Lakini pengine badala ya kulalamikia the apparent imbalance katika teuzi za mtukufu rais, twende mbele zaidi na kupendekeza solutions (naamini namna hiyo tunaweza kumsaidia zaidi rais):
- Je, tunaufahamu vizuri utaratibu (wa kisheria?) wa teuzi anazofanya Rais?
- Kuna vigezo ambavyo Rais (kisheria) analazimika kuvizingatia? Je vigezo na taratibu hizo zina uwazi kiasi gani? Kama hakuna vigezo je, isingekuwa vema kuweka vigezo na utaratibu ambao ni wa uwazi zaidi?
- Na je kama vigezo vipo, dini ya mtu ni mmoja wapo? Kama siyo, kuna umuhimu, sasa, wa kuweka dini kama kigezo kimojawapo au namna fulani ya kuhakikisha balance kati ya dini kuu zilizopo nchini? Hii itasaidia kutoa muongozo kwa Rais yeyote aliyepo madarakani kuhakikisha balance (kama ndivyo tunavyotaka).
Kwa upana wake, mimi nalitizama suala hili kama tatizo la kikatiba. Watanzania tulio wengi, inaelekea, bado ni 'wadini' (i.e. tunapenda kutizama/kupima mambo kutokea kwenye perspective ya dini). Hizi sentiments hata kipindi cha JK zilikuwapo (na yeye akituhumiwa kupendelea wa dini yake). Sasa kama hivyo ndivyo tulivyo, tuweke unafiki pembeni tu na tuweke mambo haya vizuri kwenye katiba yetu ili kutoa "haki" sawa kwa watanzania wote.
Kama kwa dhati kabisa tunaamini kuwa dini haipaswi kabisa kuzingatiwa (katika nafasi husika), then tunahitaji kuweka utaratibu mzuri wa kisheria ambao utaondoa au kupunguzauwezekano wa Rais kupendelea au kuonekana anapendelea dini au kabila au kanda fulani (tunaweza kuanisha nafasi ama vyeo ambavyo tungependa neutrality ya kiwango cha juu na tukaanza na hivyo). Kwa mfano tunaweza kuweka vigezo na pia kwa nafasi hizo zikawa za kuomba na kupitia mchujo wa wazi badala ya kuteuana (wenzetu Kenya wameanza vizuri tu....wao wana tatizo la ukabila zaidi kuliko udini).
Lakini ipo hoja inayotolewa na baadhi ya watu kuwa kwa sababu za kihistoria, dini fulani ina wasomi wengi zaidi kuliko nyingine (na hata makabila fulani yana wasomi wengi zaidi kuzidi mengine) na kwa hivyo kama vigezo ikiwa ni usomi na uzoefu, automatically dini au makabila yenye wasomi wengi yatakuwa na wateule wengi zaidi. Again, kama tunakubali hoja hii na tukiweka unafiki pembeni, tunaweza kuweka utaratibu wa kisheria ambao kunaweza kuwepo kwa affirmative action or positive discrimination (linafanyika hili kwa wanawake) kwa watu wa dini ama makabila tunayodhania hayana wasomi wengi (Kwa mfano kama kuna candidates wa dini mbili wote wanatimiza vigezo, anayetoka kwenye dini ama kabila "kandamizwa" apewe nafasi kwanza/upendeleo).
Lakini tujiulize pia kama mambo haya yatatuweka pamoja zaidi kama taifa au yatazidi kutugawa?