afrodenzi
Platinum Member
- Nov 1, 2010
- 18,153
- 9,270
Kwa vile sikubali na wewe .Afrodenzi,
Huna uwezo wa kujadili mambo haya.
Na wewe pia huna uwezo.
Asante.
Kwa vile sikubali na wewe .Afrodenzi,
Huna uwezo wa kujadili mambo haya.
Afrodenzi,Kwa vile sikubali na wewe .
Na wewe pia huna uwezo.
Asante.
Mlete mada umeileta vizuri kweli kweliKwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.
Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.
Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.
Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.
Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.
Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.
Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.
Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?
Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.
Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.
Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.
Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
Kama unalijua hilo kwanini iwe bahati mbaya ya kuteuliwa wakristo pekee?Kwani wameteuliwa ili wakafaye ibada au watumikie taifa? Msipende kuongea vitu kwa hisia Bali angalieni tija hakuna dini kwenye selikari ya Tanzania
Mpangawangu,
Tatizo hili ni la muda mrefu sana.
Msome Mwalimu Nyerere anasema nini kuhusu tatizo hili:
''Tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam. Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo. Wazee hawa wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru. Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru. Nyerere alisema kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:
Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo. Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho. Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo. Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.[1]''
Hapo chini ni uchambuzi wangu ambao upo katika kitabu cha Abdul Sykes:
Hotuba hii ilikuwa ya ulaghai. Ukweli ni kuwa miongo mitatu baada ya uhuru Waislam hawajanufaika chochote wako katika hali ile ile aliyowaacha wakoloni au mbaya zaidi. Sivalon (1992) amefichua kuwa Kanisa limeweza kujenga himaya yake ambayo inahodhi 75% ya viti katika Bunge la Tanzania. Kati ya viti hivyo 70% vipo mikononi mwa Wakatoliki na vilivyobaki vimegawika kati ya Waislam na Wakristo wa madhehebu nyingine.[1] Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingedhirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali.''
sawa mkuu,nimekusomaIparamasa,
Fånya umwelewe vizuri.
Huyo si "kanyangarakata," wala "kajamaa."
Pengine wewe na mfano wa wewe hamuwezi hata kumbebea makubazi yake.
sasa mmejaaa wakatoliki na kanda ya ziwaSheikh anataka kama ilivyo NSSF jinsi yule Dr. Dau alivyofanya au? Maana pale wamejaa wa upande wa dini ile tu, kama ilivyokuwa TRA walijaa wa K'njaro tu. Zama hizo zimepitwa na wakati.
Kwa sababu za kihistoria katoliki wametawala tangu Uhuru na wataendelea sana kutawalaUchaguzi ule, ukiwa unayaangalia mambo kwa upana zaidi utaona kuwa ulikuwa ni mchuano wenye Factors nyingi, kwa jinsi ninavyoona, factor mojawapo ni Udini. Kulikuwa na kambi kuu tatu
1) Wakatoliki
2) Waprotestanti
3) Waislamu.
Mpambano ulikuwa zaidi kati ya Wakatoliki na Protestanti hasa Walutheri. Kwa upande wa waislamu wao hawakuwa na mzuka sana wa kidini katika huu mchuano, hawa unaweza kusema ni kama kundi la " Undecided" yaani wangepigia yoyote tu.
Ukiangali kambi ya Wakatoliki ilikuwa ni BWM, JPM, na machinery nzima ya kanisa katoliki
Ukija upande wa Walutheri kambi yao iliongozwa na watu kama , EL, FAM, JM, FTS na machinery nzima ya kanisa la kilutheri, hawa walifikia hata kujiaminisha kuwa sasa ni zamu yao!
Hata hivyo kanisa katoliki ni more powerful lina mtandao mpana zaidi na limeibuka kidedea!.
Sasa linajikita katika system kwa uimara zaidi, kuhakikisha maslahi yake yako intact kwa muda mrefu ujao!. Hata hivyo wawe makini kwa sababu jamii ikishaona aina ya inequalities, hiyo jamii haiwi inara, utaifa unakuwa katika hali fulani loose! Ni hatari sana.
Hujaribiwi ila unaambiwa ukweliSijaribiwi ........
Ni mkiristo yule mm namjua tangu ni mkuu wa wilaya uramboWaziri Mkuu ni muislam ila mkewe ni Mkristo
Alivyoapa aliinua juu Biblia?
Takwimu zako zinakupa picha ya uhaba wa fikra,kwa nafasi gan mpka walio na elimu ni wakristo waislam hawapo?hili jambo lipo wazi kbsa ishu sio utendaj ishu maagzo.Swala siyo Udini, Swala ni shule. Fanya sampling ndogo tu Angalia sasa hivi hata kwenye majina ya wahitimu wa shule za msingi na sekondari. Chunguza hayo majina mengi ni ya Dini gani? Halafu rudi kwenye takwimu, wakristo na waislam wapi ni wengi? Watu wamekaa kuchunguza udini Bila hoja za Msingi.