Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
Takwimu zako zinakupa picha ya uhaba wa fikra,kwa nafasi gan mpka walio na elimu ni wakristo waislam hawapo?hili jambo lipo wazi kbsa ishu sio utendaj ishu maagzo.
Wewe ni miongoni mwa wale wapuuzi wanaodhani propaganda za mwaka 90 zinaweza kufua dafu Tanzania ya leo.

Huo upuuzi wa kysema waislaam hawajasoma uishie kwenye jumuia ndogo ndogo.

Ukija humu njoo na tafiti kama livyofanya shekh
Kwa sababu za kihistoria katoliki wametawala tangu Uhuru na wataendelea sana kutawala
 
Mzee Mohamed,
Mada kama hizi ndio zimekufanya uonekane mwana HISTORIA. Ningeshangaa kama ungekaa kimya ikapita.
 
Watanzania wanataka kuona maendeleo ya haraka ktk kila sekta na sio kusikia mambo ya Udini!!
Watanzania wanahitaji kiongozi/viongozi wazalendo ambao watawatumikia kwa nguvu zao zote bila kujali dini!
KIONGOZI yeyote anye mbagua Mtanzania mwenzake kwa sababu tu ya dini yake, asiwe na nafasi na aondolewe haraka sana!
Unazungumzia maendeleo bila umoja?

Hivi Syria ya leo ina hata huo muda wa kujadili maendeleo?

Haki ikitamaliki amani huimarika na uchumi nao huota mizizi.

Acha chuki na spinning za kijinga za kujifanya huguswi na udini wakati hapo ulipo ulibebwa na dini yako na unanufaika na mfumo uliokuweka hapo
 
Mzee Mohamed,
Mada kama hizi ndio zimekufanya uonekane mwana HISTORIA. Ningeshangaa kama ungekaa kimya ikapita.
Kila msomi anaeneo dogo alilobobea,ndio maana kuna mtu kasoma botany tu,wengine Zoology,wengine Philosophy of history tu,wengine Archaelogy,wengine wamesoma historia za dini katika maendelea ya taifa,kila mmoja na eneo lake la ulumbi
 
Sheikh Khalifa Khamis ni sehem ya mfumo huuu anachokifanya ni sehem ya kazi yake

Wala hana athari yyt tangu hapo mpaka sasa

Hana tofauti na Mzee basaleh
 
mimi ni muislamu lakini hili la udini halina mantiki kwa mh. na sijaliona! mbona akina majaliwa na samia ni waislamu na hamjalalamika???
 
Kuunda serikali kuna uhusiano gani na DINI ya mtu Mzee Mohamed Said? Dini tuzitumie kuzikana, kufunga ndoa na malezi ya familia.
 
Lakini let's be fair. Kwanza nitamke wazi kuwa mimi ni mkristo. Pili nitamke wazi pia kuwa sifurahishwi na huu mwelekeo unaoonekana kwenye hizi teuzi. Haya mambo yalishaanza kukaa sawa, hisia za unyonge zilishaanza kuondoka, sasa tunarudi nyuma. Hakuna starehe yoyote unapopata kitu halafu wenzio wakasema umependelewa, kwa hiyo ili hizo hisia za upendeleo ziondoke ni lazima ionekane kuwa haki imetendeka, na hilo ndilo analopaswa kuzingatia kiongozi na wote wanaomshauri.
Siamini kuwa alishindwa kufanya balance, mbona wenzie waliomtangulia waliweza? Tangu enzi za Nyerere, tena hata wakati mwingine baadhi ya sifa alizifumbia macho kidogo ili kuwe na balance. Tena enzi ya Nyerere angelazimisha vigezo vya usomi angeweza kuteua hata wakristo 95% kwa sababu hali ya wakati ule wa baada ya ukoloni inaeleweka, wenzetu walikuwa wamebanwa zaidi, lakini alipokea ushauri na kutumia pia busara yake kujitahidi kuweka balance nchi ikaonekana ni yetu sote. Japo wenzetu baadaye walilalamika, lakini naona kama hii ya sasa mkuu huyu amebana kuliko awamu zote zilizotangulia.
Tumshauri au kumwomba awe msikivu, atazame raia wote kwa usawa. Pengine hajafanya makusudi, sina uhakika, lakini aelewe kuwa athari zinawafikia wote, hata sisi tunaodhaniwa tumependelewa hakuna tunachofaidi. Hata angeweka wakristo watupu serikali nzima, hakuna chochote ningefaidi, yaani hainifai kitu wakati kuna wenzangu, jirani zangu, classmates wangu, rafiki zangu wanakosa amani kwa sababu siku zote upendeleo una tafsiri mbaya. Atusaidie kuondoa hizi sensitivity, tunataka tuendelee kuishi kwa amani bila manung'uniko upande wowote, au hata yakitokea yawe ni yale ambayo kwa wazi kabisa yanaonekana hayana msingi, lakini kwa sasa huwezi kusema uwiano wa 137:16 au 185:36 (kama takwimu hizi ni sahihi) eti haina msingi wa kuhojiwa!

Jana tu wakati tunajadili ushindi wa Trump, rafiki yangu mwislam akaniambia "lakini wewe ni mkristo bwana huna neno, siye wenzio ndio hataki kabisa kutuona huko!" Kauli imeniuma sana maana binafsi sifaidiki chochote na chuki za Trump, na pia hata akiwachukia sana bado watabakia kuwa ndugu zangu na jamaa zangu, siwezi kuwatenga sababu eti Trump hawataki!

Tuwe makini na haya mambo yenye sensitivity. Ashauriwe vizuri mkuu wetu huyu. Natamani hata huyu sheikh awe na uthubutu wa kumfikishia mkuu huu waraka wake, na wakristo tuunge mkono kwa kusema kuwa hatutaki kupendelewa wala kudhaniwa tunapendelewa.
 
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.

Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.

Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.

Sasa hapo mbona ni ukweli mtupu?
 
kuna dini za wabaha'i hata hawajawahi kuteuliwa kwenye nafas hata moja huwezi kuwaskia wakisma chochote,kuna wahindu nk nyie mnamatatizo gani?
ushasema wahindu ...hao si watanzania..tanzania wazawa zipo dini mbili kuu...Uislamu na Ukristo..
 
huko huko ndege mpya bei za ticket... ukanda fulani bei chini japo ni mbali ila ukanda fulani japo ni karibu bei ndogo hii ndio nini sasa...chunguza utabaini
 
Km takwimu ndio hizo shekh khalifa anafaa kupongezwa kwa kuwakuwajulisha waislam maana wao wamekuwa wapiga kelele ndani ya chama lakini matunda wanakula wagala
 
Uchaguzi ule, ukiwa unayaangalia mambo kwa upana zaidi utaona kuwa ulikuwa ni mchuano wenye Factors nyingi, kwa jinsi ninavyoona, factor mojawapo ni Udini. Kulikuwa na kambi kuu tatu

1) Wakatoliki
2) Waprotestanti
3) Waislamu.

Mpambano ulikuwa zaidi kati ya Wakatoliki na Protestanti hasa Walutheri. Kwa upande wa waislamu wao hawakuwa na mzuka sana wa kidini katika huu mchuano, hawa unaweza kusema ni kama kundi la " Undecided" yaani wangepigia yoyote tu.

Ukiangali kambi ya Wakatoliki ilikuwa ni BWM, JPM, na machinery nzima ya kanisa katoliki

Ukija upande wa Walutheri kambi yao iliongozwa na watu kama , EL, FAM, JM, FTS na machinery nzima ya kanisa la kilutheri, hawa walifikia hata kujiaminisha kuwa sasa ni zamu yao!

Ndugu yangu umeandika chini ya kiwango kuliko kawaida.Bila shaka wewe ni Jamii ile inayolalamika kuonewa na kutaka nafasi za upendeleo kila mara.Hata siku moja usidanganyike ukadhani Roman Catholic na Waprotestant wanabaguana kwenye mambo ya kitaifa.Tena wanaaminiana sana kuliko unavyofikiri.Hata sasa hivi huwezi kusikia hizi kelele eti wakatoliki wamechaguliwa wengi serikalini au waprotestant wamechaguliwa wengi Serikalini.Mara nyingi makanisa yote hayo yanaunganishwa na Kristo na kitabu chao ni Biblia.Msimamo wao mara nyingi ni mmoja kama walivyogomea Katiba Pendekezwa.
Jaribu tena kufanya utafiti.

Hata hivyo kanisa katoliki ni more powerful lina mtandao mpana zaidi na limeibuka kidedea!.

Sasa linajikita katika system kwa uimara zaidi, kuhakikisha maslahi yake yako intact kwa muda mrefu ujao!. Hata hivyo wawe makini kwa sababu jamii ikishaona aina ya inequalities, hiyo jamii haiwi inara, utaifa unakuwa katika hali fulani loose! Ni hatari sana.
 
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.

Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.

Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
As much as we hate to admit it, Hapa pana harufu kaali, kali sana ya Udini ulio kubuhu pamoja na Ukanda.
 
Waislam hawatakiwi kulalamika maana serikali ya awamu ya tano inawajengea ofisi kubwa ya bakwata na msikiti mkubwa Dar kama wakristo ndio wangefanyiwa hivyo mngelalamika sana
 
Lakini let's be fair. Kwanza nitamke wazi kuwa mimi ni mkristo. Pili nitamke wazi pia kuwa sifurahishwi na huu mwelekeo unaoonekana kwenye hizi teuzi. Haya mambo yalishaanza kukaa sawa, hisia za unyonge zilishaanza kuondoka, sasa tunarudi nyuma. Hakuna starehe yoyote unapopata kitu halafu wenzio wakasema umependelewa, kwa hiyo ili hizo hisia za upendeleo ziondoke ni lazima ionekane kuwa haki imetendeka, na hilo ndilo analopaswa kuzingatia kiongozi na wote wanaomshauri.
Siamini kuwa alishindwa kufanya balance, mbona wenzie waliomtangulia waliweza? Tangu enzi za Nyerere, tena hata wakati mwingine baadhi ya sifa alizifumbia macho kidogo ili kuwe na balance. Tena enzi ya Nyerere angelazimisha vigezo vya usomi angeweza kuteua hata wakristo 95% kwa sababu hali ya wakati ule wa baada ya ukoloni inaeleweka, wenzetu walikuwa wamebanwa zaidi, lakini alipokea ushauri na kutumia pia busara yake kujitahidi kuweka balance nchi ikaonekana ni yetu sote. Japo wenzetu baadaye walilalamika, lakini naona kama hii ya sasa mkuu huyu amebana kuliko awamu zote zilizotangulia.
Tumshauri au kumwomba awe msikivu, atazame raia wote kwa usawa. Pengine hajafanya makusudi, sina uhakika, lakini aelewe kuwa athari zinawafikia wote, hata sisi tunaodhaniwa tumependelewa hakuna tunachofaidi. Hata angeweka wakristo watupu serikali nzima, hakuna chochote ningefaidi, yaani hainifai kitu wakati kuna wenzangu, jirani zangu, classmates wangu, rafiki zangu wanakosa amani kwa sababu siku zote upendeleo una tafsiri mbaya. Atusaidie kuondoa hizi sensitivity, tunataka tuendelee kuishi kwa amani bila manung'uniko upande wowote, au hata yakitokea yawe ni yale ambayo kwa wazi kabisa yanaonekana hayana msingi, lakini kwa sasa huwezi kusema uwiano wa 137:16 au 185:36 (kama takwimu hizi ni sahihi) eti haina msingi wa kuhojiwa!

Jana tu wakati tunajadili ushindi wa Trump, rafiki yangu mwislam akaniambia "lakini wewe ni mkristo bwana huna neno, siye wenzio ndio hataki kabisa kutuona huko!" Kauli imeniuma sana maana binafsi sifaidiki chochote na chuki za Trump, na pia hata akiwachukia sana bado watabakia kuwa ndugu zangu na jamaa zangu, siwezi kuwatenga sababu eti Trump hawataki!

Tuwe makini na haya mambo yenye sensitivity. Ashauriwe vizuri mkuu wetu huyu. Natamani hata huyu sheikh awe na uthubutu wa kumfikishia mkuu huu waraka wake, na wakristo tuunge mkono kwa kusema kuwa hatutaki kupendelewa wala kudhaniwa tunapendelewa.

Acha porojo zako.Unaweza kuwa unaumia sana kwa sababu labda huelewi.
Manung'uniko ni sehemu ya maisha.Huwezi kumridhisha kila mtu.Yaani kwa akili yako unataka uongozi ugawanywe kama zawadi.Wanaolalamika ni wengi kuanzia Ombaomba,Maafa kagera,Wanafunzi,Wakulima,Wafanyakazi mishahara midogo,Daladala,Mipaka ya nchi na nchi mf.Malawi,Matokeo ya Uchaguzi,Wagonjwa n.k.
Kimsingi ni kuangalia malalamiko gani ni ya Msingi na kuyafanyia kazi.
Hili la kupewa vyeo vya upendeleo eti kwa sababu ni waislamu halina maslahi kwa taifa kwa sababu kila kabila nalo litataka lipewe upendeleo.
Mtu anachaguliwa kulingana na uwezo wake si kwa sababu anajua sana kuswalisha au kuhudhuria msikitini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom