Kipengele cha jinsi ni muhimu kwa sababu mahitaji ya mwanamke ni tofauti na mwanaume. Akinamama huhitaji vitu mbali mbali wakati mmoja kila mwezi wakati wanaume hawahitaji. Wanawake wanabeba mimba na wanaume hawabebi. Je, Mkristo na Mwislamu wana tofauti gani? Je, si kesho Ponda anaweza kuwa mkristo na kesho kutwa akarudi kuwa mwislamu? Suala la imani au itikadi sioni kama ni mantiki kulinganisha na maumbile!!! Maumbile hayabadiliki na ni muhimu katika sensa wakati imani au itikadi hubadilika.
Nakusaidia vitu viwili.
1. Unaposema Znz unatakiwa ujuwe kuwa unazungumzia Unguja na Pemba. sasa wakiwa wapemba au waunguja lakin wote ni taifa moja na nchi moja nayo ni Znz. sawa na huko bara ukisema wahaya, wachaga, wamakonde wote hao ni miongoni mwa watanganyika.
2. Wewe ulizungumzia Uislam mna kunasibisha na ZNZ. mimi nimekupa takwimu sio tu za waislam bali za WaZnz wote dhidi ya Watanganyika wote iwe mkristu au waislam. Kumbuka ZNZ karibu 99.9% ni waislam. nilichotaka kukujuza kuwa usemi wako sio sahihi ndio maana nikakupa hayo kwa kuchanganya wwatanganyika wote na waZnz wote wasomi wengi wametoka Znz na hilo angalia hata baada ya muungano wenu 1964. wasomi wengi walikuwa wa Znz na hata wamiliki wakuu wa uchumi wa TZ takriban 78% ni wa Znz. Fuatilia nalo hilo utaliona.
Nilichotaka kukufahamisha Uislam unalazimisha watu kusoma na sio kuwa mbumbumbu ndio maana wote tu wasomi.
Mwisho nakusikitikia kwa kukaakana utaifa wako Utanganyika. Sie tuna usemi unanena MKATAA ASLI AKE NI ...
pOLE SANA
kwa akili yako fupi hapo UMEJIONA umetoa point ya maana kweli,hivi kuhesabiwa kwa watu kijinsi kidini una kuumiza wewe nini? Kwa kuwa munajua muta umbuka na takwimu zenu za uwongo,kwanini mtu wa kati (serikali isiyo na dini) wahesabie watu,
karibia nchi zote zinafanya sensa za aina hizi kwa sababu wanajuwa kuwa keki ya nchi inatakiwa igawanyike kisawasawa,lkn kwakua nyie munaegemea upande mmoja basi huona kuwa wasije waislamu wakashtuka,
kwa habari yako waislamu wamesha shtuka zamani na harakati hizi hazi kuanza leo wala jana, na zita endelea hadi mwisho wa dunia hii
kama unapenda kudanganywa kuwa waislamu ni dini ya kulalamika,basi nakuombea mungu akufungue akili za propaganda ulizo bandikiwa,
tuseme sote AMIN
Tuzungumze kwa reasoning. Hivi kama ingekuwa ni kweli kuna ubaguzi au hila za wakristo dhidi ya Uislam, wasomi wote wa kiislam na viongozi wote wa kiislam wameshindwa kuliona hilo mpaka walione akina Ponda wasio na upeo wowote? Hivi akina Kawawa, Aboud Jumbe, Rais Mwinyi, Salim Ahmed Salim, Rais Kikwete, Jaji Mkuu, Makamba (former katibu mkuu wa CCM), IGP, n.k. wote hawa wameshindwa kuuona huo mfumo gandamizi dhidi ya Uislam kiasi kwamba pamoja na kushikilia nafasi za juu kabisa za maamuzi wameshindwa kuuvunja? Huo mfumo unashikiliwa na nani hasa kiasi kwamba mawaziri wakuu, wakuu wa polisi, marais, wote washindwe kuugundua na kuuvunja? Yaani mnataka kutuaminisha kuwa Kikwete, Mwinyi, Said Mwema, Salim, hawakuwa waislam bali nao walikuwa wanatumikia mfumo wa kuwagandamiza waislam? Ukifika hapo ndipo unapoona watu wanaopiga hizi propoganda ni watupu wa dhamira na fikra. Mimi ni mkristo, nilisoma shule ya serikali, nikihudumiwa na mzazi mmoja baada ya kufariki baba yangu, nilipofika, najua hatua za taabu nilizopitia, sijawahi kufanya kazi ya serikali wala shirika la umma, watoto wangu wote hawajawahi kusoma shule ya serikali, wapo ndugu zangu ambao hawakumaliza hata darasa la saba, mbona huo 'mfumo wa Ukristo' sikuuona ukinisaidia wakati nikihangaika au kuwasaidia wale ndugu zangu ambao wengine hawakuweza kumaliza elimu ya msingi? Msaada pekee nilioupata kanisani ni mahubiri kuwa 'asiye fanya kazi na asile', na kwa lolote ulitendalo mtegemee Mungu, usikate tamaa maana Mungu humwinua yeye asiyekata tamaa. Maneno haya ndiyo wimbo wangu kwa watoto wangu leo. Mtoto wangu wa kwanza anasoma pale Feza, shule inayomilikiwa na Uturuki ambao 98% ya wakazi wake ni waislam, lakini kila mara ameweza kuwa wa kwanza darasani hadi kuzawadiwa U$1,000. Je, na pale Feza anapendelewa kwaajili ya Ukristo wake? Mnaozusha hizi tuhuma za kipuuzi mfikirie kwa makini. Tufanye kazi kwa bidii, daima tuwaambie watoto wetu umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii, kusoma kwa bidii kuliko kuwajaza ujinga wa kuwa wanaonewa. Matokeo yake wanajibweteka wakiamini kuwa kutofanikiwa kwao ni kwa sababu wanabaguliwa.
mheshimiwa kwanza ningependa upange maandiko yako kwa kuacha nafasi,ili tusome maelezo yako kwa makini na bila kuchoshwa na mpangilio,
mfumo kristo unaeleweka vibaya saana na upande wa wakristo hata baadhi ya waislam,ulivyo elewa wewe ni kuwa wakristo ni matajiri na waislamu ni maskini,wakristo ni bora kuliko waislam katika kila kitu,
rejea maana ya mfumo bila kuweka neno ukristo
mfumo kristo ni ule mfumo wa kuukuza ukristo(sio waumini) kuliko dini na makabila tofauti
siwezi kuwa laumu wafuasi wa dini kristo sana kwasbb nchi yetu imetawaliwa na wakoloni wakikristo na tumesha zoeshwa mfumo wa ukristo na kuona mfumo wowote nje ya hapo haufai,kwa sababu ya mazoea waswahili wasema mazoea yana .......
waislam naamini ni zaidi ya asilimia 50 na uwislamu ni dini (mfumo kamili wa maisha ya muumini wake) na sio imani tu ya kuingia msikitini nje ya msikiti uislam haupo,
tuchukulie mfano siku ya jumapili ni siku ya ibada ya baadhi ya wakristo na ikatengwa rasmi kuwa siku ya mapumziko kwa sababu ni siku ya ibada
lakini ukija siku ya ijumaa ni siku ya kawaida kabisa hakuna mapuziko kwaajili ya waumini wanao fanya ibada siku hiyo,
huu mfano unaonesha MFUMO KRISTO ambao umesababi shwa na utawala wa wakoloni wakristo na kuendelezwa na viongozi kwa kuendelea kufuata kanisa
sitaki kusema kuwa waislamu tupewe siku hiyo kwasbb tutakuwa na siku tatu kati ya saba ni mapumziko,ambazo ni siku nyingi kweli katika wiki.kwa nchi yetu hii MASKINI hatuhitaji siku nzima ya mapuziko isipo kuwa saa kadha za siku flani na flani kuwa siku za mapumziko,
BAKWATA waislamu sio waazilishi wa BAKWATA na bwakata mara nyingi imekuwa kimya kutetea haki za waislamu na kufanya vitu venye kuleta mgawanyiko baina ya waumini,
kwa kuwa serikali ni MFUMO KRISTO umeliunda hili baraza na kuliweka kuwa ni waakilishi wa waislamu ambao sio kweli kabisa,eti mfano mimi naanzisha baraka la kikristu alafu na chagua viongozi nao wataka alafu nainisha wazi kuwa hilo baraza litakuwa lina waakilisha wakristo wote,wewe unaona sawa?
Nimetumia mifano midogo midogo ili tujaribu kueleweshana kwa njia nyepesi,hapo sijaingia kwenye MOU
naamini wote tupo pamoja
Shida hata elites wa kiislam siyo msaada hata kidogo ktk kuwasaidia wenzao. Dunia nzima ni wao tu wenye chokochoko. MUNGU WAO HUYO sidhani kam ni wa VURUGU. Hata wangekuwa ni wao kwa wao (waislam) bado wangetafuta source ya fujo tu ona Yemen, afghanistan, pakistan, bahrein, iran, morocco,etc.
kwa akili yako fupi hapo UMEJIONA umetoa point ya maana kweli,hivi kuhesabiwa kwa watu kijinsi kidini una kuumiza wewe nini? Kwa kuwa munajua muta umbuka na takwimu zenu za uwongo,kwanini mtu wa kati (serikali isiyo na dini) wahesabie watu,
karibia nchi zote zinafanya sensa za aina hizi kwa sababu wanajuwa kuwa keki ya nchi inatakiwa igawanyike kisawasawa,lkn kwakua nyie munaegemea upande mmoja basi huona kuwa wasije waislamu wakashtuka,
kwa habari yako waislamu wamesha shtuka zamani na harakati hizi hazi kuanza leo wala jana, na zita endelea hadi mwisho wa dunia hii
kama unapenda kudanganywa kuwa waislamu ni dini ya kulalamika,basi nakuombea mungu akufungue akili za propaganda ulizo bandikiwa,
tuseme sote AMIN
Mfumo kristo ndio unaotawala nchi hii mtake msitake. Kwenye vyumba vya hoteli utakuta biblia! Kwa nini kusiwekwe korani? Kwenye vyombo vya usafiri kunapigwa kanda za injili kwa nini kusipigwe kaswida?
Kazi ndio msingi wa maendeleo, maendeleo ya watu yataletwa na kufanya kazi kwa ufanisi na nidhamu. Kuhusu kipengele cha dini kwenye fomu za sensa nakiafiki sana, pia kiwepo kipengele cha kiwango cha elimu chini yake, nadhani malalamiko ya mashehe, maimamu na maamuma wao yanaweza kupatiwa jibu la muda mrefu. Jaribu kufanya utafiti kidogo kwa makandarasi waliofanya kazi zanzibar wakupe uzoefu wao wa wachapa kazi wa huko. Kazini anaingia saa 3.00, saa 6.30 anaenda kuswali mpaka saa nane, saa 10.00 anaenda kuswali harudi mpaka kesho. Mwezi mtukufu wa ramadhani ndo balaa, akitoka saa 6.30 harudi mpaka kesho (swaumu). Mtasema tunawakashifu lakini tuseme kweli, mliona wapi binadamu akajikwamua toka katika umasikini kwa kufanya kazi masaa matatu kwa siku? Hata shule kusoma ndio style yao, wakifeli maandamano. Mungu baba muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo alifanya kazi ya uumbaji siku sita, siku ya saba akapumzika, akaibariki na kutuamuru tufanye kazi kwa siku sita ya saba tumwabudu na kumtukuza. Fanyeni kazi, acheni kushinda kwenye vijiwe vya kahawa na kulala misikitini kwa kisingizio cha kuabudu.
Sioni ubaya wa kukusanya takwimu zozote zile, ikiwa ni pamoja na idadi ya waumini wa dini au madhehebu. Ubaya au uzuri wa kukusanya takwimu hizo unategemea unataka kuzitumia takwimu hizo kwa nia gani, nia nzuri au mbaya? Kama unataka kupata takwimu yeyote ile kwa nia ya kuleta fitina, ubaguzi wa aina yeyote ile, basi hata tendo lenyewe la ukusanyaji takwimu hizo linakuwa haramu kutokana na nia ovu uliyokuwa nayo.
Shekhe Ponda (japo siamini kama ni shekhe kweli) ameshalifanya tendo lolote la kukusanya takwimu za waumini wa dini kuwa ovu kutokana na nia yake ovu. Nia yake kubwa ni kuleta ubaguzi wa kidini, kuwataka watu wagawanyike kidini, wafikiri kidini na watende kwa kuegemea dini zao. Anataka kuwa na Tanzania iliyogawika kwa misingi ya kidini. Ameishaweka wazi kuwa nia ya kupata idadi ya waumini wa dini ya kiislam ni kutaka kuwa na uwiano wa kiuongozi, ajira na kila jambo kwa kuegemea dini wala siyo mahitaji na uwezo wa raia wetu. Huyu ni mfitini mkubwa, na hapo ndipo unapoona ubaya wa demokrasia unapokuwa na watu waliojaa hila, uovu na dhamira mbaya kama akina Ponda. Angetaka takwimu hizo kwa nia nzuri, mimi ningemwunga mkono lakini kwa nia aliyoitaja, kamwe siwezi kuunga mkono udhalimu wowote unaolenga kuigawanya Tanzania kwa misingi ya dini. Huyu ni mpuuzi mkubwa. Waumini wa dini mbalimbali wanapenda na wana haki kujua idadi ya waumini lakini iwe ni kwa nia iliyojaa utakatifu. Anachokifanya Ponda, madhara yake kwa jamii, ni aheri ya kuwa na jambazi kuliko mtu wa namna hii.