Sheikh Ponda amezitoa wapi hizi takwimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Ponda amezitoa wapi hizi takwimu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ukoo Flani, Jun 29, 2012.

 1. Ukoo Flani

  Ukoo Flani Senior Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jumuiya na Taasisi za Kiislamu imepanga kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa na kupinga kauli iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu (Bakwata), Mufti Issa Shaban Simba, kwamba Waislamu wamekubali kuhesabiwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kauli ya Mufti Simba, inaashiria kwamba Bakwata limekiuka makubaliano yaliyofikiwa mjini Dodoma na jumuiya zote za waumini wa dini hiyo.

  Alisema kauli hiyo haitakuwa na athari kubwa kwa msimamo wa Waislamu wengi ambao hawatashiriki zoezi la sensa.

  "Waislamu tumepanga tarehe hiyo ya sensa kufanya maandamano ya amani nchi nzima kwani sensa inayokusudiwa haitakuwa na matokeo sahihi kwakuwa asilimia 80 ya Waislamu ambao ni zaidi ya nusu ya Watanzania hawatahesabiwa," alisema Shekh Ponda.

  Hivi karibuni Mufti Simba, alitoa msimamo wa Bakwata, akiwataka Waislamu wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.

  Chanzo: Nipashe

  Huyu Sheikh amezipata wapi hizo takwimu kwamba 80% ya Waislamu TZ ni zaidi ya nusu ya Watanzania wote? Halafu baada ya Sensa ya dini ikajulikana waumini wa dini fulani ndio majority italisaidiaje Taifa? Ninaamini kuwa wapo waislamu wengi Tanzania wasioyumbishwa na kauli na misimamo ya viongozi wao, lakini viongozi wa aina hii wana mchango gani kwenye ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla?
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  huo ndiyo muda mzuri wa kujifanyia sensa. kila atakayeandamana na ahesabiwe, mwisho mtajuwa mko wangapi.

  Boko Haram
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  mi napendekeza waweke huo udini wao, ili tufuatilie nyendo zao. nimechoka na kelele zao. kuna mmoja alitoa ufafanuzi kuwa, eneo la kiseke mwanza, maeneo ya huduma za jamii, wakati wakristo wametengewa zaidi ya hekata 1,000 kufanya shughuli za kijamii kujenga makanisa na mambo memngine yanayowahusu, waislamu wametengewa hekata 100 tu. sina hakika na takwimu hizi, lakini akasisitiza, kilichosababisha utofauti wa ukubwa wa maeneo, ni kwa kuwa serikali ina takwimu za idadi ya watu kwa kuzingatia dini zao kitu ambacho hakijawahi kufanyiwa kazi tanzania.

  mimi nilimjibu nikamweleza kuwa, waislamu kuna madhehebu makubwa manne, wakati wakristo utahesabu madhehebu hadi utachoka. kiukweli sijui idadi ya madhehebu kwani yaliyopo si chini ya 50 kwa yale ninayoyafahamu. kwa hiyo iwapo kila dhehebu litaomba kiwanja huko kiseke, hata hizo hekata 1,000/ hazitatosha, lakini waislam kwa idadi ya madhehebu yao, wana uhakika wa kupata kila dhehebu hekta 25, ambalo ni eneo kubwa mno.

  sasa kama wanahisi wananyanyaswa katika kugawa rasilimali za taifa, tuhesabiwe kwa dini zetu ili tuone mwishoni itakuwaje
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kazitoa kwenye kijiwe cha kahawa.....
   
 5. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  80% ya waislamu ni tofauti na kusema 80% ya watanzania ni waislamu. nadhani yeye alimaanisha ile ya kwanza. Ila kasema zaidi ya 50% ya watanzania ndio waislamu ikimaanisha kuwa asilimia ni kati ya 50%-59.5
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe ni dini ipi?
   
 7. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Hivi idadi kubwa ya waumini wa dini bila kuwa na uwezo kiakili inasaidia nini katika Dunia hii? Hivi idadi kubwa ya wapalestina imesaidiaje kuwaondoa katika makucha kandamizi na utwala wa waisraeli? Hivi bado hatuwaoni wamasai na wasukuma mtu mmoja avyoswaga kundi la makumi ya ng'ombe?
  Ndugu zangu tuache ujinga wakujitambulisha na kutengana kwa kufuata dini za wakandamizaji na wanyanyasaji. Kila siku najiuliza itakuaje babu zetu wale walio hasiwa kwenye bandari za bara Arab wakiamka na kuwakuta wakina sheikh Ponda na misimamo Yao ya KUWATENGA ndugu zao waafrika weusi na kuwakumbatia waarabu na dini yao?
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,836
  Trophy Points: 280
  Hivi cheo cha usheikh amepewa na nani? Sheikh ponda ameishia darasa la ngapi?

  Hivi huyu ni sheikh au muuni?
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Enzi zetu zile, huyu Sheikh angekuwa kwenye moja ya kisiwa kinachofikwa na "wavuvi" tu. Akirudi, sensa imeisha na hadi yeye amehesabiwa!
   
 10. G

  GRILL Senior Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii Nchi sasa kila mtu anajisemea la kwake huu uchokozi ipo siku watashindwa kuuvumilia na watatoka kama inavyostahili.
   
 11. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Izo Zama za Kutangaza Dini kwa kutumia Energy (nguvu) zishapitwa na wakati..hasitake kuwafanya waislam wote wajinga..Kama kweli Mshika Dini kwa asiendelee Mawaidha yenye kujenga Dini..

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 12. D

  DOMA JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Kwa nini msimpuuze mtu huyu
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nafikir sio jambo baya kujua idadi na sio kujua idadi tu bali ni kuweka takwimu za nchi sawa ,ili kujua majority ya idadi ya wenye dini na hata wale wasio na dini. Tunaelewa kuwa serikali yetu ni ya kipagani lakini utaona imeikataa OIC na kuikubali Vatican ,ni kosa la kikatiba nchi nyingi tu hata kwenye passport zao unaweza kuona sehemu inayokutaka kubainisha dini yako.NA KWA NINI JAMBO HILI LIKATALIWE KUNAOGOPWA NINI ? au ni sawa kama vile CCM wanacyokataa kuweka tume huru ya Uchaguzi inayoshirikisha wadau wote ??
   
 14. S

  SPANERBOY UDZUNGWA JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 623
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Vatican ni nchi . Je oic ni nchi?
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  When one wants to deceive people they try and convince them that their opinions are facts.
  Kama ameweza kujua kuwa 80% ya Waislamu ambao anadai ni zaidi ya nusu ya Watanzania anashindwaje kujua idadi ya Waislamu Tanzania?
   
 16. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wasipohesabiwa watapata faida gani? ujuha huo.
   
 17. T

  Tata JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,734
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa wanaojiita viongozi wa waislam hawana "seniority" kwenye uongozi wao? Inakuwaje Shehe Mkuu wa Tanzania anatoa tamko halafu Shehe mwingine ambaye siyo mkuu anapingana naye hadharani. Anachosahau huyu Ponda ni kuwa kuna watu wangependa sana sensa ionyeshe makabila ya watu ili tujue kabila gani ni kubwa kuliko jingine na raslimali zigawanywe kwa kuzingatia ukabila.

  Kama alifuatilia mjadala wa bunge jana kuna mbunge wa jimbo mojawapo la kanda ya ziwa alikuwa anahoji, pamoja na mambo mengine ya kijimbo, kuwa inakuwaje kanda ya ziwa pamoja na kuwa na raslimali nyingi haina mawaziri wa kutosha kwenye baraza jipya. Ninachosema hapa ni kuwa ukiruhusu sensa kwa misingi ya dini za watu hutakuwa na hoja ya msingi ya kuzuia sensa kwa misingi ya makabila ya watanzania. Kwa waafrika ukabila unawaunganisha watu kuliko udini na ni hatari sana kuchochea hilo kwa nchi yetu. Waafrika tunaamini zaidi katika ukabila kuliko udini na ndio maana siyo ajabu kumkuta mwafrika anaingia kwenye hizo dini za kigeni huku bado akendelea na imani zake za kijadi. Ukabila ni chanzo cha mauaji makubwa kwa majirani zetu - Kenya, Rwanda, Burundi, Conco n.k.
   
 18. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Akili za madrassa hizo! kulinganisha chungwa na nanasi! Vatican na OIC wapi na wapi? Ungeniambia Vatican na Iran ningekuelewa. Kwa akili hizi hata mkiwa 80% mtaendelea kuburuzwa tu na 20%
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,734
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Sio kila kinachofanywa na nchi nyingine ni sahihi kufanyika na hapa kwetu. Huo ni ukasuku wa kuiga mambo bila kujua msingi wake na faida zake kwa nchi yetu. Hakuna mtu anayeogopa kuhesabu watu kwa misingi ya dini, kabila, rangi, asili ya mtu, "sexual preferences" - kama ni shoga au wa kawaida na kadhalika. Haya ni mambo binafsi ya wananchi ambayo taifa halina haja ya kujua. Maswali ya msingi ya kujibu, ambayo kwa bahati mbaya hayajapata majibu ya maana, ni kwa nini tunataka kuhesabu watu kwa misingi hiyo? Je ni kwa maslahi ya nani? Je taifa litafaidika nini kwa kuhesabu watu kwa misingi hiyo? Je misingi ya taifa letu kama inavyoelekezwa kwenye katiba yetu inasemaje kuhusu suala la kuhesabu watu kwa misingi mingine yeyote zaidi ya utaifa wao?
   
 20. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Bora waende tu mahakamani ila kwa taarifa yao kwa sasa madodoso yapo tayari kwa hiyo hakuna mtu atakubali kuingia gharama kubwa ya kuaandaa upya kwani kuongeza swali moja tu kuna cost implication ya mamilioni ya shilingi
   
Loading...