mi napendekeza waweke huo udini wao, ili tufuatilie nyendo zao. nimechoka na kelele zao. kuna mmoja alitoa ufafanuzi kuwa, eneo la kiseke mwanza, maeneo ya huduma za jamii, wakati wakristo wametengewa zaidi ya hekata 1,000 kufanya shughuli za kijamii kujenga makanisa na mambo memngine yanayowahusu, waislamu wametengewa hekata 100 tu. sina hakika na takwimu hizi, lakini akasisitiza, kilichosababisha utofauti wa ukubwa wa maeneo, ni kwa kuwa serikali ina takwimu za idadi ya watu kwa kuzingatia dini zao kitu ambacho hakijawahi kufanyiwa kazi tanzania.
mimi nilimjibu nikamweleza kuwa, waislamu kuna madhehebu makubwa manne, wakati wakristo utahesabu madhehebu hadi utachoka. kiukweli sijui idadi ya madhehebu kwani yaliyopo si chini ya 50 kwa yale ninayoyafahamu. kwa hiyo iwapo kila dhehebu litaomba kiwanja huko kiseke, hata hizo hekata 1,000/ hazitatosha, lakini waislam kwa idadi ya madhehebu yao, wana uhakika wa kupata kila dhehebu hekta 25, ambalo ni eneo kubwa mno.
sasa kama wanahisi wananyanyaswa katika kugawa rasilimali za taifa, tuhesabiwe kwa dini zetu ili tuone mwishoni itakuwaje